Mengi na Kusaga kukumbatiana ni kombora kubwa kwa Serikali ya Magufuli

Kitendo cha MENGI Na KUSAGA kukumbatiana ni ishara ya kudondoka kwa serekali ya JPM.

Nakumbuka kwa muda mrefu Makonda amekuwa akihakikisha IPP na Clouds media hawawi kitu kimoja.Hata kwenye ziara zake alikuwa akiwasifu clouds na kuwanyamazia ITV kama vile hawapo.

Pia kumbuka leo hii EFM wamekumbatiana na Clouds FM hii yote ni baada ya Rais kumkingia kifua mwalifu.

Kwa mtu mwenye jicho la tatu.Hali hii itaidhoofisha sana serekali.Maana kwa sasa hata JPM afanye kitu gani kitapewa muda kidogo sana.Na bila. Vyombo imara vya habari huwezi kuwa na serekali imara kamwe.

Kumbuka pia kitendo cha bashite kubwebwa.

Nipashe,Mwananchi,Mtanzania,Tanzania Daima,Jamhuri,Mawio na Mwanahalisi nayo yameungana kuwa kitu kimoja.

Hivi,JPM atatokea wapi?Hayo ni maumivu makubwa kwa serekali.Lakini Magufuli kakubali serekali yake ipate maumivu kisa ni mtu mmoja tu.BA-SHI-TE.

Kweli nimeamini pombe sio chai!
Mawazo pumba kabisa, by the way who is Mengi in this country, who is Kusaga ? wewe lazima utakuwa Chadema
 
Heshima itarudi je.Nani anatizama TBC karne hii.Yani ndio itapotea kabisa.Maana itaanzishwa kampe Namba 2 ya kuisusia kabisa.
Umenena Mkuu Kibo10. Hata mkulu mwenyewe anaangalia Clouds 360, achilia mbali Sh...wadu! Jana tu ITV wamepotezea tambo za mkuu akimfagilia bwa mdogo pale ubungo.

Hao TBC shiida tupu, wanaingizwa mkenge kilahiisi, (refer issue ya mkuu kusifiwa na Trump). Nani wa kuwa view huo mchannel wao! Kitaeleweka tu!
 
hawajaungana hao,ila wameguswa na tukio na kuliripoti kwa pamoja,na kupeana pole.ni sawa na lowasa na magufuli kukutana katika kifo cha kigogo wa nchi,baada ya kilichowakutanisha kila mtu ataendelea na sera zake
Lakini hilo tukio na maneo ya mkulu ya piga kazi tu yame waweka/tuweka pamoja sana
 
Hata kama wakiungana wote, serikali ina makombora mengi tu ambayo ukirushiwa unabaki kuhangaika nalo:

1.TCRA

2.TRA

3.WIZARA YA HABARI

Bonus:

1.MATANGAZO

2.NSSF/LAPF/PPF na MIKATABA YA AJIRA

3.OSHA

4.NEMC
 
Arudi TBC kwa Gabriel zacharia,ameacha redio/Tv ya taifa mitambo inaliwa na mende,watangazaji waandamizi wanaishi maisha ya hovyo bila kuwa na vitendea kazi vya kisasa hata vya kugundua fake news

Cha kuazima hakisitiri masaburi,hao akina mengi na kusaga wametoa hela zao mfukoni na matunda yanaonekana,pamoja na kodi serikali imeshindwa kuijali TBC.

Tunashukuru Clouds kwa kuwafukuza Bashite na Sizonje
 
Huyu daudi albert bashitee ama paul christian malanja ama paul chrstian makonda (in gwajima's voice).
 
Hivi ikatokea makonda ameondolewa huko uliko utafaidika na kitu gani? Maana kuna watu wanashadadia mambo kumbe hawajui wanasiasa na mibepari michache imebanwa wanatafuta pakutokea
 
Najiuliza tu Siku Bashite Akivamia Jamiiforums wale Askari wake kuchukua Data base ile alokataa Maxmelo kuitoa tutapona kweli?
 
Muda muafaka wa kurudi heshima ya TBC, maana hivyo vyombo ndio vilifanya TBC inaonekane takataka tu humu nchini.
TBC ipi yakushinda Vyombo vipi??? Hata ikitumiwa na jpm na bashite tulio wengi hatuhitaji hata kusikia sauti zao...
 
Kitendo cha MENGI Na KUSAGA kukumbatiana ni ishara ya kudondoka kwa serekali ya JPM.

Nakumbuka kwa muda mrefu Makonda amekuwa akihakikisha IPP na Clouds media hawawi kitu kimoja.Hata kwenye ziara zake alikuwa akiwasifu clouds na kuwanyamazia ITV kama vile hawapo.

Pia kumbuka leo hii EFM wamekumbatiana na Clouds FM hii yote ni baada ya Rais kumkingia kifua mwalifu.

Kwa mtu mwenye jicho la tatu.Hali hii itaidhoofisha sana serekali.Maana kwa sasa hata JPM afanye kitu gani kitapewa muda kidogo sana.Na bila. Vyombo imara vya habari huwezi kuwa na serekali imara kamwe.

Kumbuka pia kitendo cha bashite kubwebwa.

Nipashe,Mwananchi,Mtanzania,Tanzania Daima,Jamhuri,Mawio na Mwanahalisi nayo yameungana kuwa kitu kimoja.

Hivi,JPM atatokea wapi?Hayo ni maumivu makubwa kwa serekali.Lakini Magufuli kakubali serekali yake ipate maumivu kisa ni mtu mmoja tu.BA-SHI-TE.

Kweli nimeamini pombe sio chai!
Kumbe bwana yule ni dikteta aisee
 
Back
Top Bottom