Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,432
- 3,498
Ni hatari tupu! Ukifika Kibaha Maili Moja njia panda ya kwenda Ofisi za Mkuu wa Mkoa, utaona kuna bustani ya miche ya miti na maua mbalimbali, pembeni yake kuna boda boda, ukifika walipo bodaboda utakutana na harufu nzito, hapo kuna mfereji uliochepushwa kutokea vilipo vyoo vya soko la Maili Moja stendi ya zamani.
Maji machafu kutoka chooni yameachiwa kupitia karavati dogo la hapo hata pasipo kuambiwa na mtu, ukifika utaona tu kuwa hiki ni kinyesi. Mbaya zaidi yale maji machafu yanatiririka kuelekea ulipo mfereji mkuu na wakulima wa mboga wanayatumia kumwagilia mboga mboga!
Swali langu Ofisi ya Bwana Afya wa Wilaya na Kata siku hizi kazi zake ni zipi? Zamani kulikuwa na patroo nyumba kwa nyumba kukagua hali ya usafi, siku hizi hakuna! Kama kuna kiongozi yeyote eneo hili tajwa ameona bandiko hili, mara moja akatatue hii kero!
Mtatuua na mnatuua kwa uzembe wenu!