Mfumo wa elimu uwe wa kikanda kutokana na fursa za kiuchumi wa eneo husika

Mende mdudu

Member
Feb 13, 2023
32
70
Niende moja kwa moja kwenye mada kutokana na uwepo wa degree nyingi mtaani bora kuwe na mfumo mpya wa elimu kutokana na kanda husika kutoka primary hadi high level.

Kwa mfano watu wa Mwanza wawe na silabasi yao inahusu uvuvi na uchumi wa blue toka shule ya msingi kama usafirishaji wa majini kutuza samaki kufuga mwenyewe kwa kutengeza mabwawa nk.

Kwa watu wa Arusha mnawafundisha utalii toka primary ata ingewezekana wangejua faidi za utalii wasinge goma kuhama mbugani, tena awa english kwao wangeanza nayo toka primary mnawapa na elimu ya utalii

Watu wa ukanda wa Dar elimu silabac inakua katika ujasiamali kutokana na kua jiji la bishara toka primary mtoto anaandaliwa kujua fursa katika jamii kama mjasiriamali ivo ivo kwa mikoa mingne

Kuliko kumkalilisha mtoto panzi ana miguu mingapi , au juma anamika flani eda ana mara mbili ya umri wa baba .

Bado hatujachelewa ili kuondoa wimbi la kulalamika watu kukosa ajira na kujiandaa kujiajiri akimaliza masomo

Uchumi kama taifa ungekua na kwa mtu mmoja mmoja.
 
Back
Top Bottom