Kuelekea 2025 Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa: Nchimbi kaingia mitini, wengine wagoma kushiriki!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
ingekua ajabu ya dunia, eti daktari mzima wa falsafa Comrade Dr.Emmanuel Nchimbi kushiriki hicho kinachoitwa mdahalo usio na kichwa wala miguu, na hao vijanaa waliobebeshwa tu majina ya ukatibu mkuu kwenye vyama vyao, lakini kiuhalisia ni shadow SGs, hawana hadhi wala uwezo wa majukumu hayo kitaalamu 🐒
Kwa maana hiyo Rais Samia asiitwe Rais kwasababu kwa hadhi ya Urais halingani na Rais wa Marekani, Uchina na nchi zingine zilizojuu ya Tanzania kimaendeleo?
 
A
Katibu Mkuu wetu Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Yupo kwenye vikao vizito sana katika maandalizi ya kikao maalumu cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kitakachoketi Tarehe 2 septemba chini ya uwenyekiti wa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Hivyo hawezi kuacha vikao hivi halafu aende huko kwingine.Kumbuka macho na masikio yoote ya watanzania yameelekezwa kwenye vikao vya CCM na kusubiri kwa hamu na shauku kubwa na nzito Maazimio yake.View attachment 3083807
Nasema hivi, nimecheka kwa nguvu vibaya. Hayo ndio madhara ya kufanya siasa za kutegemea mbeleko za vyombo vya dola, mkiitwa sehemu isiyo na mbeleko ya vyombo vya lazima mkimbie. Nani ana muda wa kufuatilia mkutano wa chama cha majizi, yaani watu wafuatilie mkutano wa kupanga watu kutekwa!
 
Kutoshiriki pia ni mbinu kujua mawazo ya wengine.

Nchimbi hajakimbia mmekurupuka kusema amekimbia ilihali anaandaa vikao vya chama .. muda upo anaweza kupanga wakati mwingine baada ya kamati kuu akashiriki mdahalo

Nyie ongeeni tu tunawasikiliza
 
Kwanini Nchimbi hakuwakilishwa na Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah ? Hawa jamaa ni ma genius!
for sure ningeomba udhuru w kutoshiriki hicho kihoja kisicho na maana yoyote tena kwa wanaoitwa eti makatibu wakuu ambao ninajua fika they are pure shadow SGs,

kwenye hili mbobevu nisingeweza kabisa kumkubalia katibu Mkuu makini sana wa CCM, na kwakweli ningemshauri afutilie mbali wito huo kwenye ratiba za CCM, apuuzilie mbali mdahalo huo, kwani hauna tija wala afya kwa hadhi na siasa za Chama Cha Mapinduzi 🐒
 
Naangalia mdahalo ila naona Mrangazaji kama anatoa machozi kwa kukosekana makatibu wakuu chanzo kikitajwa kuwa ni kutofika kwa Katibu Mkuu wa CCM, Dr. Emmanuel Nchimbi.

Inasikitisha sana, ila leo CCM imevuna aibu kubwa sana kwa tukio hili.

Tusubiri drama za kujitetea na kujisaficha baada ya kuharibu.

Anyway, Mungu ana makusudi na kila jambo.
 
Katibu Mkuu wetu Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Yupo kwenye vikao vizito sana katika maandalizi ya kikao maalumu cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kitakachoketi Tarehe 2 septemba chini ya uwenyekiti wa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Hivyo hawezi kuacha vikao hivi halafu aende huko kwingine.Kumbuka macho na masikio yoote ya watanzania yameelekezwa kwenye vikao vya CCM na kusubiri kwa hamu na shauku kubwa na nzito Maazimio yake.View attachment 3083807
Kwendraaa! Hoja ya kijinga kabisa hiyo
 
ingekua ajabu ya dunia, eti daktari mzima wa falsafa Comrade Dr.Emmanuel Nchimbi kushiriki hicho kinachoitwa mdahalo usio na kichwa wala miguu, na hao vijanaa waliobebeshwa tu majina ya ukatibu mkuu kwenye vyama vyao, lakini kiuhalisia ni shadow SGs, hawana hadhi wala uwezo wa majukumu hayo kitaalamu 🐒
Bwahaa, bwahaaaaa, yaani nimecheks kwa nguvu hadi mtoto wangu kaamka. Tunaposema mnategemea mbeleko ya vyombo vya dola huu ndio ushahidi. Sehemu ambayo hamna mbeleko ya vyombo vya dola hamuwezi kutia team. Nyie mtaishia tu kupora uchaguzi kwa kubebwa na vyombo vya dola. Na siku hivyo vyombo vya dola vikiacha mshindane kwa haki, ndio kiama chenu.
 
Fuatilia live Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM.​

Fuatilia mubashara Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM ambapo wanaotazamiwa kushiriki ni;

1. Dk. Emmanuel Nchimbi - CCM
2. Martha Chiomba - NNCR Mageuzi
3. Ado Shaibu ACT Wazalendo
4. Ahmad Masoud - CUF
5 John Mnyika - CHADEMA

Odemba akitangaza kwa masikitiko makubwa huku akilia amewaambiwa waliofika kwenye mdahalo huo kuwa Nchimbi mpaka muda huu hajatokea kwenye mdahalo, ambapo Mnyika amefika kwenye mhalo huo lakini kutokana na kuwa Nchimbi hayupo hivyo naye hatoshiriki kwenye mdahalo huo.

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shahibu amefika kwenye mdahalo huo, lakini kwakuwa wa CHADEMA na CCM hawashiriki naye pia amegoma kushirki, NCCR Mageuzi walituma mwakilishi, ila kwakuwa wengine hawashirki nao pia wamesema hawatashiriki.

Odemba amelaani vikali kilichotokea, lakini mjadala unaendelea hata baada ya changamoto hii kutokea ambapo yaliyopangwa kujadiliwa yatakuwa mjadala wa wazi kwa washiriki waliofika.

Hao wanaokwepa midahalo hawana cha kuongea ?....Ccm ya kina Pascal Mayalla Ina vituko kweli kweli
 
Back
Top Bottom