Mgombea Udiwani wa CCM atekwa usiku wa kuamkia leo

Mhakiki

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,384
2,100
Ni mgombea udiwani kupitia CCM wa kata ya MASUMUNI Jimbo la MBINGA MJINI ndugu LAURENT VITUS GOMANI AMETEKWA na watu wasiojulikana USIKU wa kuamkia leo.

Watu hao wapatao wanne walifika majira ya saa sita USIKU wakiwa na slaha 2 na kujitambulisha kuwa wao NI Askari polisi.

Ndugu GOMANI aligoma kufungua milango kwa sharti kuwa NI LAZIMA awepo balozi wake na majirani NDIPO atafungua mlango.

Baada ya mabishano hayo wahalifu hao walivunja milango na kuingia ndani wakamchukua na kutokomea naye kusikojulikana. Juhudi za kuwasiliana na polisi zilifanyika lakini polisi walikana kumshikilia. Hadi Sasa hakuna MTU anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo na diwani mtarajiwa hajulikani alipo.

Haya yametokea muda mfupi baada ya kutangazwa majina ya wapeperusha bendera wa CCM.

Asubuhi ya leo baada ya taarifa hizi kusaambaa WANANCHI wenye hasira Kali chupu chupu wachome nyumba ya aliyekuwa diwani anayemaliza muda wake wakimtuhumu kuhusika na tukio hio kwani na yeye anautaka Tena udiwani ingawa hakubaliki.Wananchi hao walitulia baada ya kutulizwa na wenyeviti wao wa mitaa.

Chanzo: Nilikuwepo polisi, nyumbani kwa mgombea wa Sasa na nyumbani kwa diwani aliyemaliza muda wake.
 
Simba akizoea kula nyama siku akikosa anamla binadamu
Hapana hii ni tofauti kiodogo, simba hamli simba hata akiwa na njaa kiasi gani. Hiyo ni tabia ya fisi...awe na njaa halafu amwone mwenzake anapangusa mdomo baada ya shibe! Huyo atapata taabu sana kama hakuliwa. Tunachokosea Watanzania ni kukabidhi hatma ya taifa letu mikononi mwa fisi! Na cha kusikitisha zaidi ni kwamba hatujifunzi...akitoka fisi huyu tunamkabidhi ndugu yake.
 
Back
Top Bottom