Mdogo Wangu anataka nimfungulie biashara hii

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,025
2,257
Wakuu habari

Nataka nimfungulie biashara mdogo wangu nikamuuliza kwanza biashara gani amefikilia kuifanya kwa mtaji wa chini ya 500,000 kaniambia kuuza ndizi mzuzu ,Yani anaenda kuchukua mizogo kule morogoro (mbingu) afu anakuja kuuza huku kwa reja reja.(Kwa mafungu )

Kuna mambo nataka binafsi kufahamu nifahamu mwenye kujua anisaidie .

kwanza ulaji wa ndizi mzuzu kwa dar upoje mkubwa au mdogo,

Pili maeneo gani biashara hii inaweza kufanya vizuri ,

Tatu mkungu mmoja kwa mkulima unaweza kuwa shingapi

Kiasi nimevutiwa na wazo la dogo ila Sina detail za soko la zao hili hasa kwa hapa dar.

Karibuni
 
Hio hela umeongeza sifuri ama ipo sahihi?
Wakuu habari

Nataka nimfungulie biashara mdogo wangu nikamuuliza kwanza biashara gani amefikilia kuifanya kwa mtaji wa chini ya 500,0000 kaniambia kuuza ndizi mzuzu ,Yani anaenda kuchukua mizogo kule morogoro (mbingu) afu anakuja kuuza huku kwa reja reja.(Kwa mafungu )

Kuna mambo nataka binafsi kufahamu nifahamu mwenye kujua anisaidie .

kwanza ulaji wa ndizi mzuzu kwa dar upoje mkubwa au mdogo,

Pili maeneo gani biashara hii inaweza kufanya vizuri ,

Tatu mkungu mmoja kwa mkulima unaweza kuwa shingapi

Kiasi nimevutiwa na wazo la dogo ila Sina detail za soko la zao hili hasa kwa hapa dar.

Karibuni
 
Wakuu habari

Nataka nimfungulie biashara mdogo wangu nikamuuliza kwanza biashara gani amefikilia kuifanya kwa mtaji wa chini ya 500,000 kaniambia kuuza ndizi mzuzu ,Yani anaenda kuchukua mizogo kule morogoro (mbingu) afu anakuja kuuza huku kwa reja reja.(Kwa mafungu )

Kuna mambo nataka binafsi kufahamu nifahamu mwenye kujua anisaidie .

kwanza ulaji wa ndizi mzuzu kwa dar upoje mkubwa au mdogo,

Pili maeneo gani biashara hii inaweza kufanya vizuri ,

Tatu mkungu mmoja kwa mkulima unaweza kuwa shingapi

Kiasi nimevutiwa na wazo la dogo ila Sina detail za soko la zao hili hasa kwa hapa dar.

Karibuni
Wewe ndiye mwenye wazo hili
Unajificha nini
 
Sifahamu uelewa plus uzoefu wa dogo kuhusu biashara ya ndizi. Ila kwa kutumia akili ya kawaida laki tano uende Mbingu tena ndani ndani then uchukue mikungu ya ndizi mpaka Dar!

Amepiga gharama za uendeshaji plus dharula zake vizuri au anaendeshwa zaidi na nadharia?? Iwe kwa gari au treni bado ni ngumu kwa huo mtaji.

Ushauri :

1)
Kama anataka kuuza rejareja, aende masoko ya ndizi ya dar, kwa huo mtaji bado ana nafasi ya kutoboa.

2) Aende Turiani coz ana uwezo wa kwenda na kurudi achukue hiyo mikungu.

3) Mpe aende kisha ajifunze uhalisia wa mambo ambao utampa uzoefu mkubwa hata kama akipoteza.

Nb: Dogo anawaza kubeba mikungu mingi kichwani huku akisahau kuwa kuna gharama zake na mtaji mdogo! Kama uwezo upo muongezee mtaji.

Ni mtazamo tu!
 
Back
Top Bottom