Membe amkosoa Magufuli

Unaweza kuwa na Bifu na RAIS wa nchi? Tena nchi unayoishi. Tuwe makini msijisahau kwamba huyo jamaa huwa hajiulizi mara mbili. Membe angetulia tu huko alipo kwa sasa. Sidhani Kama ametumia busara kutoa hayo maneno dhidi ya RAIS.
 
Haka kajamaa hakajitambui, ni fisadi Jnr. Yeye atasema chochote atakacho ili tu kumyumbisha Magufuli asitumbue majipu ya JK na mawaziri wake majambazi. Naona ni wivu tu ndiyo unaomsumbua Membe kwani alitaka sana kuwa rais ili aendelee kuiba na kutetea maslahi ya JK. Rais Magufuli inabidi atumbue majipu ya Membe haraka sana.
Majipu unayajua wewe au unayaskia...Membe ana point hapo afu jamaa ni genius sana anajua anachokisimamia anaona jamaa anaenda mrama lazima aseme.Ni heri huyu bwana angekua rais kuliko huyu tulie nae sasa.
 
Majipu unayajua wewe au unayaskia...Membe ana point hapo afu jamaa ni genius sana anajua anachokisimamia anaona jamaa anaenda mrama lazima aseme.Ni heri huyu bwana angekua rais kuliko huyu tulie nae sasa.
Pole shemeji. Mwaka 2020 sio mbali.
 
Membe hajakurupuka kuna uasi ndani ya ccm, kuna kundi tayari linajuana wana itikadi kinyume na magufuli, huyo katumwa na hiyo ni ka strategy ya kumuharibu magufuli psychologically ili aanze kuwa na mawazo mengi kinzani kwani kasi yake ishaanza kuwagusa wengi waliotoka mle sebuleni wengi mmesikia ya mkulu ikihusishwa na UDA hivi karibuni,
 
Bulembo na Ole Sendeka wasiishie kumjibu Makongoro wamjibu na huyu
Bulembo domo kaya utamsikia tu na elimu yake ndogo lazima ajitokeze Sababu huwa hakosi neno la kusema ili mradi wajue nae yupo ndani ya chama, meneja kampeni wahafidhina wanamsubiri kwenye uchaguzi wa ile jumuiya yake.
 
Sasa cha ajabu ni nini? Kwa maoni yake Membe anaona baraza halijapungua na kuhusu kwenda nje JPM atakwenda muda ukifika na akihitaji. Msipende kutumia vichwa vya habari kujaji alichosema mtu someni habari kamili.
 
Watu wengi tunatoa povu kwa vichwa vya habari kabla ya kusoma stori ndani. Isije ikawa uchonganishi tu.
 
CCM ni mabingwa wa fitina ngoja tuendelee kuusoma mchezo ,walianza kutuma ujumbe wakati wa uchaguzi wa meya Ilala na vikatuni vyao vya nguruwe na red carpet, ngoja tuendelee kuangalia hii ngoma.
 
Inawezekana sana mkuu kuwa na bifu na raisi na unaishi nchini ,kwani Nyerere aliwaweka watu kizuizini kwa sababu gani ??? Au utawala uliopita Lowasa na Jk walikua na nini ??
Point yangu nafikiri imekupita utosini mkuu. Kilichowatokea hao waliokuwa na Bifu na Rais nadhani unakielewa. Na Huyo jamaa uliyemtaja alikuwa na Bifu na Mh Rais nafikiri matokeo yake uliyaona mpaka sasa hivi anaishia kuwa mhamasishaji wa madiwani. Politricks is a nasty game.
 
Point yangu nafikiri imekupita utosini mkuu. Kilichowatokea hao waliokuwa na Bifu na Rais nadhani unakielewa. Na Huyo jamaa uliyemtaja alikuwa na Bifu na Mh Rais nafikiri matokeo yake uliyaona mpaka sasa hivi anaishia kuwa mhamasishaji wa madiwani. Politricks is a nasty game.
Mkuu wewe labda ndio point yangu imekupitia utosini hapa hatuongelei matokeo ya bifu ,tunaongelea uwezekano wa bifu kutokea ,na ndio nikakujibu hilo linawezekana vizuri na nikakutolea mifano ,sasa kama mtu kaleta bifu na raisi akaishia kuwekwa kizuizini au vinginevyo hilo ni swala jingine
 
Back
Top Bottom