ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 617
- 1,542
Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo pamoja na mgombea mwenza Profesa Omar Hamad leo Agosti 7, 2020, wamechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za NEC Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe katika Ofisi za NEC Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 7,2020, kushoto ni Mgombea Mwenza, Prof. Omar Faki Hamad . Chama hicho kinakuwa cha nane kuchukua fomu.
====
TAARIFA KWA UMMA
MEMBE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Mgombea Urais wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ndugu Bernard Kamilius Membe leo tarehe 7, Agosti 2020 amechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Membe amekabidhiwa fomu hiyo ya uteuzi na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage Jijini Dodoma.
Katika uchukuaji huo wa fomu, Membe aliambatana na Mgombea mwenza wake, Profesa Omary Fakih Hamad.
Aidha msafara huo wa Membe uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu, Ndugu Ado Shaibu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Ndugu Mhonga Said Ruhwanya, Katibu wa Mambo ya Nje Ndugu Bonifasia Mapunda, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Ndugu Janeth Rithe, Katibu wa Ngome ya Vijana Ndugu Mwanaisha Mndeme na viongozi wengine waandamizi wa Chama.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Ndugu Bernard Membe amesema kuwa amejiandaa kufanya kampeni kabambe kila Kona ya nchi ili kuipatia ACT Wazalendo ushindi mnono na kuhakikisha ifikapo tarehe 28 Oktoba 2020, utawala wa Rais Magufuli unafikia tamati.
Imetolewa na:
Janeth Joel Rithe
Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
Imetolewa leo tarehe 07 Agosti 2020.