Mbunge wa Ukonga, Chacha Waitara kazi imekushinda

NAAMINI

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
672
234
Habarini wanajamvi.....

Ilikuwa mwaka 2015 wakati mbio za uchaguzi zilipoanza na kipenga kupulizwa nikiwa mmoja wa vijana tusio na upande nikisubiri sera za wagombea kuzisikia ingawa kwa ccm sikutaka kabisa kumsikia mayor slaa kwahiyo nikawa na shauku ya kumuona mkombozi mpya wa jimbo la ukonga,.

Siku ilipowadia sisi vijana, bodaboda,madereva bajaji, wazee,akina mama kwa akina baba tulio wengi tulienda na waitara chacha tukiamini kuwa anakuja kuleta ukombozi uliotukuka wa Jimbo la ukonga.

Miaka michache iliyopita aliepata kuwa mbunge wa ukonga EUGEN Mwaiposa ambaye kwasasa ni marehemu tuliwahi anzisha vuguvugu la kumuondoa tulipodai barabara ya kutoka mombasa kuja moshi bar nakumbuka vikao vilianzia masika bar badae meseji zikapita tukaanzisha vikao vya watu ukonga pale uwanjani kwa temba hakika muitikio ulikuwa mkubwa hadi ukamfanya mwaiposa Eugen akiwa na mayor kuja kuzungumza na kuanza harakati za ujenzi wa barabara.

Nimeanza na historia ya nyuma kidogo ili ujue tulipotokea, tulipo na tuendapo. CHACHA WAITARA umepokea jimbo barabara zikiwa njema na za kutukuka, bodaboda wakiwa na furaha kidogo mombasa,banabana,gongo la mboto n.k.,umepokea jimbo likiwa njema kwa sisi wafanyabiashara na kulikuwa hakuna maonevu yoyote.

KIKAO KILICHOKAA UWANJA MPANA RELINI CHA WANYWAJI JUMAMOSI.

KUHUSU BARABARA.

KUANZIA NJIA PANDA-BANANA,BANANA-KITUNDA,MOMBASA-MOSHIBAR-MKOLEMBA-DIWANI,GONGO LA MBOTO-MAJOHE N.K. BARABARA KWA UJUMLA NI MBOVU SANA NA HAZITAMANIKI, MH.MBUNGE UPO DODOMA UKISIMAMA KUONGEA UNAONGELEA SIASA ZA CCM NA CHADEMA BADALA YA KUWASILISHA MALALAMIKO HAYO....Hii barabara usipokuwa makini hivi karibuni yatatokea kama ya mwaiposa na uzuri wa huku ukonga hatuna masihara.

SISI BODABODA NA BAJAJI..

Tulikupigania sana na tulifanya kampeni nyumba kwa nyumba,abiria wote tuliwaambia wakupatie kura mh. ila kinachoendelea ni usanii mtupu hasa kwa tunayofanyiwa..MH.WAITARA umetusahau na ututhamini tena, tunapigwa fines zisizo na msingi, diwani wako shehe mwaipopo nae sauti haisikiki tena kweli mpe mtu uongozi utajua tabia yake.

Tuliwahi muita diwani atusaidia kutengeneza kajibarabara pale mombasa ili bajaji na pikipiki zipite salama na kuondoa foleni barabara kuu ahadi hiyo imekuwa haitekelezeki na bado miaka miwili..mwambie mwaipopo tutamshangaza...

Hatuna amani ya kufanya biashara mombasa,gongo la mboto na hata banana sababu ya hofu ya fines zisizo na maana..

Yapo mengi ila kwa leo nikuachie na nukuu ya mwalimu nyerere

Kazi ya kuchagua viongozi ni kazi ya wanachama wananchi; kwamba jambo hili ni kubwa sana. Haifai kuchagua kiongozi kwa sababu ni mjomba, au binamu au ana sauti au sura nzuri. Wala haifai kuacha kumchagua mtu kuwa kiongozi kwa sababu kama hizo. Jambo kubwa ni kuchagua kiongozi mwenye tabia nzuri na anayeweza kazi. Hatuna budi tutii kanuni hii katika kuajiri wafanya kazi katika TANU au serikalini. Hawa pia hawana budi wachaguliwe kwa sababu wanaiweza kazi wanayoajiriwa kufanya, na ni watu wenye tabia nzuri.

Kujuana na ukabila vilituponza tukachagua uongozi usiotumikia watu, Endelea kula bata dodoma, bishana juu ya uccm na uchadema, siku zaja.....


Ni mimi mwanywaji wa pombe masika bar, Luko bar, na uwanja mpana(relini),mzambarauni, na big jons.
 
UKONGA HAKUNA MBUNGE ANAITWA chacha waitara, MBUNGE WA UKONGA ANAITWA mwita mwikwabe waitara. HUENDA UKAWA UNAMAANISHA UKONGA YA NANJILINJI GEZA ULOLE. POLE
 
Huyu jamaa hafai, ila ni mwiko kuwapa jimbo ccm, ccm ni mkosi kwa Taifa.

Vyama mbadala vichuje vizuri wagombea wamlete mgombea mwingine huyu jamaa hana uwezo naunga mkono hoja.
Huyu jamaa ni kupiga chini...vikao vimeanza nitazidi wapa taarifa.
 
Kazi ya kujenga barabara ni ya serikali, sio ya mbunge, mbunge hakusanyi kodi, uliza ziko wapi 1.51T.
Kazi ya mbunge ni kuishauri serikali na kuikumbusha juu ya matatizo ya jimbo lake...yeye akipewa nafasi utakuta anatoa povu la itikadi za chama badala ya kupigia kelele miundo mbinu..nakuhakikishia huku ukonga atuangalii uchama ukizingua either kamanda au kada tunakupiga chini...tulia usikilize mchezo unavyoenda..kama upo nae karibu mkumbushe
 
UKONGA HAKUNA MBUNGE ANAITWA chacha waitara, MBUNGE WA UKONGA ANAITWA mwita mwikwabe waitara. HUENDA UKAWA UNAMAANISHA UKONGA YA NANJILINJI GEZA ULOLE. POLE
ujumbe umefika, sasa kama hayo maeneo mengine tajwa yapo nanjilinji basi amen...subiri 2020 utaona kama waitara wa nanjilinji au gezaulole
 
kwa nini usigombee wewe naona kazi utaimudu
nashukuru sana kwa ushauri...naufanyia kazi..ila msalimu waitara kazi imemshinda...ukonga sio tarime...mjini lazima uwe na pesa ili uongoze ukitegemea kila kitu serikali utakwama....yameshamkuta
 
Back
Top Bottom