Mchungaji Lusekelo kumchulia kifo Nay wa Mitego, sio jambo dogo

MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
518
613
Wakuu kama sikosei mwezi uliopita alisikika Mchungaji Anthony Lusekelo kwenye ibada ya jumapili kanisani kwake huko ubunge kibangu, akimtolea povu Msanii Emanuel Elibariki aka Nay Wa Mitego , kisa ni Nay kusema: nitajenga kanisa la kuabudu watu wote.
Mzee Lusekelo alienda mbali na kuthubutu kusema Mtoto Nay atakufa ndani ya miaka mitatu.
Ninacho uliza sasa kwani Makanisa ya wakiristu yanajengwa na watu maalum?
Je ukristu unasemaje, kuhusu kumchulia binadamu mwenzako kifo?
Je tabia hii ya mchungaji huyu ni MAONO au niakili zake? Coz sio mara yake ya kwanza, hata waandishi wa habari aliwahi kuwachulia kufa.
Mwisho nauliza Je kisheria sikosa kumuambia mtu utakufa ndani ya miaka mitatu?
 
Mwaka huu tutazika wengi kufuatia unabii wa Mch. Lusekelo..... wale waandishi wa habari walioripoti tukio la Mzee wa Upako kuwa amejazwa upako wa ile product pendwa ya Tanzania Distilarizi, mmeshajiandaa?? Da Happy Muyabazi sijui ushafanya toba dadangu?
 
Hv ndio alisema mwez huu wa 3 means tujiandaae na michango au sio
 
Mpumbavu tu huyo, anafikiri sadaka ana hatimiliki yeye peke yake? Au anadhani wenzake hawapendi kula bata kama yeye anavyolewa kwa raha zake, biashara ushindani ati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…