Mbunge Vedasto Ngombale (CUF) ''ahenyeshwa" na Magufuli Somanga

Wakuu,
Katika ziara ya Mhe Rais katika Mkoa wa Lindi,amefanya mengi!
Ila moja la kufurahisha ni kumbwaga chini mbunge wa eneo husika katika kuwajari wananchi wa Somanga!
Wananchi walipoomba zahanati,Magufuli ametoa 2o millioni,Mkurugenzi 10 millioni,na mbunge ametoa 0 millioni!
NB:
Wapinzani mjiandae,Operesheni Funika Upinzani Imeanza!
Wametoa wapi hizo fedha?
Acheni utani na hela za wananchi nyie.

Ni jukumu la serikali kuwaletea wananchi huduma muhimu si ombi ni lazima kutokana na kodi wanazolipa ktk kila kitu.
Shule, huduma za afya, miundombinu, Maji,umeme, ...... ni wajibu wa serikali kutekeleza hayo.
Kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali siyo kuja kutoa 20/10m kusiko julikana zimetoka wapi.

Mambo mengine muache kujidhalilisha wenyewe
 
Mawazo duni ni umasikini wa kudumu, sasa Magufuli hizo pesa kafanya kazi gani kuzipata?
Huyo mkurugenzi kafanya kazi gani kupata hizo pesa?

Unakuja hapa mbio mbio unasifia rais katoa pesa kutoka wapi?
Lini ulisikia hii serikali ina pesa zake tofauti na kodi inayokusanywa kutoka kwetu?

Ulitaka mbunge atoe pesa zake mfukoni kuwapa wananchi?

Tuanche unafiki watanzania, tufanye siasa safi sio majungu na umbea.

Ieleweke sina chama wala sitakuja kua na chama na kwa kazi yangu siwezi kua na chama chochote cha siasa wala sina interest.
JPM alimuuliza huyo mbunge juu ya fedha za Jimbo, akampigia hesabu mpaka alizopewa kwa sasa, akamuuliza hapo Somanga kaleta ngapi, akasema Sh mil 3, hivyo akamuuliza kama anaweza kuongeza au kuchangia ujezi wa hiyo zahanati kutoka katika fedha za mfuko wa jimbo anazopewa. Akajikanyaga
 
Mawazo duni ni umasikini wa kudumu, sasa Magufuli hizo pesa kafanya kazi gani kuzipata?
Huyo mkurugenzi kafanya kazi gani kupata hizo pesa?

Unakuja hapa mbio mbio unasifia rais katoa pesa kutoka wapi?
Lini ulisikia hii serikali ina pesa zake tofauti na kodi inayokusanywa kutoka kwetu?

Ulitaka mbunge atoe pesa zake mfukoni kuwapa wananchi?

Tuanche unafiki watanzania, tufanye siasa safi sio majungu na umbea.

Ieleweke sina chama wala sitakuja kua na chama na kwa kazi yangu siwezi kua na chama chochote cha siasa wala sina interest.
Halafu wanasahau kuwa ni wajibu wa serekali kujenga mashule na zahanati. Elimu ya uraia inahitajika sana ili watu wajue yapi ni majukumu yao na yapi ni ya serekali.
 
Lisaidie jukwaa letu kwa kulitajia chanzo cha mapato cha mbunge hadi awe na uwezo wa kumwaga mamilioni kwenye miladi inayopaswa kufanywa na serikali.Hayo mamilioni unayoyaorodhesha hapa ukijaribu kuliaminisha jukwaa kuwa yametolewa na Rais na mkurugenzi ni mapato ya serikali kupitia kodi zetu,kusimama jukwaani kwa mbwembwe na kuwahadaa wananchi kuwa utatoa hiki na kile na wananchi wakashangilia utadhani italetwa cheque ya kiasi kilichotajwa yenye jina la mchangiaji ikidhibitisha ametumia hela zake kutekeleza ahadi yake ni sanaa zaidi ya ile ya kulia mbele ya kamera za wanahabari iliyofanywa na Stive nyerere.
Kuna jamaa mmoja ni mbunge wa Hai na KUB. Yeye hela zake za ubunge anakwendaga kuzitumbua Dubai na mbunge mwenzie wa viti maalum
 
Halafu ikifika 2020 wakishindwa uchaguzi wanaanza kulialia eti tume ya uchaguzi sio huru.

Muda huu baada ya kuutumia katika kuumiza kichwa kwenye kuyagusa maisha ya watu wa hali ya chini, wao wanahangaika na vyeti vya Makonda. Hii nchi imerogwa na mchawi ameshafariki siku nyingi zilizopita, mbaya zaidi hatujui kazikwa kaburi gani ili twende tukalitembelee.

Katika watu ninaowaheshimu hapa jukwaani ni ww Phillipo sikutarajia kama unaweza kushabikia jambo jepesi hivyo!! Ninachojua upatikanaji wa zahanati nchi nzima unafanywa na serekali kupitia mipango makini na sio jukwaani. Rais ana muda gani madarakani ama chama chake? Hilo tatizo la zahanati limeanza jana jioni? Sasa hapo sifa ya upatikanaji wa zahanati ni wa rais au wa serekali? Kama zahanati zitakuwa zinapatikana rais anapopita una uhakika gani huo mradi utaendelea hasa ukizingatia ni ahadi ya jukwaani? Mkuu miradi ikianza kutolewa kama zile sifa tunazofanya za kumuhonga mwanamke ili akuone una hela tutatoboa kweli? Anyway labda kwa kuwa uwezo wa wananchi ni wa maigizo ya hivyo sio mbaya. Ila nakuhakikishia huo mradi rudi ndani ya mwaka kama utaukuta unaendelea vizuri.
 
Wakuu,
Katika ziara ya Mhe Rais katika Mkoa wa Lindi,amefanya mengi!
Ila moja la kufurahisha ni kumbwaga chini mbunge wa eneo husika katika kuwajari wananchi wa Somanga!
Wananchi walipoomba zahanati,Magufuli ametoa 2o millioni,Mkurugenzi 10 millioni,na mbunge ametoa 0 millioni!
NB:
Wapinzani mjiandae,Operesheni Funika Upinzani Imeanza!

Hizo za Magufuli zimetoka wapi??Naona zimetoka kwa mfuko wa Serikali.Kila mtu anauwezo wake,hutakiwi kujikuna usipofikia.Hata huyo Mkurugenzi amesema tu lakini kweli hizo milioni kumi anazo?Au ndiyo zinaenda kuchotwa kwenye HALMASHAURI??

Mbona mie sioni cha maana hapo!Kwanini Serikali istoe pesa ikajenga hiyo zahanati mpaka mchangishane??
 
Wakuu,
Katika ziara ya Mhe Rais katika Mkoa wa Lindi,amefanya mengi!
Ila moja la kufurahisha ni kumbwaga chini mbunge wa eneo husika katika kuwajari wananchi wa Somanga!
Wananchi walipoomba zahanati,Magufuli ametoa 2o millioni,Mkurugenzi 10 millioni,na mbunge ametoa 0 millioni!
NB:
Wapinzani mjiandae,Operesheni Funika Upinzani Imeanza!

Kwa akili yako unafikiri anatoa hela zake za mshahara, hizo ni kodi zetu jisifu wewe kama unalipaga kodi....
 
Kuna jamaa mmoja ni mbunge wa Hai na KUB. Yeye hela zake za ubunge anakwendaga kuzitumbua Dubai na mbunge mwenzie wa viti maalum

Hongera sana.NAona Huwezi kula wala kulala bila kumtaja Mbowe.
 
Katika watu ninaowaheshimu hapa jukwaani ni ww Phillipo sikutarajia kama unaweza kushabikia jambo jepesi hivyo!! Ninachojua upatikanaji wa maji nchi nzima unafanywa na serekali kupitia mipango makini na sio jukwaani. Rais ana muda gani madarakani ama chama chake? Hilo tatizo la maji limeanza jana jioni? Sasa hapo sifa ya upatikanaji wa maji ni wa rais au wa serekali? Kama maji yatakuwa yanapatikana rais anapopita una uhakika gani huo mradi utaendelea hasa ukizingatia ni ahadi ya jukwaani? Mkuu miradi ikianza kutolewa kama zile sifa tunazofanya za kumuhonga mwanamke ili akuone una hela tutatoboa kweli? Anyway labda kwa kuwa uwezo wa wananchi ni wa maigizo ya hivyo sio mbaya. Ila nakuhakikishia huo mradi rudi ndani ya mwaka kama utaukuta.
Mkuu Tindo na wewe umeingia kwenye mtego ule ule.

Naongelea mindset nzima ya upinzani, labda wapo wachache wanaojielewa kama Joshua Nassari lakini wengi wao wanaendekeza masikhara hata kwenye masuala sensitive ya kitaifa.
 
Hatoi mfukoni kwake
Kama angekua msamalia mwema kiasi hicho basi angeacha kuchukua mshahara wake wa kila mwezi ambao ni millions of money
msamalia gani ambaye hachukuia pesa ,hivi maana ya msamalia nikuache kuchukua mshahara kumbe ,kwa hiyo rais wa chadema atakuwa hachukui mshahara.??
 
Na yeye angetoa kwenye mfuko wa mbunge au kashapelekea totoz dubai
Umeambiwa ana ATM card ya huo mfuko wa jimbo kiasi cha kwenda kutoa tu. Tusiwe wavivu kujielimisha hata kwa vitu visivyotuhusu moja kwa moja
 
Back
Top Bottom