Mchumba wangu wa miaka 5 anafunga ndoa kesho inaniuma sana, nifanyaje?

trojan92

Member
May 18, 2024
91
276
Mapenzi yanauma kuliko chochote sababu hayana dawa kabisa. Huyu binti nilimpenda kupenda, anatembea na nusu ya uhai wangu.

Tumekuwa kwenye mahusiano muda mrefu na tulipanga mengi, nilijitahidi kumridhisha katika mahitaji yake ya kimwili, kihisia na kiroho. Kwa bahati isiyo yangu binti katamka kuwa hanitaki yaani amekutana na better half hivyo anafunga ndoa.

Alivyo na jeuri kanipa na kadi kabisa. Hapa nimepanga na wahuni wa kitaa tukamharibie. Yaani hawezi niacha kizembe hivi. Ameanzisha lazima nimalizie, ngoja leo nilewe kabisa.
 
Title imekaa kuwa unaomba ushauri ufanyeje ila ndani ya uzi tayari una uamuzi wako sasa sijui kipi ni kipi. Ila kama hicho ulichoandik ndicho kweli unapanga kukifanya sidhani kama ni sahihi. Kitakupa ahueni ya muda mchache lakini baada ya muda fulani utakuja ujutie na kujiona mjinga.

Nenda harusini, kula, shiba, cheza amapiano, rudi kalale. Kama huwezi kaa ndani kwako liaaa mpaka uchungu uishe na baada ya muda utakuwa sawa...

Naomba kuwasilisha...
 
Move on kijana
 
Kibali tu mkuu, it's over
 
Jitahidi uachane naye .
Mwenzio niliachwa na wife na tumezaa ila akaomba talaka na akadhibitisha watoto si wangu alafu nikapewa kadi ya harusi siko alipoolewa na bwana mpya ,nilihudhuria nilikuwa kila muda naenda chooni kufuta machozi na kurudi ukumbini ila sikufanya chochote zaidi nakumbuka nililewa Sana mpaka wakanibeba kunipeleka kwangu .

Alafu asubuhi nilikaa kikao na halmashauri ya kichwa changu ili tujadili kilichojiri na kipi kinafanyika ,halmashauri na kichwa kwa pamoja turiridhia kuacha yaliyopita yapite ,Sasa ni miaka mingi nipo nadunda na mzima wa afya kaka .

Jifunze kukubali yapite ndugu ,uhai na afya yako ni Bora kuliko mapenzi ,dah umeniumiza Mara ya pili nimeandika nalia tena 😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Sio kweli kabisa...πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…