TAARIFA KWA UMMA
UTEKELEZAJI WA MALIPO YA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI WA KITURUKI WA
MKANDARASI WA SGR, YAPI MERKEZI
Dar es Salaam, Tarehe 21 Agosti 2023
Kampuni ya YAPI MERKEZI inayofanya ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa (SGR) kati ya Dar es salaam Isaka inaitaarifu umma kuwa imetatua changamoto ya malipo ya wafanyakazi wa kituruki wanaoshiriki kwenye ujenzi wa reli ya SGR chini ya Mkandarasi wa Kampuni ya Yapi Merkezi kuanzia tarehe 18.8.2023 na inaendelea kutekeleza kutatatua changamoto yeyote itakayojitokeza.
Kampuni ya YAPI MERKEZI inahakikisha kuwa, utekelezaji wa mradi wa SGR unaendelea vema na wafanyakazi wote wa kituruki wamerudi kuendelelea na majukum ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya SGR na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Kampuni ya YAPI MERKEZI inaomba radhi kwa Umma na Raia wa Kigeni wanaoshiriki kwenye Mradi wa ujenzi wa Reli ya SGR kutokana na changamoto iliyojitokeza hivi karibuni.
Soma pia:
Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa
Kampuni ya YAPI MERKEZI inaishukuru Serikali ya Jamhuri ya muunganano wa Tanzania kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kuweza kushirikiana katika kazi pamoja na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza na kuhakikisha mradi wa ujenzi wa Reli ya SGR unatekelezwa na kukamilika kwa wakati.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Amisa Juma