Mbunge Twaha Mpembenwe: Nimekuja Kutatua Kero na Kutimiza Ahadi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,666
1,228
Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mkoa wa Pwani, Mhe. Twaha Mpembenwe ameongozana na Diwani wa Kata ya Kibiti, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kibiti na Sekretarieti ya CCM kufanya mkutano na kutatua changamoto za Wananchi wa Kata ya Kibiti.

"Nilifanya Ziara ya Kusikiliza Kero na Changamoto za Wananchi kwenye Kata ya Kibiti, Yapo Ambayo niliahidi na Sasa ni wakati wa Kutekeleza Yale Ambayo niliahidi. Nimeanza Ziara na Tukio la Kwanza Nimezindua Shina la Vijana Mwenge Jogging Club hapa Mwangia" - Mhe. Twaha Mpembenwe

"Nilikuja kufanya mikutano Kata ya Kibiti na kuna mambo tulikuwa tumezungumza na wananchi wetu na tukawaahidi kwamba tutakuja kuyatekeleza tukishirikiana na Diwani pamoja na viongozi wengine na wananchi yale yote ambayo wananchi wana changamoto nayo"

"Tumekubaliana na Diwani, ilikuwa tufanye zoezi la kutatua changamoto hizi mwakani 2025 lakini tumesema hapana, tufanye sasa. Wanasema mchuzi wa Mbwa unaliwa na motomoto" - Mpembenwe
 
Back
Top Bottom