Meya wa Kinondoni amjibu Rais Magufuli, hakuwa na mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa Polisi

Asalaam aleikum wananchi wa wilaya ya kinondoni na viunga vyake, niendelee kuwaombea ndugu zetu waislamu funga yao iwe na heri na baraka tele ikiwa leo ni chungu cha 19.

Leo tarehe 25 june 2016, nimepigiwa simu nyingi sana na kupokea taarifa kwa njia mbalimbali, nikiulizwa nilipo? kwanini sipo kwenye tukio la Biafra la uzinduzi wa shughuli ya jeshi la polisi? na wengine wakiniuliza neno baada ya kuuliziwa hadharani na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

MHESHIMIWA RAIS John pombe Magufuli; Mstahiki meya manispaa ya kinondoni leo siku ya jumamosi kijana wako na mtumishi wa wananchi wa manipsaa ya kinondoni nilikuwa naunga mkono shughuli za usafi. Nimeshinda na wananchi wa ubungo kisiwani kutwa tukifukua mitaro ya maji machafu kuhakikisha usalama wa afya za ubungo kisiwani zipo salama na zaidi kuweka miundo mbinu yetu sawa.

Nami nilitamani sana kukuona japo kwa karibu sana au kuongea na wewe mambo kadhaa kwa mustakabali wa kinondoni yetu na nchi yetu kwa ujumla, hasa hali ya kisiasa na kiuchumi ili kurahisisha upatikanaji wa Maendeleo.

Mheshimiwa Rais leo nadhani umejionea mahusiano yenye shaka na mabaya niliyokuwa nalalamikia siku zote kwa njia mbalimbali. Viongozi wa wilaya na mkoa hatuna tena ukaribu wakupashana wala kutaarifiana habari yoyote,
iwe nzuri au mbaya.

Mheshimiwa Rais, meza kuu ilipaswa kukwambia ama kukupa jibu kuwa sikuwa na mwaliko leo wa kuhudhuria shughuli hiyo hakuna kiongozi wa polisi yeyote ,awe IGP, RPC, OCD wala OCS aliyenipigia simu au kunitumia unumbe wa aina yeyote kuwa nikaribie tukio lako la leo. Hakuna mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wala wilaya aliye nitumia ujumbe wa aina yeyote au kinipigia simu akinijulisha au kuniomba nikaribie kwenye tukio lako leo.

Mheshimiwa Rais; shughuli za ulinzi na usalama zina taratibu zake, na mimi mstahiki meya wa kinondoni siyo mjumbe wa kamati ya ulinzi, kuanzia mtaa, kata, wilaya mpaka mkoa. Hivyo ni ngumu sana kujua shughuli hizo wala kuhusishwa kama haujapewa taarifa na wahusika walioandaa ujio wako na uzinduzi wa leo.

Mheshimiwa Rais, binafsi nilichukulia kwa uzito kuwa sihitajiki mahala hapo kwakuwa tukio lako la leo nilishatoa ushirikiano kabla ya kuona sina mualiko, kwakuwa greda la kusafisha na kuandaa eneo la tukio lako nili idhinisha mimi na kuhakikisha polisi wanapatiwa kutoka kwa wananchi wa kata ya Goba lilipo kuwepo likikwangua barabara.

Baada ya ombi lao la greda kufanikiwa kusafisha vizuri, Juzi siku ya alhamisi, karani wangu alipokea barua maalum yenye malekezo maalumu yakitaka madiwani watano waje kwemye shughuli hiyo. Barua hiyo maalumu yenye mihuri ya siri niliitekeleza kwa kuteua madiwani watano tena kutoka kwenye kamati ya fedha,nilijua ni taratibu tuh za kiusalama, ambapo leo walihudhuria. Laiti barua hiyo ya polisi ingenitaja tuh au kama ningetumiwa barua yangu binafsi basi ningehudhuria tukio hilo bila shaka.

Mheshimkwa Rais,binafsi nimeshindwa kulielewa jeshi la polisi kama ulivyoshindwa kunielewa mimi, kwakuwa bado ninaamini kuwa pamoja na makandokando ya kisiasa yaliyopo walipaswa kunialika. Si mimi tu, bali pamoja na viongozi wengine wa upinzani kwakuwa zoezi hili lilikua ni lakitaifa.

Mheshimiwa Rais nimalize kwa kusema kuwa laiti ninge pata mualiko ningefika kwa heshima yako kwakuwa naamini bado kinondoni inahitaji mahusiano bora baina ya manispaa ya kinondoni na serikali kuu. Jambo la leo lilitawaliwa na baadhi ya watendaji kusutwa na dhamira zao, kuona ningekaaje meza kuu mimi meya wa upinzani, ndiyo maana sikuwa meza kuu na kiti changu,wala rasimu ya ratiba ainitaji popote wala kunipa walau nafasi ya kusalimia,ukiondoa nia yako njema binafsi ya kunitambua,kwao waliona sistahili na hakuna haja hiyo ya kuapata wasaa au heshima wakati wamejipa kazi kuua demokrasia ambapo mimi ni tunda la siasa za vyama vingi.

Mheshimiwa Rais, binafsi nina historia ngumu sana ya kuonja machungu ya jeshi la polisi kama walivyo wapinzani wote. Ila kwenye maendeleo wakinihitaji wakati wowote,nitatoa ushirikiano wangu kwa nguvu na akili zote, ndiyo maana tumekuwa tukisisitiza *polisi wasitupige mabomu chadema ni serikali ijayo*.

ASANTENI,

IMETOLEWA TAR 25/6/2016
NA MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI: BONIFACE JACOB

Pamoja na ukweli kwamba mimi binafsi siikubali CHADEMA ingekuwa ni mtihani barua hii ningeipa PASS. ningetoa maksi 58/100 ambayo ni B. Ili iweze kupata alama ya A yaani kuanzia maksi 70 na kwenda juu ningeifanyia editing kubwa kwa kushirikikisha wataalamu wa protocol, uhusiano, wasomi na wanasiasa wazuri...
 
Magufuli: Halo kijana habari yako? Unaongea na Rais wako
Mkuu wa wilaya: Sssalama Rais shkamoo
Magufuli: Mbona sikuoni hapa kwenye maadhimisho?
Mkuu wa wilaya: Sssssikuwa na mwaliko mzee. Watendaji wako wa wilaya hawana ushirikiano na mimi.
Magufuli: Kutokufika kwako tumlaumu nani?
Mkuu wa wilaya: Kimya...

Hahahahahaha.. weeee unamchezea Magufuli wewe Tinga tingaaaaaaa... Mi mzee wangu Magufuli nakukubali sana aisee. endelea kuwapeleka puta hivo hivo. Halafu nafurahi unawapeleka kotekote si CCM wala Upinzani. Safi sana mzee wangu unastahili kabisa kutunukiwa Degree ya heshima "HONORIS CAUSA SUMMA CUM LAUDE"
 
Haya mahusiaano mabaya hivi, yaliyojaa vitisho, matusi, ubaguzi na udhalilishaji kwa viongozi na watetezi wa Wananchi, yanaasisiwa katika ngazi gani ya awamu hii ya tano? Ninaona yamerasimishwa kila mahala na sioni anayesimama kitaifa kukemea angalua kwa kutambua kwamba binadamu ni mnyama pia. Hakuna mtu hata uwe na sifa zipi utaishi kwa furaha katikati ya wanyama waliochoka. Niliona mkanda mmoja wa Kenya ambapo kulikuwa na ukame na njaa sana porini, nyani wakaamua kuenda kwenye makao ya binadamu kujipatia riziki. Vita ikawa kati ya nyani wa msituni na watu majumbani.

Ninaomba viogozi wasilewe historia. Unafiki ni kama uvumilivu ambao huwa unamwisho. Unganisheni taifa kwa maslahi mapana y amsutakabali wa nchi. Binadamu ni wanyama.
 
CCM mnakosea sana kwenye mambo ya kitaifa kama haya. Acheni hizi siasa za maji taka. Ujambazi hauchagui chama.

WHY mstahiki Meya asialikwe kwenye tukio muhimu kama hilo? Yaani mnaalika madiwani tu na kumbagua Meya??!!

Lengo lenu ni nini hasa, ili ionekane kuwa Meya kasusia hilo tukio kwa maksudi eeh? Binafsi nakilaani sana kitendo hicho cha kutomualika Meya.

Ndugu zangu watanzania, tukienda hivi hatutafika. Tukiweka siasa kwenye kila jambo tutakwama tu. Ifikie mahala tuwe serious na kuweka siasa pembeni yanapokuja masuala muhimu ya Kitaifa.

Mh Rais kaelewa kuwa Meya kasusia/kadharau tukio hilo. Na wananchi pia wakaelewa hivyo hivyo. Kumbe Meya hakupewa mualiko rasmi ! daaah hili linashangaza sana kwakweli. Bado tuna safari ndefu sana kama Taifa.

Hili Taifa mnaliweka bondi !

-Kaveli-
 
Pamoja na ukweli kwamba mimi binafsi siikubali CHADEMA ingekuwa ni mtihani barua hii ningeipa PASS. ningetoa maksi 58/100 ambayo ni B. Ili iweze kupata alama ya A yaani kuanzia maksi 70 na kwenda juu ningeifanyia editing kubwa kwa kushirikikisha wataalamu wa protocol, uhusiano, wasomi na wanasiasa wazuri...
Chuo gani hicho ambacho 58 ni B na 70 A? Kumbe kuna watu wanasoma kwa raha hivyo.
 
Back
Top Bottom