Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 528
- 1,254
Fuatilia live Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM.
Fuatilia mubashara Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM ambapo wanaotazamiwa kushiriki ni;1. Dk. Emmanuel Nchimbi - CCM
2. Martha Chiomba - NNCR Mageuzi
3. Ado Shaibu ACT Wazalendo
4. Ahmad Masoud - CUF
5 John Mnyika - CHADEMA
Odemba akitangaza kwa masikitiko makubwa huku akilia amewaambiwa waliofika kwenye mdahalo huo kuwa Nchimbi mpaka muda huu hajatokea kwenye mdahalo, ambapo Mnyika amefika kwenye mhalo huo lakini kutokana na kuwa Nchimbi hayupo hivyo naye hatoshiriki kwenye mdahalo huo.
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shahibu amefika kwenye mdahalo huo, lakini kwakuwa wa CHADEMA na CCM hawashiriki naye pia amegoma kushirki, NCCR Mageuzi walituma mwakilishi, ila kwakuwa wengine hawashirki nao pia wamesema hawatashiriki.
Odemba amelaani vikali kilichotokea, lakini mjadala unaendelea hata baada ya changamoto hii kutokea ambapo yaliyopangwa kujadiliwa yatakuwa mjadala wa wazi kwa washiriki waliofika.
Mambo ambayo watu watashiriki kwenye mjadala huu ni nini kifanyike kuhusu watu kukamatwa ama kupotea kipindi cha uchaguzi, tufanye nini ili tuwe na uchaguzi wenye tija na kupata viongozi bora pamoja na nini maoni ya watanzania kuhusu makatibu wa vyama vya siasa nchini kukimbia midahalo?
Baadhi ya hoja zilizotolewa na wahudhuriaji
- Wahudhuriaji wengi walaani kitendo cha Nchimbi kuingia mitini kwenye mdahalo huu na kusema wanatoa mfano mbovu kwa vijana ambao wanawaangalia na kujifunza kutoka kwao
- Baadhi ya wadau wasema watu hupotezwa kwa hofu ya CCM kushindwa uchaguzi
- Watanzania tuungane kupinga vitendo vya utekaji
- CCM wanaenda kinyume na 4R za Rais Samia
- CCM ni wazuri kungumza lakini vitendo ni 0
- Vijana wa CCM wamechukua njaa tumboni wameihamisha kichwani, ofisi ya katibu mkuu ina watu watendaji wingi, Nchimbi angeweza kuacha watendaji wengine na akafika kwenye mdahalo
- Uchaguzi wa mwaka huu (2024) CCM wamejipanga kufanya mabaya na ndio maana wamekimbia mdahalo sababu walijua wataulizwa kuhusu hayo
- Jeshi la polisi ni kwaajili ya wananchi wote na siyo chama, hivyo wasijihusishe na masuala ya kisiasa na waache vyama vipambane
- Vyombo vya Habari watoe habari za ukweli bila hofu, sababu kwa kuweka hofu wanakuwa wanalea mambo ya hovyo na wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa vyama vya upinzani
- Majibu ya CCM Mdahalo wa Odemba: Tunasikitishwa na jinsi alivyoupotosha umma, tumeshangazwa na machozi yake!