Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 301
- 1,029
Dunia ina mambo na vijimambo
Katika miaka ya 1880+ pale nchini Afrika-Kusini alikwepo bwana mmoja maarufu kwa jina la "Jumper" akihudumu kwenye kampuni ya Reli akiwa kama "SingnalMan".Bwana huyu aliitwa "Mr. Jumper" kwa uwezo wake mkubwa aliokuwa nao wa kuweza kuruka miruko ya hatari kutoka behewa moja hadi lingine kwa kasi ya ajabu pale ilipobidi kufanya hivyo.
Hata hivyo kwa bahati mbaya ikawa siku moja akaruka vibaya na kujikuta anapata ajali mbaya sana iliyompelekea bwana "Jumper" kupoteza miguu yake yote miwili!!.Majina yake halisi aliitwa James Wide. Mwaka 1881 James Wide "Mr. Jumper" aliamua kumnunua Nyani ili aweze kumsadia kufanya kazi zake kwa kuwa yeye tayari alikuwa na ulemavu wa kudumu!
Naam, Nyani huyo aliyefahamika kwa jina la "Jack" baada ya kufundishwa vyema alimudu kufanya kazi zote za bosi wake kama "SignalMan" kwa malipo ya Bia,treni inapotaka kuwasili tu Nyani anazunguusha mtambo!! kazi inaenda vizuri na baadaye anapomaliza kazi yake malipo yake ni kutengewa chupa za Bia,basi ni kufungua moja baada ya nyingine,kulewa kwa kwenda mbele-mwanzo-mwisho!
Matukio yote haya yalijiri pale Cape Town,Port Elizabeth "South Africa-Railyway Station 🚉 " mwaka 1881.