SoC02 Meno kuoza: Madhara na kujikinga

Stories of Change - 2022 Competition

Angina

Senior Member
May 13, 2018
142
137
Kuoza kwa meno ni moja kati ya magonjwa yasio ya kuambukiza Kama kisukuri na shinikizo la damu . Tofauti na magonjwa mengine yasio ya kuambukizwa kuoza kwa meno ni moja ya shida kubwa Sana inayo athiri mtu yoyote yule mwenye meno.

Watoto wadogo,vijana ,wazee na wanawake wote wanaweza patwa na hii shida.Nchi nyingi duniani Tanzania miongoni hazitoi kipao mbele katika huu ugonjwa japo kuwa umekua chanzo kikubwa cha maumivu ,kupoteza meno na wakati mwngne hupelekea kifo sababu katika hatua za mbele Zaidi husababisha usaha ambao unaweza fika adi kwenye mapafu na kusababisha shida katika upumuaji.

SABABU YA MENO KUOZA

1. Bakteria : ndani ya kinywa cha mwanadamu Kuna kiasi kikubwa Cha bakteria ambao kwa mazingira ya kawaida hawasababishi shida,lakini endapo Kuna mabadiliko yoyote mfano kutokuwa na kinywa kisafi .Bakteria hao huvunja mabaki ya chakula bila uwepo wa hewa ya oksijen na kutengeneza laktik asidi ambayo ndo huozesha meno kwa huvunja na kuondoa madini kutoka kwenye jino hivyo jino lnakuwa dhaifu na baadae kupelekea kutoboka.

2. Vyakula venye sukari:Asilimia kubwa ya watu hasa watoto hupendelea Sana kula vyakula vyenye sukari sababu kubwa ni vitamu.Vyakula hivyi ndivyo bakteria huvunja mabaki yake na kuzalisha asidi .Mfano wa hivyo vyakula ni Kama mkate ,biskuiti ,soda na maziwa hasa kwa watoto wadogo wanao nyonya.

3. Jino : Mara nyingi meno ya nyuma (magego ) ndo uoza hii ni kutokana na mwonekano wake hasa sehemu ya kutafunia ambayo ni chanzo cha utunzaji wa mabaki ya chakula hivyo ni rahisi kwa bakteria kuvamia na kuozesha hayo meno.

NANI YUPO KATIKA HATARI YA KUOZA MENO

1. Wenye mpangilia mbaya wa meno:Mpangilio mbaya wa meno husababisha mtu kushindwa kusafisha meno vizuri hivyo mabaki ya chakula hubaki kwenye meno na bakteria huvunja hicho chakula na kutengeneza asidi ambayo husababisha matundu na kuoza kwa meno.

2. Waliofanya matibabu ya kufunga nyaya kwenye meno na kuziba jino: nyaya na dawa zinazotumika kuziba meno zinauwezo mkubwa kwa kutunza mabaki ya chakula ikiwa mtu uyo hawez safisha kinywa vizur.Hivyo bakteria ushambulia ayo mabaki na kusababisha kuoza kwa meno

3. Kutosafisha kinywa walau mara moja kwa sku: kwa kawaida unashauriwa kupga mswaki mara mbili kwa sku kabla ya kulala na baada ya kunywa chai .Lengo kubwa likiwa ni kuondoa mabaki ya chakula ambayo bakteria uyatumia kutengeneza asidi ambayo inaozesha meno.

4. Wasiotumia dawa ya mswaki yenye madini ya floride: Madini ya flouride husaidia kuriimarisha jino na kulifanya lisitoboke au kuharibika kwa haraka.
Watu wanaishi kaskazini mwa tanzania ,shinyanga na singinda meno yao ni ya brown sababu kubwa maji watumiayo yana kiwango kikubwa Cha fluride ndo maana watu hao meno yao hayaozi kwa haraka ukilinganisha na watu wengne.

5. Umri : watoto wadogo hasa wale walio katika umri wa kunyonya huathiriwa Sana na meno kuoza hii ni kutokana na sababu Kama vile watoto kulala na chuchu mdomoni hasa wakati wa usku , mtoto kunyonyeshwa Kila wakati pia Kuna baadhi ya maeneo mtoto anapewa uji wenye sukari nyingi kabla ya umri wa kuanza kunywa uo uji.

Unashauriwa kwa kipindi Cha miezi sita baada ya mtoto kuzaliwa chakula chake yawe maziwa ya mama tu. Kwa maana katika iyo miezi sita mfumo wa chakula bado hujakaa vizuri na vtu laini Kama maziwa ya mama ndo vinaweza mengenywa.

Je mtoto wako alianza kula vyakula vingine tofauti na maziwa ya mama akiwa na miezi mingapi ?

Kuna baadhi ya kina mama na mabibi hasa vijijini hupenda kutafuna chakula Kisha kukitemea mdomoni kwa watoto wadogo ambao bado hawana uwezo wa kutafuna vyakula vigumu.Hii nayo ni sababu kubwa ya kuoza kwa meno hasa kwa watoto wadogo.Kwa maana bakteria huamishwa kutoka kwa mama/Bibi kwenda kwa mtoto.

6. Midomo mikavu: hii huwatokea watu hasa waliofanya mionzi ya matibabu maeneo ya kichwani ,matumizi ya baadhi ya madawa.

Ndani ya mate Kuna madini kama carbonate ambayo Kazi yake kubwa ni kushusha kiwango cha asidi ndani ya mdomo baada ya bakteria kuvunja mabaki ya chakula.

MADHARA GANI HUTOKEA BAADA YA MENO KUOZA.

1. Maumivu ya meno: Hii hutokea ni baada ya bakteria wanaoozesha meno kufika katika mishipa ya fahamu ya jino.

Pia maumivu hayo yanakuwa makali akinywa vitu vya baridi au Moto ,pia wengne hata upepo ukipiga kwenye meno hulalamika maumivu.

2. Uvimbe kwenye fizi unaoambatana na usaha:

Ilo jino lisipotelewa kwa mda usaha hua unasambaa adi kufika kwenye shingo na wakati mwingine usaha unaweza fika adi kwenye mapafu na kumfanya mtu asiweze pumua vzur na kupelekea kifo.

3.Kushindwa kutafuna hasa upande wenye maumivu.Hivyo mtu hushindwa kula ambayo hupelekea mtu kupoteza uzito.

4. Jino kutoboka ,kulegea na kuanza kumeguka vipande mwisho wa sku jino lnabaki mzizi tu.

Kuoza kwa meno ndo chanzo kikubwa Cha mtu kuwa kibogoyo.

JINSI YA KUPAMBANA NA KUZUIA HALI YA UOZAJI WA MENO

1. Safisha meno walau mara mbili kwa siku: kabla ya kulala na baada ya kunywa chai asubuhi kwa kutumia dawa ya mswaki yenye madini ya flouride hii husaidia kuongeza ugumu kwenye meno hivyo huzuia meno kuoza.

Ili kutimiza ilo inabd uwe na mswaki imara na kwa kawaida inabidi mswaki ubadilishwe Kila baada ya miezi mitatu.Je wako unabadili baada ya mda gani ?

Kwa watoto wadogo kuanzia miaka 0-6 wazazi na walezi ndo wenye jukumu la kuwasifisha hao watoto ili uweze kufikia kiwango Safi cha kinywa na meno mzazi au mlezi ndo mtu sahihi kulitimiza hilo.

Kwa watoto wa miaka 6-9 wanaweza kujisafisha wao wenyewe lkn chini ya uangalizi wa mzazi au mlezi.

Mtoto inatakiwa aanze kujisafisha meno yake bila usimamizi akifikisha miaka tisa yaani Darasa la tatu,vp mtoto wako alianza kujisafisha mwenyewe meno akiwa na miaka mingapi ?

2. Hudhuria kwa daktari wa meno walau mara mbili kwa mwaka : Hatua zote adi jino lioze ni miezi 18 kwa iyo unapohudhuria kwa daktari wa meno na kufanya chekapu inasaidia sababu meno yenye shida yote hutambuliwa na kutibiwa mapema kabla hayajaleta shida zaidi.

3. Punguza ulaji wa vyakula vyenye sukari: hii itasaidia maana bakteria watakosa sehemu ya kushambulia.

Wazazi wenye watoto wanaonyonya wanapaswa kuzuia kuwalaza watoto wao na chuchu zikiwa mdomoni hasa wakati wa usiku. Wakati wa usku mtoto akiitaji kunyonya amka kaa kitandani mnyonyeshe mwanao ili kumpunguzia hatari ya kuoza meno.
 
yote hayo mnajisumbua nenda duka la dawa mwambie akupe vitamin c ni vidonge vya kumumunya tumia kama sehemu ya kinga mlo hutakaa kusikia meno kuuma kufa ganzi kutoboka kwakua vitamin c inasaidia sana kujenga uimara wa meno ila ukitegemea kuipata kwenye machungwa na mboga mboga lazma utoboke meno kwakua mule inapatikana kwa asilimia ndogo sana
 
yote hayo mnajisumbua nenda duka la dawa mwambie akupe vitamin c ni vidonge vya kumumunya tumia kama sehemu ya kinga mlo hutakaa kusikia meno kuuma kufa ganzi kutoboka kwakua vitamin c inasaidia sana kujenga uimara wa meno ila ukitegemea kuipata kwenye machungwa na mboga mboga lazma utoboke meno kwakua mule inapatikana kwa asilimia ndogo sana
Hapo unazungumzia vitamin D na sio vitamin C maana kubwa ya vitamin D ndo kuimarisha mifupa na meno ,lkn uimarishaji uo wa meno ni wakati ukiwa mdogo meno yakiwa yanaota na mengine yakiwa bado hayajaota.

Kazi kubwa ya vitamin C ni kulinda fizi zako na mara nyingi mtu mwenye upungufu wa Vitamin C hua anatoka damu kwenye fizi hasa anapokua anapiga mswaki au anapokula vitu vigumu Kama embe bichi.
 
Hapo unazungumzia vitamin D na sio vitamin C maana kubwa ya vitamin D ndo kuimarisha mifupa na meno ,lkn uimarishaji uo wa meno ni wakati ukiwa mdogo meno yakiwa yanaota na mengine yakiwa bado hayajaota.

Kazi kubwa ya vitamin C ni kulinda fizi zako na mara nyingi mtu mwenye upungufu wa Vitamin C hua anatoka damu kwenye fizi hasa anapokua anapiga mswaki au anapokula vitu vigumu Kama embe bichi.
Karbuni sana ujipatie elimu ya bure kuhusu kuoza kwa meno na namna ya kujikinga pia usiache kupigia kura andiko hili
 
Back
Top Bottom