KERO Mfereji wenye maji yenye kinyesi unatumiwa kumwagilia bustani za mbogamboga Kibaha Maili Moja, Wataalamu wetu mko wapi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ni hatari tupu! Ukifika Kibaha Maili Moja njia panda ya kwenda Ofisi za Mkuu wa Mkoa, utaona kuna bustani ya miche ya miti na maua mbalimbali, pembeni yake kuna boda boda, ukifika walipo bodaboda utakutana na harufu nzito, hapo kuna mfereji uliochepushwa kutokea vilipo vyoo vya soko la Maili Moja stendi ya zamani.

Maji machafu kutoka chooni yameachiwa kupitia karavati dogo la hapo hata pasipo kuambiwa na mtu, ukifika utaona tu kuwa hiki ni kinyesi. Mbaya zaidi yale maji machafu yanatiririka kuelekea ulipo mfereji mkuu na wakulima wa mboga wanayatumia kumwagilia mboga mboga!

Swali langu Ofisi ya Bwana Afya wa Wilaya na Kata siku hizi kazi zake ni zipi? Zamani kulikuwa na patroo nyumba kwa nyumba kukagua hali ya usafi, siku hizi hakuna! Kama kuna kiongozi yeyote eneo hili tajwa ameona bandiko hili, mara moja akatatue hii kero!

Mtatuua na mnatuua kwa uzembe wenu!
Kwan si mbolea ??? au
 
Sinza tu hapo chemba ilikuwa inamwaga vinyesi wazi wazi... Kariakoo nako week mbili zilizopita nilikuwa hapo Mavi nje nje chemba zimefurika hatariii
Hii nchi ni Mungu tu anatulinda Ila ni shida
 
Sinza tu hapo chemba ilikuwa inamwaga vinyesi wazi wazi... Kariakoo nako week mbili zilizopita nilikuwa hapo Mavi nje nje chemba zimefurika hatariii
Hii nchi ni Mungu tu anatulinda Ila ni shida
Ukute kwenye hio chemba ya sinza, kimba la Lucas mwashambwa nalo lipo humo
 
Afadhali umelisema hili na mm niondoe dukuduku langu.Tuache kibaha tuje bongo,jiji la mchongo unakuta mboga nzuri kijani Hadi inataka kuwa nyeusi,Utaskia wakisifia hii ndio mboga tena haitakiwi ichemshwe sana kumbe imelimwa na kukuzwa na kinyesi na maji yakiwanda Cha urafiki.Jiulize bongo maji dumu mia 2 pengine buku maeneo kibao maji hamna ndio wapate ya kumwagilia mboga?
 
Wachina wachafu sana. Humo kuna mavipindupindu, mataifodi, ma amoeba, ma minyoo ma tetenus na magonjwa mengine kibao kibao. Mbolea ya binadamu haifai kwa mbolea, na nchi zingine ukitaka kutumia mbolea ya wanyama lazima uichome na utumie majivu yake.
Sasa hao jamaa walikuwa wanaiweka kama ilivyo
 
Daaaaaaah mbona Dar kuhusu Vinyesi ni kama Samaki na Maji?, lakini mboga hizo zinazomwagiliwa kwa maji ya vinyesi nafikili hazina madhara endapo baada ya kuchumwa zinaoshwa vizuri na kupikwa.
 
Back
Top Bottom