Mfahamu vyema mnyama Rhino (Faru)

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Jul 25, 2016
533
739
d8b2b7fe6381d1a97c259bb2c696dc8a.jpg
Faru kwa kiingereza anafahamika kama Rhino na kiswahili ni Faru na sio kifaru kama wengi wanavyomwita. Mnyama huyu anapatikana katika order inayojulikana kama PERISSODACTYLA na familia yake ni RHINOCEROTIDAE na jina lake la kisayansi ni DICEROUS BICORNIS kwa black rhino na White rhino jina lake la kisayansi anajulikana kama CERATOTHERIUM SIMUM.

Faru ni miongoni mwa wanyama ambao ni BIG FIVE kwa Africa, wengine ni chui, simba, mbogo na tembo. Kuna takribani aina tano za faru duniani na Africa tuna aina mbili za faru ambazo ni WHITE RHINO na BLACK RHINO na aina nyingine tatu silizobaki zinapatikana barani Asia, na kwa Tanzania sisi tuna aina moja tu ya faru ambayo ni Black rhino ingawa pia kuna white rhino wanaopatikana mkomazi ambayo ni introduced species waliochukuliwa kutoka South Africa.

Faru pia ni wanyama ambao wapo hatarini kutoweka duniani kutokana na kuwindwa sana na majangili kutokana na pembe zao ambazo zina thamani kubwa barani Asia na pembe hizi hutumika kutengenezea dagger pamoja na dawa maarufu ambayo hutumiwa na akina Baba kuleta heshima nyumbani (VIAGRA) ambayo ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume na wanaamini hivyo kutokana na huyu mnyama FARU kutumia mda mwingi wakati wa kujamiana ambapo anaweza kukaa mgongoni kwa jike kwa zaidi ya dakika 40.

Kutokana na kuwa na nguvu za kujamiana kwa mda mrefu watu wakafikiri kuwa nguvu zake zinatoka katika pembe kitu ambacho kimethibitishwa na wanasayansi kwamba si kweli kuwa pembe zake ndizo zimamsaidia kustahimili mda mrefu wakati wa kujamiana. Kwa kawaida faru ni wanyama ambayo huishi maisha ya mmoja mmoja (Solitary ) na dume na jike hukutana tu katika msimu wao wa ujamianaji ambapo kipindi hicho hutafutana kwa njia ya harufu ambayo hutolewa na jike pale anapokuwa anamuhitaji dume.

Anabeba ujauzito wake kwa kipindi cha miezi 18 na huwa anazaa mtoto mmoja ( Mapacha huwa ni nadra). Faru pia ni miongoni mwa wanyama wakubwa wanaopatikana nchi kavu ambapo anaweza kufikia hadi uzito wa 2000-2300KG kwa white rhino na 800-1500KG kwa black rhino.

Na tofauti kati ya Black rhino na White rhino ni kuwa ana mdomo mweusi uliochongoka ambao unamwezesha kula majani ya juu katika matawi ya mti (Browser) na white rhino yeye anakuwa na mdomo mpana mweupe kwa ndani ambao unamwezesha kula nyasi(Grazers), tofauti nyingine ni kwamba White rhino akiwa na mtoto huwa anatabia ya kumtanguliza mtoto mbele Kama wafanyavyo wamama wa kizungu ambao humbeba mtoto kwa mbele na kwa upande wa Black rhino yeye huwa mtoto anakaa nyuma ya mama kama wafanyavyo wamama wa kiafrica ambao huwabeba watoto wao mgongoni.

Na tofauti nyingine ni kwamba White Rhino ni mkubwa kuliko Black rhino. Na rhino huishi kwa kipindi cha miaka 30-50 na wanapendelea maeneo tambarare na yenye fichaka na kila mmoja huwa anamiliki eneo lake la himaya ambapo hutumia mkojo kuweka mipaka katika maeneo yao yaani hawa tunawaita territorial (Wanyama ambao humiliki maeneo ya himaya). Na kwa hapa Tanzania sehemu nzuri ya kuwaona hawa FARU ni NGORONGORO CRATER.
 
Huyo ndo faru na kadri nitakavyopata mda nitawaleteeni aina tofauti tofauti za wanyama na ndege ambao wanapatikana nchini kwetu Tanzania.

Anatisha mkuu mziki wake si kitoto na usiombe akasirike ukiwa na gari karibu yake lazima alichane yaani hawa jamaa ni very very aggressive
Nampenda huyu mnyama kwakuwa ma2c yake yanatumika kutengeneza Viagra
 
d8b2b7fe6381d1a97c259bb2c696dc8a.jpg
Faru kwa kiingereza anafahamika kama Rhino na kiswahili ni Faru na sio kifaru kama wengi wanavyomwita. Mnyama huyu anapatikana katika order inayojulikana kama PERISSODACTYLA na familia yake ni RHINOCEROTIDAE na jina lake la kisayansi ni DICEROUS BICORNIS kwa black rhino na White rhino jina lake la kisayansi anajulikana kama CERATOTHERIUM SIMUM.

Faru ni miongoni mwa wanyama ambao ni BIG FIVE kwa Africa, wengine ni chui, simba, mbogo na tembo. Kuna takribani aina tano za faru duniani na Africa tuna aina mbili za faru ambazo ni WHITE RHINO na BLACK RHINO na aina nyingine tatu silizobaki zinapatikana barani Asia, na kwa Tanzania sisi tuna aina moja tu ya faru ambayo ni Black rhino ingawa pia kuna white rhino wanaopatikana mkomazi ambayo ni introduced species waliochukuliwa kutoka South Africa.

Faru pia ni wanyama ambao wapo hatarini kutoweka duniani kutokana na kuwindwa sana na majangili kutokana na pembe zao ambazo zina thamani kubwa barani Asia na pembe hizi hutumika kutengenezea dagger pamoja na dawa maarufu ambayo hutumiwa na akina Baba kuleta heshima nyumbani (VIAGRA) ambayo ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume na wanaamini hivyo kutokana na huyu mnyama FARU kutumia mda mwingi wakati wa kujamiana ambapo anaweza kukaa mgongoni kwa jike kwa zaidi ya dakika 40.

Kutokana na kuwa na nguvu za kujamiana kwa mda mrefu watu wakafikiri kuwa nguvu zake zinatoka katika pembe kitu ambacho kimethibitishwa na wanasayansi kwamba si kweli kuwa pembe zake ndizo zimamsaidia kustahimili mda mrefu wakati wa kujamiana. Kwa kawaida faru ni wanyama ambayo huishi maisha ya mmoja mmoja (Solitary ) na dume na jike hukutana tu katika msimu wao wa ujamianaji ambapo kipindi hicho hutafutana kwa njia ya harufu ambayo hutolewa na jike pale anapokuwa anamuhitaji dume.

Anabeba ujauzito wake kwa kipindi cha miezi 18 na huwa anazaa mtoto mmoja ( Mapacha huwa ni nadra). Faru pia ni miongoni mwa wanyama wakubwa wanaopatikana nchi kavu ambapo anaweza kufikia hadi uzito wa 2000-2300KG kwa white rhino na 800-1500KG kwa black rhino.

Na tofauti kati ya Black rhino na White rhino ni kuwa ana mdomo mweusi uliochongoka ambao unamwezesha kula majani ya juu katika matawi ya mti (Browser) na white rhino yeye anakuwa na mdomo mpana mweupe kwa ndani ambao unamwezesha kula nyasi(Grazers), tofauti nyingine ni kwamba White rhino akiwa na mtoto huwa anatabia ya kumtanguliza mtoto mbele Kama wafanyavyo wamama wa kizungu ambao humbeba mtoto kwa mbele na kwa upande wa Black rhino yeye huwa mtoto anakaa nyuma ya mama kama wafanyavyo wamama wa kiafrica ambao huwabeba watoto wao mgongoni.

Na tofauti nyingine ni kwamba White Rhino ni mkubwa kuliko Black rhino. Na rhino huishi kwa kipindi cha miaka 30-50 na wanapendelea maeneo tambarare na yenye fichaka na kila mmoja huwa anamiliki eneo lake la himaya ambapo hutumia mkojo kuweka mipaka katika maeneo yao yaani hawa tunawaita territorial (Wanyama ambao humiliki maeneo ya himaya). Na kwa hapa Tanzania sehemu nzuri ya kuwaona hawa FARU ni NGORONGORO CRATER.
hivi kwenye big five kiboko hayumo? au ubig five unapatikanaje, nimeona kwenye listi yako kuna chui
 
Kuna yule mnyama ambaye ukipanda juu ya mti anakojoa then anakurushia mkojo....unawashwa mpaka unashuka mwenyewe....huyo ni faru??
huyo myama anaitwa karungu yeye......ni hatari sana uyo myama lazima uombe pooo akianza shughuli yake kwa mkojo huyo ni balaaaaa
 
hivi kwenye big five kiboko hayumo? au ubig five unapatikanaje, nimeona kwenye listi yako kuna chui
Kiboko hayupo kwenye Big five. Tunaposema Big five tunamaanisha ni wale wanyama watano Africa ambao walipewa jina hilo la big five na wale wawindaji wa zamani ambao walikumbana na wakati mgumu kuwawinda hawa wanyama. Na sababu nyingine inayopelekea hawa wanyama kuitwa Big five ni kwamba trophy zao zina thamani kubwa mfano meno kwa tembo, pembe kwa faru na ngozi kwa chui na simba pamoja na sifa za ukorofi na ubabe alizonazo mbogo ambazo zimemwezesha kuwa kwenye Big five. Na hawa ndo wanyama ambao ni Big five kwa Africa Simba (Lion ), mbogo au nyati (Buffalo ), chui (Leopard ), Faru (Rhino ) na tembo (Elephant )
 
Stori nzuri, japo umesahau kuweka chumvi hizi
1. Kifaru ana upeo mdogo sana wa kuona (impaired eye sight), kwa zaidi anategemea kunusa/upepo
2. Faru hapatani na moto, akiona moto atajitahidi kuuzima kadri awezavyo
3. Ni moja ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka kabisa duniani
4. kawaida faru ni wanyama wapole, lakini wana hasira kali sana wanapokorofishwa, tena huwa hawakubali kushindwa
 
White rhino ndo ambaye kidogo ni mpole lakini kwa upande wa Black huyu ndo ambaye ni aggressive
 
Back
Top Bottom