Mei Mosi imepita vizuri sana! Manyanyaso kwa wafanyakazi yataongezeka zaidi baada ya Uchaguzi!

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
652
1,058
Hapo zamani na pengine hata sasa jamii nyingi za Kiafrika watoto walikuwa wakizuiwa kula nyama ya ubongo - wanaopaswa kula ni watu wazima tu - yaani katika familia ni baba tu. Kwa kweli mpaka sasa naona ndivyo ilivyo sehemu nyingi - uhakika kabisa baadhi ya wazee kijijini kwangu Idukilo baada ya kuwaulizia watoto wao nimeambiwa ni kweli hawagusi ubongo km amechinjwa mfugo km mbuzi, kondoo au ng'ombe. Ndivyo ilivyo!

Kwa kuwa nilikuwa mtumishi wa umma na nimekuwa na machungu sana na manyanyaso ya watawala hawa waliosababisha nikauchukia utumishi wa umma - hata leo nimeona ni vema kuongelea maslahi ya wafanyakazi hawa mara tu baada ya kupita siku tatu za Sikukuu yao Duniani - yaani Mei Mosi. Wafanyakazi hawa wamebaniwa kuongezewa mishahara na hata marupurupu mengine kama ambavyo hufanyika kwa zuio la kula ubongo, wakati watawala wenyewe wakila huo ubongo kwa namna tofauti. Nani asiyejua kuwa wale waliopo kazini na Rais kule alipo sasa wanakula tu per-diems zao kama kawaida. Lakini Mwl leo hata kama anaumwa na napaswa kusafirishwa kwenda matibabuni kutoka idukilo hadi bugando tu hawezi kulipwa hata per-diems, ajabu sana. Kuna viongozi mbalimbali wameitwa na Mkulu kule alipo na nina uhakika wamekula per-diems za kutosha. Hao pengine wangekuwa makao makuu kule Dodoma wasingekula hizo perdiems.

Tanzania ina wala ubongo na wala nyama za kawaida. Nilipitia Sheria ya kumlipa pensheni Mkuu wa Nchi na Viongozi wengine wa juu nikaona jinsi walivyo wala ubongo hapa nchini iliyosainiwa na Msukuma mwenzetu Masaju baada ya kufanyiwa marekebisho Mwaka 2016 kipindi cha Mukulu huyu nikashangaa kabisa. Rais na baadhi ya viongozi wa kisiasa, pamoja na mishahara mikubwa na marupurupu mengine kibao bado hawachangii kwenye Mifuko ya Pensheni na badala yake wale wafanyakazi wa chini ambao na marupurupu yao ni madogo madogo na pengine hawana kabisa ndiyo wanachangia kwenye hiyo Mifuko na pia fomula ya kuwatengenezea mafao yao wanatengenezewa na hao hao wala ubongo. Sasa maruprupu ya Rais kama yalivyoainishwa kwenye Kifungu cha 9 cha Sheria hiyo ni kiasi hiki:
- analipwa pensheni ya kila mwezi ambayo ni sawa na asilimia 80 ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani mpaka atakapingia kaburini na haikatwi kodi.
- analipwa nusu ya mishahara yake yote aliyotumikia akiwa kama Rais kama penshni ya mkupuo
-akisafiri nje ya nchi yeye na mwenza watalipwa perdiems na kuwa na msaidizi.
-akisafiri nchini gharama zote pamoja na dreva ni za serikali,
-atapewa winding allowance,
- magari mawili ya kumhudumia kila baada ya miaka mitatu
-nyumba
-sekretari
-msaidizi binafsi
-mlinzi
-mhudumu mmoja (office attendant)
-mpishi,
-dobi
-mfanyakazi wa ndani (domestic servant)
-shamba boy (gardener)
-madreva wawili, nk.

Kumbuka tena kuwa Rais na viongozi wengine hawakatwi kwenye mishahara yao michango ya kwenda Mifuko ya pensheni. Ndiyo maana wao Mifuko hata isipoweza kulipa wastaafu hawajali kitu sababu ubongo wanakula wao.

Kilichonisababisha nikaacha kazi ni kwa mambo kama haya nyeti kuwaacha wanasiasa wanatupangia huku wao wakipendelea waziwazi. Vyama vya kutetea wafanyakazi hamna kitu kabisa - tena ni wapu..bavu tu. Ona Mei Mosi hii inapita hata katamko tu kutoka kwa Chama chochote cha Wafanyakazi kuhusu hatima yao hamna. Yaani nchi hii - ndiyo maana hata dalili zinaonesha wazi kuwa tunaficha visa vya corona. Hatuna kabisa uzalendo na upendo kwa nchi yetu na watu wetu.

Sasa kama mishahara yenyewe haijapanda na watu wanakula per-diems huko Chato, wewe unafikiri baada ya uchaguzi unaotegemewa kuwa wa kibabe tu ndiyo mambo yatakuja kuwa mazuri. Tena wote wale walioonekana ni watu hatari kama kina Membe ambao angalau wangeweza kuleta mabadiliko ndiyo hawatakiwi kabisa. Wamejificha angalau waendelee hata kuishi tu.

Basi tuendelee kuwa watoto - kula ubongo mwiko!
 
Back
Top Bottom