Meya wa Dar kupitia upya mikataba ya UDA, DART na stand ya Ubungo

huyo meya hajasoma pubic management na wala hajui kwa nini wabunge wanaapa kulindaa siri za bunge wakati huo huo mijadala ya bunge inaonekana live azam tv. hajui ni kwa nini viongozi wote baada tu ya kiapo cha uaminifu wanaapa kutunza siri ... siri gani hizo ? sasa kama mikataba ya kibiashara huwa ni siri na hulindwa kwa maslahi ya pande zote mbili zinazonufaika na hiyo mikataba.kimsingi matatizo ya wana wa dar es salaam sio kujua siri iliyofichwa kwa miaka mingi ... hapana. jukumu la meya ni moja tu kutatua kero sio kutujaza taarifa sisi wapiga kura ili tufurahi au tusikitike ... achukue hatua. matunda na machungu ya hatua alizochukua ndizo tunazotaka kuziishi
Umesomea wapi hio public management
 
Moja wapo ya kero zetu Wana DSM ni pamoja na watu kuimilikisha UDA, UBT, pamoja na DART. Tena waliomiliki wanakabidhiana tu na hatujui tunanufaika nini na vitu hivi.

Meya anapaswa kuweka mazingira mazuri ya ukusanyaji wa pesa kwa ajili ya kutatua kero. Hivi unafikiri atapata wapi pesa za kutatua hizo kero???????

Meya waliopita wote walikuwa wanaficha hiyo siri unayosema wewe kwa manufaa yao binafsi na siyo kwa faida ya wana DSM.

Unataka kifichwe nini ambacho sisi wana DSM hatupaswi kukifahama????

mbona makampuni yenye wana hisa huwa wana utatratibu wa kuweka hadharani mapato na matumizi tena katika vyombo vya habari ili wananchi na wana hisa wote wapate kujua kinachoendelea??

Mbona Uongozi wa Awamu yua tano mara tu baada ya kuapishwa wakaanza ziara ya BOT, TRA yaani sehemu zenye pesa kwani walielewa kuwa ili kuongoza wananchi vizuri lazima uwe na pesa.

Hivyo na meya naye ana jukumu la kufahamu atapata wapi pesa!!!!!
 
kwahiyo hajengi tena madampo kila wilaya? zile 800m za vijana ndio zimekwisha tayari, wiki mbili yuko ofisini kafanya nini cha maana? akiona hiyo mikataba haina dosari kisheria inakuwaje? ukisikia porojo ndio hizi.
 
huyo meya hajasoma pubic management na wala hajui kwa nini wabunge wanaapa kulindaa siri za bunge wakati huo huo mijadala ya bunge inaonekana live azam tv. hajui ni kwa nini viongozi wote baada tu ya kiapo cha uaminifu wanaapa kutunza siri ... siri gani hizo ? sasa kama mikataba ya kibiashara huwa ni siri na hulindwa kwa maslahi ya pande zote mbili zinazonufaika na hiyo mikataba.kimsingi matatizo ya wana wa dar es salaam sio kujua siri iliyofichwa kwa miaka mingi ... hapana. jukumu la meya ni moja tu kutatua kero sio kutujaza taarifa sisi wapiga kura ili tufurahi au tusikitike ... achukue hatua. matunda na machungu ya hatua alizochukua ndizo tunazotaka kuziishi

siri gan boss? ya ujambazi
 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, aliyetokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Charles Mwita, amesema mikataba tata iliyoingiwa na Jiji ukiwamo ule wa mabasi yaendayo kasi (DART) na Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) pamoja na ule wa Kituo cha Mabasi Ubungo, itapitiwa upya na wanasheria kisha taarifa zake kuwekwa wazi kwa umma.

Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum mwishoni mwa wiki, Meya Mwita alisema: “Tutaita wanasheria na tutaipitia hadharani na tutawaeleza wananchi. Nina siku tatu ofisini, nipeni muda zaidi nitaeleza tuliyobaini kwenye mikataba husika.”

Meya huyo ambaye alichaguliwa na madiwani wa CHADEMA na wa CUF, alisema hakutakuwa na ubabaishaji katika mikataba hiyo kwani ndiko mapato mengi yanakopotea na kusababisha miradi ya maendeleo inayohudumia wananchi wengi kukwama ama kutotelekezwa.

“Ninachotaka bora mimi nife, lakini wananchi mpate haki, mmekuwa maskini kwa muda mrefu sana, mmedharauliwa vya kutosha, haiwezekani nchi ni yetu sote, siyo ‘majitu’ fulani yanakuja hapa yanatengeneza genge la wizi na kutajirika, wakati raslimali zipo na fedha za kutekeleza miradi ipo, kinachotakiwa ni usimamiaji na ufuatiliaji kuhakikisha hakuna shilingi inapotea,” alisisitiza na kuongeza.

“Tutaheshimiana hapa mjini Mungu ndiye ametupa Dar es Salaam, tutawatumikia sana kwa nguvu zote,” alisema Mwita ambaye ni diwani wa kata ya Vijibweni.

Meya huyo alianza na mradi wa Uda kuwa atahitaji ripoti kutoka kwa waliokuwepo na kusoma kwa undani ndipo atakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia.

"Kituo cha Ubungo,mwaka jana kulikuwa na mpango wa kukihamisha kwenda Mbezi, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika, ninachosubiri ni ripoti ya kwanini waliamua kubomoa kabla hawajamaliza kujenga kituo mbadala," alisema na kuongeza.

“Tutaamua kwa pamoja katika kikao chetu cha Jiji kwamba tutaendelea na kituo kilichopo au Mbezi. Nina jambo la dharura nitakwenda kulifanya juu ya kituo hiki ambacho kinatoza fedha kwa watumiaji, lakini hakuna huduma za choo, kujikinga na jua na mpangilio kwa ujumla,” alisema.

BODABODA
Meya huyo alisema hatakubaliana na kamatakamata ya waendesha pikipiki inayofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji kwa kuwa vijana wanajitafutia riziki ya kuendesha familia zao.

“Hawa ni Watanzania wenzetu ambao serikali iliwanyima elimu, mtu akijiajiri tumuonee huruma, tumsaidie na siyo kumfanya awe maskini zaidi,” alisema.
Meya Mwita alisema suala la pikipiki kuingia katikati ya Jiji litajadiliwa kwenye vikao na kusikiliza walioamua kuwazua kwanini walifanya hivyo na kama inawezekana kuweka utaratibu wa muda wa kuingia na kutoka.

Alisema wengi wanakamatwa kwa makosa ya leseni, lakini kinachoonekana ni kukosekana kwa elimu, hivyo Polisi na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuwaelimisha umuhimu wa kuwa na leseni na bima za vyombo vyao.

“Nitaendelea kutoa elimu kwenye vyombo vya habari, nitawakusanya waendesha bodaboda wote nitaongea nao, pia madiwani wa vyama vyote tujadili kwa kina na kuwa na utaratibu maalum kwa ajili yao nao watoe elimu ya uraia kwenye kata zao,” alisema.

Chanzo: Nipashe
 
Exactly.. But ajilinde..asijiachie aji huko kuna maslahi ya watu wakubwa sana ...#
na hao wakubwa ndio inasemekana walifungua kesi mahakamani kuzuia uchaguzi wa Meya kwa lengo la kuficha uchafu wao , ukishawaanika hadharani wahusika wote hiyo ni kinga kubwa zaidi .
 
Nchi hii ni kituko, baada ya kuona majiji makubwa mengi yameshikwa na upinzani nasikia Serikali imeanza kubadirisha baadhi ya Sheria/Taratibu za makusanyo ya Property Tax, kwasasa makusanyo haya yatakua chini ya TRA badala ya Halmashauri ili upinzani usije ukiwafunika katika makusanyo katika Halmashauri, Sitaki kuamini kwamba hata Magu ameishaingia kwenye huu mtego wa uchama chama
Story hizo
 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Charles Mwita, amesema mikataba tata iliyoingiwa na Jiji ukiwamo ule wa mabasi yaendayo kasi (Dart) na Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) pamoja na ule wa Kituo cha Mabasi Ubungo, itapitiwa upya na wanasheria kisha taarifa zake kuwekwa wazi kwa umma.

Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum mwishoni mwa wiki, Meya Mwita alisema: “Tutaita wanasheria na tutaipitia hadharani na tutawaeleza wananchi. Nina siku tatu ofisini, nipeni muda zaidi nitaeleza tuliyobaini kwenye mikataba husika.”

Meya huyo ambaye alichaguliwa na madiwani wa Chadema na wa CUF, alisema hakutakuwa na ubabaishaji katika mikataba hiyo kwani ndiko mapato mengi yanakopotea na kusababisha miradi ya maendeleo inayohudumia wananchi wengi kukwama ama kutotelekezwa.

“Ninachotaka bora mimi nife, lakini wananchi mpate haki, mmekuwa maskini kwa muda mrefu sana, mmedharauliwa vya kutosha, haiwezekani nchi ni yetu sote, siyo ‘majitu’ fulani yanakuja hapa yanatengeneza genge la wizi na kutajirika, wakati raslimali zipo na fedha za kutekeleza miradi ipo, kinachotakiwa ni usimamiaji na ufuatiliaji kuhakikisha hakuna shilingi inapotea,” alisisitiza na kuongeza.

“Tutaheshimiana hapa mjini, Mungu ndiye ametupa Dar es Salaam, tutawatumikia sana kwa nguvu zote,” alisema Mwita ambaye ni diwani wa kata ya Vijibweni.

Meya huyo alianza na mradi wa Uda kuwa atahitaji ripoti kutoka kwa waliokuwepo na kusoma kwa undani ndipo atakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia.

"Kituo cha Ubungo, mwaka jana kulikuwa na mpango wa kukihamisha kwenda Mbezi, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika, ninachosubiri ni ripoti ya kwanini waliamua kubomoa kabla hawajamaliza kujenga kituo mbadala," alisema na kuongeza.

“Tutaamua kwa pamoja katika kikao chetu cha Jiji kwamba tutaendelea na kituo kilichopo au Mbezi. Nina jambo la dharura nitakwenda kulifanya juu ya kituo hiki ambacho kinatoza fedha kwa watumiaji, lakini hakuna huduma za choo, kujikinga na jua na mpangiliop kwa ujumla,” alisema.

BODABODA
Meya huyo alisema hatakubaliana na kamatakamata ya waendesha pikipiki inayofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji kwa kuwa vijana wanajitafutia riziki ya kuendesha familia zao.

“Hawa ni Watanzania wenzetu ambao serikali iliwanyima elimu, mtu akijiajiri tumuonee huruma, tumsaidie na siyo kumfanya awe maskini zaidi,” alisema.

Meya Mwita alisema suala la pikipiki kuingia katikati ya Jiji litajadiliwa kwenye vikao na kusikiliza walioamua kuwazua kwanini walifanya hivyo na kama inawezekana kuweka utaratibu wa muda wa kuingia na kutoka.

Alisema wengi wanakamatwa kwa makosa ya leseni, lakini kinachoonekana ni kukosekana kwa elimu, hivyo Polisi na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuwaelimisha umuhimu wa kuwa na leseni na bima za vyombo vyao.

“Nitaendelea kutoa elimu kwenye vyombo vya habari, nitawakusanya waendesha bodaboda wote nitaongea nao, pia madiwani wa vyama vyote tujadili kwa kina na kuwa na utaratibu maalum kwa ajili yao nao watoe elimu ya uraia kwenye kata zao,” alisema.

Chanzo: Nipashe
Hii ya Boda boda wajenge njia za kupita boda boda na sio kuchanganyika na magari makubwa, kama wanayo nia ya kuwasaidia kweli. La sivyo utaratibu wa sasa sio condusive kwa waendesha boda boda, Tuache siasa na kutafuta popularity bila kutumia akili
 
Nchi hii ni kituko, baada ya kuona majiji makubwa mengi yameshikwa na upinzani nasikia Serikali imeanza kubadirisha baadhi ya Sheria/Taratibu za makusanyo ya Property Tax, kwasasa makusanyo haya yatakua chini ya TRA badala ya Halmashauri ili upinzani usije ukiwafunika katika makusanyo katika Halmashauri, Sitaki kuamini kwamba hata Magu ameishaingia kwenye huu mtego wa uchama chama

Zamani TRA walikuwa wanakusanya kodi za majengo kwa niaba ya Halmashauri, walichokipata sitaki kuamini kama itakuwa busara kurudisha uwakala TRA.
 
Back
Top Bottom