Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,524
- 1,173
"Jambo hili watu wengi wamelizungumzia huko nje, wapo waliolipotosha na wapo waliokwenda mbali zaidi na kuzungumza yale ambayo ni hatari kwa Umoja wa nchi yetu na mshikamano wa Taifa letu. Nataka niwakumbushe wakati nchi yetu ilipopita kipindi kigumu cha COVID-19 wakati Dunia yote ilijifungia ndani haikuzalisha, Watanzania tulikuwa tunatembea mtaani na tulikuwa tunafanya shughuli zetu na Makamu wa Rais wa nchi hii alikuwa ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye alikuwa Mshauri mkuu wa Rais aliyekuwepo, tulivuka salama na hatukumtilia mashaka kuwa ni Mtanzania au si Mtanzania" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini
"Jambo hili hatupaswi kuliendekeza yanapokuja mambo ya msingi ya hoja tutofautiane kwa hoja na si kwa kubaguana. Miaka Miwili iliyopita shughuli za kisiasa hazikuwa zinaruhusiwa kufanyika; hapakuwa na Mkutano wa Chama cha siasa wala Press Conference za kwenye vyombo vya Habari. Ni Rais huyu huyu alikuja kufungua minyororo" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini
"Kwanini wakati ule hamkuhoji kuwa huyu ni Mzanzibar amekuja kufungulia vyombo vya Habari? Miaka Miwili iliyopita kulikuwa na magazeti zaidi ya 4 yamefungiwa, Online TV, Online Media karibu vyombo 30 - 40 vimefungiwa. Ni Rais huyu huyu aliyepo alifungua vyombo vyote vilivyokuwa vimefungiwa. Mpaka sasa hakuna kesi Mahakamani ya Chombo chochote cha Habari wala mwandishi wa Habari" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini.
====
Pia soma: