Mchungaji Daniel Mgogo anasema Sadaka zinatolewa hili ziliwe na wachungaji. Mungu hana account ya kupokelea Sadaka, Wachungaji ndio Meno ya Mungu

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
3,191
7,322
Pastor Daniel Mgogo anasema sadaka zinatolewa hili ziliwe na wachungaji, maana Mungu hana account ya kupokelea pesa za sadaka.

wachungaji ndio wawakilishi wa Mungu hivyo wana haki ya kuzila sadaka kwa niaba ya Mungu


 
Yupo sahihi nawao ni moja ya wawakilishi wa Mungu,wakiwemo Mafukara,Masikini,Mayatima,Walemavu na wajane.
Wewe kama umeamua kuchagua kumpa yeye usilalame,hayo makundi mengine yapo katika jamii umeshindwa nini kuwapelekea?

wachungaji hao hao wanapinga ukisema sadaka yako ama fungu la kumi lako unapeleka kwa yatima ama wajane.

unatengwa na kanisa kwamba sio mtoaji wa sadaka, na unajaziwa madeni kanisani kupitia jumuia
 
Sisi masikini inabidi tuombewe Ili tupate sadaka zaidi za kuwapa wachungaji
 
Maneno ya mchungaji yamenivunja sana moyo wa kutoa sadaka.

Nimeacha kutoa sadaka kanisani, maneno ya huyu mchungaji yameniumiza sana. Kwamba sadaka ni chakula cha wachungaji. Mungu hana Account ya kuwekewa pesa.

wanatuambia Toa fungu la kumi , utabarikiwa!!!!, usipotoa umemuibia Mungu. halafu baadae wanasema Mungu hana account ya kupokelea pesa

 
Kwahiyo kumbe siku zote ulijua sadaka zinaliwa na Mungu?

Toa sadata usaidie kupeleka injili kwa watu.

nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya
 
Back
Top Bottom