Mgogoro wa Zanzibar usuluhishwe na Koffi Annan na Luis Ocampo

....kama watu wamepingwa na dunia nzima kuhusu kufuta matokeo na kurudia uchaguzi lakini hawakusikia....sitegemei watakubali wapatanishi wa nje..tena watasema mgogoro ni wa ndani na hivyo hakuna haja ya wapatanishi wa nje....mawazo/utashi wa watawala kuhusu hatma ya zenj unawategemea wao na wala si wazanzibar waliopiga kura zikafutwa....nafananisha utashi huu kibri na ule wa mukurunziza wa Burundi kukataa vikosi vya amani toka AU....ni utashi wa watu katili...
 
..au, unafikiri Marekani anapaswa kuchukua hatua sasa hivi, au asubiri mpaka mambo yanaelekea kuwa mabaya, au yawe mabaya?
.

Marekani alishaathiriwa sana na Wapemba.Au mnafikiri kasahau kuwa waliolipua ubalozi wa marekani walitokea wapi? Anaijua pemba mmarekani kuliko unavyoijua wewe.Usidhani aweza kuingizwa kichwa kichwa .Anawajua UAMSHO NI kina nani na chaka lao liko wapi.Pemba inajulikana kama hujui.Anawajua wamwagia tindikali watu,wachoma makanisa na ndugu wa Alshababu na siasa kali kuwa kwao makao makuu kule zanzibar ni wapi.

Anawajua waua mapadri kule Zanzibar ni kina nani pia.
 
Nakubaliana na mapendekezo ya Balozi Mpungwe kwamba ndugu zetu wa Znz wanahitaji mpatanishi ili kuwasuluhisha kutokana na mgogoro wao wa kihistoria na kisiasa.

Kama kuna watu wanaopaswa kusikilizwa basi ni Balozi Mpungwe. Huyu alikuwa kati wa washiriki wakuu wa mazungumzo ya amani ya Rwanda yaliyozaa mkataba unaoitwa Arusha accord. Kwa hiyo ni mtu mwenye uzoefu.

Lakini sikubaliani na Balozi Mpungwe anaposema tuwatumie wazee wastaafu wa hapa Tanzania. Wastaafu tulio nao wenye hadhi ya kutatua mgogoro huo wote ni wanachama wa CCM. Hiyo inawaondolea sifa kuu kwamba msuluhishi wa mgogoro wowote ule ni lazima aaminike na pande zote na asiwe na historia ya mahusiano ya karibu na upande mmoja ktk mgogoro anaotarajiwa kuusuluhisha.

Kwa kuangalia hapa Afrika na hata nje ya Afrika, nadhani Koffi Annan na Luis Moreno-Ocampo wanaweza kuwasaidia ndugu zetu wa Zanzibar kuondoka ktk mkwamo wa kisiasa na kijamii unaondelea nchini kwao.

cc Kakke, Foum Jnr, Nguruvi3, The Boss, ZeMarcopolo, Mohamed Said, crabat, Nonda, Kapwela, Ritz, MsemajiUkweli

Kafie mbele huko Zanzibar ni sehemu ya JMTZ hivyo matatizo ya Zanzibar ni sehemu ya matatizo yetu na tutayatatua sisi wenyewe ni kama kusema Mbeya kuna tatizo basi aje sijui takataka Anani au Okampo nasema fvck wewe, Anani wako na takataka mwingine Okampo sijui!
 
..Duh!!

..sijawahi kushuhudia umetibuka kiasi hiki.

..lakini bila shaka unakubaliana na mimi kwamba kuna tatizo Znz.

..sasa toa maoni yako ni jinsi gani tutaondoka ktk huu mkwamo na mgogoro wa muda mrefu Znz.
 
JokaKuu ninakataa utartibu wa suluhu kwasababu unaonekana kuchukua nafasi ya sheria na haki.

Kwa mfano utaratibu wa kubabaisha umelikumba jiji la Dar pia.

Hakuna tatizo, linatengenezwa tatizo tena chini ya ofisi ya Rais.
Tunahitaji msuluhishi kwa hili pia?

Kulekea uchaguzi ZNZ hakuna kanuni, sheria au utaratibu unaosema 'wana mapinduzi' watashinda tu. CCM walikubali kuingia katika kinyng'anyiro, wakanadi sera na kila kitu

Hakuna aliyelalamika kuhusu uchaguzi isipokuwa Jecha ndiye analalamika
Washindi walitangazwa wakapewa vyeti, Jecha akafuta

Huu ni utamaduni wa kutumia maguvu kushinda, hautushawishi kutafuta usuluhishi

Endapo Mapinduzi ndicho kigezo, CCM Taifa wajitokeze na kusema iwepo sheria kuwa wana mapinduzi watatawala daima

Kualika wasuluhishi ni kuwatwisha mzigo usio na maana. Yaani tumeshindwa kuhesabu kura? Hakuna tatizo jingine, ni kukataa kujumlisha hadi mwisho.

Hakuna tatizo jingine ni Jecha kuchukua jukumu la tume. Tunahitaji msuluhishi kweli?

Balozi alikuwa wapi hadi anataka kulifanya tatizo la kutangaza ni tatizo la kihistoria.

Hakukemea haya anakuja na suluhu, suluhu gani inatafutwa bila kueleza kiini cha tatizo?

Mapinduzi hayana maana ya ubwana. Ikiwa ni hivyo alikuwepo sultan kwanini aliondolewa?

Mapinduzi yalilenga kumkomboa mzanzibar, kutoa haki sawa na kuleta heshima kwa wote

Leo hakuna haki, hakuna usawa na ubaguzi ni hadharani kuliko wakati wa Sultani

Bado tunaamini mapinduzi yana maana wakati maana nzima inasiginwa tukiangalia
 
Timing ni muhimu. Zanzibar wamekuwa na majidiliano ya miaka mingi na hata kuwa na muafaka wa kisiasa lakini bado misukosuko imekuwa inajirudia. Kwa maoni yangu muda wa kupata suluhu ya kudumu bado haujafika, bado kuna miaka mingine kama 20 ili Zanzibar iwe kwenye njia ya kupata mwafaka wa kudumu. Watu walipoteza maisha (1964) kwa ajili ya Mapinduzi na baadhi yao wangali hai, leo hii unamwambiaje agawane madaraka na nani? Kizazi kijacho kinaweza kuwa na nafasi nzuri ya kupatana na lakini sio sasa.
Kwani tukobkatika mfumo gani wa kisiasa .unachekesha sana
 
Swahib kumbe umetufahamu.. Uzuri wa uchaguzi mkuu wa oct 2015 tumedhihirisha beyond any reasonable doubt kwamba wazanzibari walio wengi hawakubaliana na mengi yanayofanywa na zaidi wamefungwa mikono katika kufanya maamuzi. Mkoloni kwa sasa ni ccm na ni katili zaidi ya mkoloni aliepita, ma kinachowapa nguvu ni jeshi la jamhuri ya muungano pamoja na mkuu wa nchi, anaeamini ataongoza malaika siku ya ufufuo huku akikosa hata hamu ya kusimami haki anayohubiri upande wa pili.

Haki itasimama, iko siku.

JokaKuu ninakataa utartibu wa suluhu kwasababu unaonekana kuchukua nafasi ya sheria na haki.

Kwa mfano utaratibu wa kubabaisha umelikumba jiji la Dar pia.

Hakuna tatizo, linatengenezwa tatizo tena chini ya ofisi ya Rais.
Tunahitaji msuluhishi kwa hili pia?

Kulekea uchaguzi ZNZ hakuna kanuni, sheria au utaratibu unaosema 'wana mapinduzi' watashinda tu. CCM walikubali kuingia katika kinyng'anyiro, wakanadi sera na kila kitu

Hakuna aliyelalamika kuhusu uchaguzi isipokuwa Jecha ndiye analalamika
Washindi walitangazwa wakapewa vyeti, Jecha akafuta

Huu ni utamaduni wa kutumia maguvu kushinda, hautushawishi kutafuta usuluhishi

Endapo Mapinduzi ndicho kigezo, CCM Taifa wajitokeze na kusema iwepo sheria kuwa wana mapinduzi watatawala daima

Kualika wasuluhishi ni kuwatwisha mzigo usio na maana. Yaani tumeshindwa kuhesabu kura? Hakuna tatizo jingine, ni kukataa kujumlisha hadi mwisho.

Hakuna tatizo jingine ni Jecha kuchukua jukumu la tume. Tunahitaji msuluhishi kweli?

Balozi alikuwa wapi hadi anataka kulifanya tatizo la kutangaza ni tatizo la kihistoria.

Hakukemea haya anakuja na suluhu, suluhu gani inatafutwa bila kueleza kiini cha tatizo?

Mapinduzi hayana maana ya ubwana. Ikiwa ni hivyo alikuwepo sultan kwanini aliondolewa?

Mapinduzi yalilenga kumkomboa mzanzibar, kutoa haki sawa na kuleta heshima kwa wote

Leo hakuna haki, hakuna usawa na ubaguzi ni hadharani kuliko wakati wa Sultani

Bado tunaamini mapinduzi yana maana wakati maana nzima inasiginwa tukiangalia
 
Hakuna msuluhishi mwenye nguvu zaidi ya wale wenye jeshi na linalowapa nguvu Jecha na genge lake kufanya wanayoyataka. Jecha ni nani hasa aweze kufanya alichokifanya kama si sababu ya jeshi na mkuu wake aliena bias latika maamuzi yalio na haki?

Kama wasuluhishi wangapi wamekuja na mbona hakujawa na chochote, kulikuwa na Chief Anyauku alieleta muafaka mwaka 1995 - 2000 tukamshangiria na kumtunuku hata uraia lakini alipooondoka tu tukafanya makubwa zaidi ya kuwauwa watu 27 walipodai haki yao ya kujiendesha. Hivi Rais wa Zanzibar anauwezo hasa wa kufanya yanayofanyika bila ya ridhaa na baraka kutoka kwa mkuu wa jamhuri hasa katika masuala ya polisi na jeshi?

Ukitaka kuifahamu mentality na kilichopangwa na ccm bara na Zanzibar ni kimoja tu, hawako tayari kukubali maamuzi ya wazanzibari kiasi kwamba wamekuja na kelele mpya kwamba chaguzi za mbele zisitowe Rais kutoka upinzani na iwe haki ya ccm pekee. Hukusikia hata ccm kuikana kauli hii ya kiongozi wake atakae kuwa katika cabinet inayofuata na atakaepeleka hoja katika baraza la wawakilishi la mabadiliko ya katiba itakayoridhia ufalme wa ccm zanzibar.

ukweli naona kwa zanzibar hakuna haja ya vyama vingi, vyama vingi ni mateso kwa wananchi hasa wanapoitikia haki ya demokrasia ya kutaka mabadiliko. Dunia hii zipo nchi mpaka leo zisizofuata mfumo wa vyama vingi, zanzibar haitakuwa ya mwanzo nafikiri watawala kipindi hichi cha wenyewe kwa wenyewe 100% wajiandae kubadilisha katiba ikidhi haja zao za utukufu na ufalme walioupindua kumbe kwa kuyatamani wao wenyewe.

Zaidi la kufurahisha ni kwamba tulikubali maridhiano ya 2010 na kukubali kuwa sehemu ya serikali kwa sababu ya kujenga mazingira mema ya demokrasia lakini tulipigwa vita tukaitwa ccm b, wapenda vyeo na maneno mengi. Leo tumedhihirisha kwamba ile ilikuwa ni gesture of goodwill na sio rushwa ya kuzuia haki ya wananchi ya kubadili uongozi.

Miaka mitano si mingi, iko siku tutavuna tunachopanda, na hakuna atakaesalimika. Tumeona duniani matatizo makubwa ni kukata tamaa kwa wananchi katika demokrasia na athari zake ni mbaya sana. Mungu asitufikishe huko.
 
Nakubaliana na mapendekezo ya Balozi Mpungwe kwamba ndugu zetu wa Znz wanahitaji mpatanishi ili kuwasuluhisha kutokana na mgogoro wao wa kihistoria na kisiasa.

Kama kuna watu wanaopaswa kusikilizwa basi ni Balozi Mpungwe. Huyu alikuwa kati wa washiriki wakuu wa mazungumzo ya amani ya Rwanda yaliyozaa mkataba unaoitwa Arusha accord. Kwa hiyo ni mtu mwenye uzoefu.

Lakini sikubaliani na Balozi Mpungwe anaposema tuwatumie wazee wastaafu wa hapa Tanzania. Wastaafu tulio nao wenye hadhi ya kutatua mgogoro huo wote ni wanachama wa CCM. Hiyo inawaondolea sifa kuu kwamba msuluhishi wa mgogoro wowote ule ni lazima aaminike na pande zote na asiwe na historia ya mahusiano ya karibu na upande mmoja ktk mgogoro anaotarajiwa kuusuluhisha.

Kwa kuangalia hapa Afrika na hata nje ya Afrika, nadhani Koffi Annan na Luis Moreno-Ocampo wanaweza kuwasaidia ndugu zetu wa Zanzibar kuondoka ktk mkwamo wa kisiasa na kijamii unaondelea nchini kwao.

cc Kakke, Foum Jnr, Nguruvi3, The Boss, ZeMarcopolo, Mohamed Said, crabat, Nonda, Kapwela, Ritz, MsemajiUkweli
hakuna mpatanishi wala nini fitina mkubwa ni Tanganyika ndie anaye chocheya kwa kupinduwa demokrasi kwa majeshi
 
..baadhi ya waliokuwa wakiwaita ccm b juzi walikuwa wakishangilia ushindi wa umeya wa Dsm kwa kuimba "Maalim Seif..Maalim Seif.."!!

..hata wa-Tgk na sisi tumeanza kuuelewa mgogoro wa Znz. Ni bahati mbaya tu imetuchukua muda mrefu kufahamu nani haswa anayewakwamisha wa-Znz.
 
hakuna mpatanishi wala nini fitina mkubwa ni Tanganyika ndie anaye chocheya kwa kupinduwa demokrasi kwa majeshi

..siyo wote.

..ukiwalundika wa-Tgk wote ktk kundi moja utakuwa unakosea.

..hivi hujaona wabunge wa ki-Tgk wakigomea hotuba ya Raisi Magufuli bungeni kwasababu Dr.Shein alikuwepo pale?

..wa-Znz mnakosea kuwalaumu wa-Tgk ktk ujumla wao. Jaribuni kutoa ELIMU ya nini kinachoendelea huko kwenu. Nina hakika mkifanya hivyo wapo wa-Tgk wengi watawaelewa na kuwaunga mkono.
 
Nakubaliana na mapendekezo ya Balozi Mpungwe kwamba ndugu zetu wa Znz wanahitaji mpatanishi ili kuwasuluhisha kutokana na mgogoro wao wa kihistoria na kisiasa.

Kama kuna watu wanaopaswa kusikilizwa basi ni Balozi Mpungwe. Huyu alikuwa kati wa washiriki wakuu wa mazungumzo ya amani ya Rwanda yaliyozaa mkataba unaoitwa Arusha accord. Kwa hiyo ni mtu mwenye uzoefu.

Lakini sikubaliani na Balozi Mpungwe anaposema tuwatumie wazee wastaafu wa hapa Tanzania. Wastaafu tulio nao wenye hadhi ya kutatua mgogoro huo wote ni wanachama wa CCM. Hiyo inawaondolea sifa kuu kwamba msuluhishi wa mgogoro wowote ule ni lazima aaminike na pande zote na asiwe na historia ya mahusiano ya karibu na upande mmoja ktk mgogoro anaotarajiwa kuusuluhisha.

Kwa kuangalia hapa Afrika na hata nje ya Afrika, nadhani Koffi Annan na Luis Moreno-Ocampo wanaweza kuwasaidia ndugu zetu wa Zanzibar kuondoka ktk mkwamo wa kisiasa na kijamii unaondelea nchini kwao.

cc Kakke, Foum Jnr, Nguruvi3, The Boss, ZeMarcopolo, Mohamed Said, crabat, Nonda, Kapwela, Ritz, MsemajiUkweli
hakuna mgogo zanzibar ila kuna ubishi tu. watu wana asili ya kudhani lazima watawale huku siku zote kura hazitoshi. sasa akija huyo annan mtamwambia mgogoro ni nini? maana uchaguzi wamesusa ila madaraka wanataka, sasa bila uchaguzi wanapataje madaraka!! urais sio kwa zamu ila kwa ridhaa halali ya wananchi. mtu anajitangaza rais halafu anadai kuapishwa..hiyo ndio demokrasia gani?
 
..cuf nao wanadai ccm hawajawahi kushinda uchaguzi Znz toka mwaka 1995.

..wanadai kila unapofanyika uchaguzi ccm inapora ushindi kwa kusaidiwa na wanajeshi toka Tanganyika.

..wamesusa uchaguzi kwasababu waanamini walishinda uchaguzi wa October na Jecha akawapora ushindi.

..pendekezo lingine ni uchaguzi wa Znz kusimamiwa na TUME YA KIMATAIFA.
 
ok,.. wangedai uangalizi wa kimataifa tight. wangetaka jicho la ulimwengu kuja zanzibar kushuhudia kwa mara ya pili katika uchaguzi mmoja wanadhulumiwa. hilo hawajathubutu kudai ila tu 'sitaki sitaki' nataka kuapishwa, wakati lazima utangazwe kushinda na mamlaka ndio uapishwe. wao seif kajitangazia halafu anadai mamlaka imuapishe..teh teh
 
..mambo yote mabaya unayowatuhumu cuf yanafanywa pia na ccm.

..mazingira hayo ndiyo yaliyonisukuma mimi kupendekeza mgogoro huu ushughulikiwe na msuluhishi wa kimataifa asiyeegemea upande wowote.

..mgogoro huu unaleta taswira mbaya kwa nchi yetu. mimi ningependa awamu hii isiwe na makando-kando kama haya ya Znz ile tuelekeze nguvu zetu zote ktk kujijenga kiuchumi.
 
Back
Top Bottom