Steven mushi mushi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2016
- 533
- 739
- Thread starter
- #41
Faru pia miguu yao ina vidole vitatu vyenye kwato kwa kila mguu. Black rhino yeye anakuwa na nundu juu kidogo ya mabega wakati White rhino yeye hana nundu na staili yao ya ujamianaji ni polygynous( Dume kujamiana na jike zaidi ya mmoja) na majike wa faru wanakuwa na pembe fupi kuliko madume na wana matiti mawili. Na watoto wa faru huishi na mama yao kwa kwa zaidi ya miaka mitatu hadi hapo jike atakapopata tena ujauzito. Maadui wakubwa wa faru ni binadamu ambao huwaua kwa sababu ya pembe zao na Simba ambao huwinda watoto wao kwa ajili ya kitoweo. Ni wanyama ambao hupendelea kula hasahasa wakati wa asubuhi na jioni ambapo hula takribani aina 200 tofauti tofauti za mimea na wana uwezo mzuri wa kuona, kunusa pamoja na kusikia. Kwa upande wa Black rhino yeye hupendelea maeneo yenye vichaka na miti mifupi kwa sababu yeye ni mlaji wa juu katika matawi ya miti wakati White rhino yeye anapendelea maeneo ambayo ni plains kwa sababu yeye ni mlaji wa nyasi. Pia faru ni wanyama wanaowekewa ulinzi wa kutosha kuwakinga dhidi ya majangili na wanalindwa na askari wa wanyama pori (Park rangers ) kwa saa 24,