Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu amwaga chozi hadharani akiwa kwenye ziara ya kukagua changamoto za shule hasa vyoo na madarasa

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
6,380
13,440
Ndugu wana jamii tafadhali pokea taarifa hiyo yenye uchungu mkubwa toka kwa Mhe. Tabasamu ametoa machozi hadharani, mwenye video tafadhari atuwekee hapa.

Video ipo kwenye comments (Manjagata ameiweka)

Hii ni taarifa halisi isipokuwa kwa kuwa sina video ndio mana sijaweka katika uhakika wake.

Tuendelee kuliombea taifa linapitia wakati mgumu sana, hio Shule yenye changamoto ya vyoo Iko kilometa 3 tu kutoka ofisi za halmashauri ya Sengerema. Mkurugenzi yupo, CCM ipo, Mwenyekiti wa halmashauri yupo, Madiwani wapo, Wakaguzi wa Shule wapo, waratibu wapo, watendaji wapo na kamati za shule na vijiji zipo.

Nawatakia bidii katika kuliombea taifa linapitia wakati mgumu sana.

Wadiz nikiwa viunga vya Dodoma
 
Ndugu wana jamii tafadhari pokea taarifa hiyo yenye uchungu mkubwa toka kwa Mhe. Tabasamu ametoa machozi hadharani, mwenye video tafadhari atuwekee hapa.

Hii ni taarifa halisi isipokuwa kwa kuwa sina video ndiomana sijaweka katika uhakika wake.

Tuendelee kuliombea taifa linapitia wakati mgumu sana, hio Shule yenye changamoto ya vyoo Iko kilometa 3 tu kutoka ofisi za halmashauri ya Sengerema. Mkurugenzi yupo, CCM ipo, Mwenyekiti wa halmashauri yupo, Madiwani wapo, Wakaguzi wa Shule wapo, waratibu wapo, watendaji wapo na kamati za shule na vijiji zipo.

Nawatakia bidii katika kuliombea taifa linapitia wakati mgumu sana.

Wadiz nikiwa viunga vya Dodoma
IMG_7950.jpeg
 
Tabasamu ni mbunge halisi wa wananchi, na muislamu wa kweli kabisa mwenye dini yake na anaishi dini Kila siku
Ohh.. Ila la DP World na wamasai kuondolewa ngorongoro halimuumi na dini ya haki anayo😁😁.. Asijitafutishe Kiki bana siku zote iyo shule ipo mbona hajafanya kitu... Sasa hivi ndio wanajirudisha ma jimboni kujiosha baada ya Sakata la DP World kuwaaibisha ufidhuli wao?
 
Hizo ni Drama !!, Kwamba yeye ni mgeni nchini na hakujua kuna changamoto kama hizo; Inaonyesha yupo out of touch na hajui kinachoendelea which is worse..
Si muda mrefu wataanza kupiga magoti na kijigaragaza kwenye mikutano.Kiinua mgongo cha milioni zaidi ya mia mbili(200,000,000/=)humfanya mtu kuwa kibweka.Jumlisha na mshahara wa zaidi ya 13,000,000/= kila mwezi.
 
Siku zote hajayaona hayo leo ndio aje ajilize? yeye kama Mbunge wao alifanya nini labda kama iyo shule kaijua leo.. unafki wa kiwango cha juu janaume kujiliza
 
Back
Top Bottom