kichongeochuma
JF-Expert Member
- Jan 21, 2024
- 1,655
- 2,826
Polisi anakukamata huna kosa au kwa kosa la kuhisiwa tu, ukianza kuhoji kuna nini anakukamata bila sababu, unatandikwa haswaa, unafika Kituoni.
Unaambiwa saini hapa ukiuliza kwanini mbona sielewi na saini nini? Unapigwa haswa, na baada ya hapo unawekwa ndani, kisha ndugu wakija wanaambiwa hawezi kutokae huyu akae kwanza siku 10 si anajifanya mjuaji anajua sheria tuone sasa, na mkija bila laki 4 hatoki milele
Baada ya siku 4 ndugu wanalia kuomba msaada utoke anaambiwa atoe laki 6, ndugu wanajichanga wanatoa laki 6 mtu anatoka akiwa kaumizwa na majeraha mengi mwilini ambayo kapigwa bila kosa.
Jeshi hili ni la kionezi kwa raia libadilishiwe muundo wake wa utendaji kazi, kwa jinsi ilivyo sasa Polisi yuko juu sheria na hasa kwa raia ambao hawana watetezi.
Wananchi hawa wa kawaida wananumizwa na kuteswa sana hiki chombo yani Polisi wakiwa na shida na pesa tu wanatafuta sababu ya kukamata raia na kuwatoza fedha nyingi bila kosa na hawataki kuhojiwa ukowahoji unapigwa haswa
Hiki chombo si rafiki kwa raia si msaada kwa raia kabisa na raia akinyanyaswa hakuna mamlaka ya kukiwajibisha hiki chombo, polisi wabadilishiwe namna ya kutekeleza kazi zao na kama ilivyo hivi sasa.