Membe ananikumbusha Kolimba

Membe katoa maoni yake kama raia wengine humu na huko mtaani. Acheni kucomplicate mambo, sijui TISS, Kolimba etc
 
Wale ambao hawakuwepo zamani na hawajui kilichotokea kipindi hiko
basi ni vizuri tukawasimulia kidogo
Kuelekea uchaguzi wa mwaka 1995 CCM walikuwa na kambi mbili kubwa
ya kwanza ilikuwa ya John Malecela Waziri mkuu na ya pili ilikuwa
ya Horace Kolimba alikuwa katibu mkuu wa chama...

Upinzani ulikuwa mkali sana hadi Mwl. Nyerere alipoingilia kati na
kutunga kitabu akiwaponda wote wawili akiwataka wajiuzulu
waliposhindwa zuia hoja za serikali ya Tanganyika ,Baada ya Mkapa kuapishwa na
kuanza kuongoza....Kolimba akajitokeza hadharani kuikosoa na kuiponda serikali ya Mkapa
maneno yake maarufu yalikuwa 'serikali haina dira wa muelekeo'..

Alipoongea maneno hayo CCM wakamuita kumhoji Dodoma...
akiwa katikati ya kuhojiwa..akafariki....ndio chanzo cha maneno maarrufu
'watakukolimba' maneno haya hasa yalianzishwa na Mchungaji Mtikila
ambae alisisitiza Kolimba 'alichezewa' faulo....

Baada ya leo Membe kumkosoa hadharani Magufuli kwa jinsi anavyoendesha serikali yake
na baada ya leo kumuona Magufuli akiwa ndani ya uniform za JWTZ..
nimejikuta najiuliza......'Membe anamkumbuka Kolimba'?

CCM wote akiwemo Membe walisisitiza Magufuli ni chaguo sahihi
ni mtu wa kufanya utumishi wa kutukuka na atakuwa Rais bora kabisa
sasa mbona wanaanza kumkosoa hata miezi minne bado?
Si wamuache 'Rais wetu mpendwa apige kazi'? wanahofia nini?
wameona dalili zipi? lakini je wanamkumbuka Kolimba?
Ukisikia Mayowe kutoka upande huo Ujue ameshatumbuliwa.....kwahiyo Mkuu usipoteze muda wako....
 
Hivi si wizara yake ilitapanya karibu billioni 174 na ushee kwa safari za nje ?? Anataka kutuaminisha nini Membe ??
Huyu jamaa nadhani bado kwenye akili yake Kikwete anatawala ,kumshauri tu he should choose his battles wisely ,Kikwete is no longer his backborne
 
Lakini huyu aliwahi kunukuliwa kuwa '' Mawaziri wa JK walikuwa wanapishana angani kana kwamba kuna moto ardhini''
Kabadilika ? Au labda pengine hata yeye safari zake za nje alizotegemea zitalipiwa na serikali ya JPM zinapigwa stop..
Huwa unawaamini wana siasa?
 
Kwa wanaojua historia ya ccm watajua anayeongea sio Membe ni kundi la watu wakubwa ndani ya ccm kama yeye alivyo mkubwa hawezi tumwa na wadogo. Anayoyajua membe magufuli hayajui yako mengi nyuma ya pazia sasa kama yako mengi nyuma ya pasia ayajuayo membe bila magufuli kujua nini maana yake? hapo ndo tuna conclude uasi mkubwa umepangwa na wana ccm kwa serikali ya magufuli. Shame on you ccm. CCM ni chama kisichopenda kabisa maendeleo ya Tanzania yaani wanatamani wananchi wote wangekuwa mazezeta ili wawaongoze bila kupata criticism. Sasa bahati tumepata Magufuli angalau kidogo yuko tofauti tayari washaanza kumfanyia hujuma hata miezi 4 haijafika
 
Hapana mkuu respect wa boda, aliyekufa hivyo ni mzee Kombe na si Kolimba. Kolimba alifia Dom na Kombe alifia karibu na nyumbani kwake kwa kupigwa risasi ili mambo flani yasitirike.
Hapana mkuu respect wa boda, aliyekufa hivyo ni mzee Kombe na si Kolimba. Kolimba alifia Dom na Kombe alifia karibu na nyumbani kwake kwa kupigwa risasi ili mambo flani yasitirike.

Tuko pamoja mkuu,

Unajua ukiwa unatype huku unadaiwa kodi, watoto wanasumbua ada na wenyekibanda wanataka kodi zao haya ndo matokeo yake..!!!

Thanks mkuu Frediluu na wengine wote hapo juu

BACK TANGANYIKA
 
Membe Ana uhuru na haki ya kushauri kile ambacho anakiona ni sahihi kwake na kwa serikali.. Tutambue na kujua kuwa Membe sio mtu mdogo katika nchi hii na hata kule kwenye Idara alikuwa ni jasusi ambaye alitegemewa hasa kwa ujuzi wake. Kwahiyo kama unachoongea ni mpango mkakati basi wajipange
 
Hizo ni hofu za mfa maji.mm najiuliza je, kama membe angeweza kuwa mgombea kiti hicho urais na akapata angeongea hivo?!shida ni kwamba wana ccm wengi walijua ccm ni ileile iliyokuwa imejaa uchafu na kunuka ufisadi na rushwa kutawala.lazima sasa watanzania wajue hii ni serikali ya ccm.na anayeiongoza hii serikali sasa ni mtu tofauti na huyo walokuwa wamemzoea.mambo yamebadilika nchi hii sasa inaendeshwa ki sheria na taratibu.aache kuchonga wa kukosa ni wa kukosa tuu,atunze heshima yke.
 
Kama una pay attention Magufuli ana 'watu wake' ndani ya systeam
ambao ndo haswaa wanam advice
na kama hao watu Membe angekuwa na influence nao
asingehitaji kuongea kwa magazeti
angemfuata moja kwa moja
kama anaongea na Magufuli thru media my guess ni kuwa hata huko TISS Membe sio favorite person..

na hapo ndo swali linakuja....anamkumbuka Kolimba?
usisahau Amrani Kombe alikuwa mkuu wa TISS but alipoingia tu Mkapa unajua ilikuwaje...

Nahisi kuna a lot of struggle behind the scene....mara Maswi kapelekwa TRA mara kaondolewa
*Imran
 
ni aibu kubwa na kumtukana horace kolimba kumfananisha na membe. ni aibu kwa sisi tunaoijua siasa. membe si wa kumfananisha na kolimba. membe ni wa kumfananisha na akina nape, kibajaji n.k kolimba alikuwa ni mtu mwenye akili na uwezo wa kjenga hoja. sitak kumzungumzia membe. namzungumzia kolimba kidogo tu. huyu alikuwa na mwono, alikuwa na uongozi ndani yake. huwez mlinganisha na membe hata kidogo. umenitia kichefuchefu sana kwa kumlinganisha membe na kolimba huu ni ukosefu wa heshima kwa mzee wetu na mtu aliyekuwa makini kumlinganisha na watu wa hovyo hovyo.
 
Kila siku thread kuhusu magufuli.magufuli mwenyewe haijui jf
 
Kama una pay attention Magufuli ana 'watu wake' ndani ya systeam
ambao ndo haswaa wanam advice
na kama hao watu Membe angekuwa na influence nao
asingehitaji kuongea kwa magazeti
angemfuata moja kwa moja
kama anaongea na Magufuli thru media my guess ni kuwa hata huko TISS Membe sio favorite person..

na hapo ndo swali linakuja....anamkumbuka Kolimba?
usisahau Amrani Kombe alikuwa mkuu wa TISS but alipoingia tu Mkapa unajua ilikuwaje...

Nahisi kuna a lot of struggle behind the scene....mara Maswi kapelekwa TRA mara kaondolewa

Hivi imekuwaje nguri wa diplomasia anazungumza na media badala ya kumfuata mwenzake ofisini na kumpa ushauri in camera!

Kinacho shangaza Mh.Membe na Dk.Magufuli wote waliwahi kuwa Mapandri watarajiwa miaka ya nyuma, sina shaka walijifunza ethics fulani ambazo wanapaswa kuwa nazo mpaka mwisho wa maisha yao - moja wapo ya ethics hizo ni jinsi ya kumshauri mwenzako kwa upendo mkiwa wawili bila ya ku-involve mtu wa tatu, unapo fikia hatua ya kuvishirikisha vyombo vya habari hapo sasa itadhirisha kuna kitu cha ziada si bure.

Watanzani wote wenye akili timamu bila kujali itikadi za vyama vyao, wanajua wazi wazi kwamba Mzalendo Magufuli ndiye alikuwa chaguo la Mungu kuongoza Taifa letu, sitanii - kumbuka alivyo ruka vihunzi vya chama chake kimihujiza hujiza ya Mungu,aliwekewa spana kila sehemu lakini wapi bwana kahibuka kidedea na kuwashangaza wengi,lilipo kuja suala la kura za Urais that too ilikuwa plain sailing!

Nataka nawakumbushe wana CCM kwamba uchaguzi umekwisha pita, wote tunawajibika kumu-support Dk.Magufuli sio vizuri kujaribu kumpiga vita vya kichini chini - inaonekana vikundi remnant ndani ya CHAMA viko well and kicking i.e havijafa, wasipo vivunja vitasababisha CHAMA kugawanyika vipande vipande.
 
Mimi sijawahi kukuona siwezi kukupiga mikwara, nakukumbusha tu hali halisi ya sasa. Watanzania tunabakia kuamini sababu za ziada za vifo, hata siku moja mtanzania hafi kifo cha kawaida lazima kuna hadithi ndefu nyuma ya kifo chake. Huu unaitwa umasikini wa mawazo.
Unataka kutuaminisha kwamba unajua kila mtanzania anayekufa amekufaje? Are every where that you know for sure causes of the dearth? Ukiona watu wanachangia humu elewa kwamba some have facts so usibishe bishe tuu na kusema watu ni masikini wa mawazo.
 
Back
Top Bottom