BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,820
Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daud Msasi ametaja sababu kuwa ni matumizi yasiyosahihi ya dawa ikiwemo kutomaliza dozi na kushirikiana dawa kwa wagonjwa bila maelekezo ya wataalamu.
Amesema matumizi holela ya dawa nchini yameongeza idadi ya vifo, ugumba na magonjwa ya figo huku homa za matumbo na UTI zikitajwa kuongoza kwa watu kutumia dawa bila utaratibu sahihi.
Ametaja pia uchache wa Wahudumu wa Afya nchini kuwa ni kati ya sababu zinazochangia wagonjwa kutopata maelezo sahihi ya dawa kutokana na watoa huduma kuelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa.