Mbunge kahoji mbele Waziri Nchemba kwanini hapigiwi saluti na polisi?

Ni swali zuri, kama wabunge wengine wanapigiwa saluti, kwanini yeye asipigiwe au kwa kuwa ni wa upinzani na alipambana sana na polisi hadi kufanikiwa kutangazwa mbunge? Kwa kuwa waziri Nchemba ndiye anahusika na mapolisi ilikuwa sahihi kuuliza hilo swali mbele ya mapolisi wenyewe! Kama wabunge wanapigiwa saluti yeye kutopigiwa inampunguzia kwa namna fulani "nguvu" ya kushughulikia hata hiyo migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo pia kwa namna fulani inachochewa na hao hao polisi wenyewe!
Mbunge anapaswa kupigiwa salute akiwa ndani ya jimbo lake au ndani ya eneo la bunge na si vinginevyo bt ni upuuzi kulilia salute wakati kuna watu wanavyeo vya kupigiwa salute hawana mpango nayo vpo vya maana zaid ya salute
 
Akili hana huyu yaani hilo ndiyo kaona jambo la maana sana kwake wabunge wengine ziro kabisa
 
Mbunge anastahili salute hata akiwa nje ya jimbo lake. Issue hapo ni ubaguzi wa kichama na kama sio sahihi kwake kupigiwa salute basi bunge likae tena kuondoa kipengere hicho cha salute
 
Wasio na akili watafikiri mbunge anataka kupigiwa saluti wakati anafikisha ujumbe kuwa wabunge wa upinzani hawapewi heshima inayostahili kwa hiyo hata wakienda kueleza matatizo ya wananchi hayapewi uzito haiitaji phd kujua hili.
 
natoka hapa bwana! Unashangaa nini? Au huwa mnapitisha vitu bungeni bila kujua ni kitu gani mmepitisha?Tujuavyo sisi ni kwamba bunge lilipitisha sheria kwamba mbunge asalimiwe na askari kwa kupigiwa Salute. Na tunajua fika kwamba bungeni walio wengi ndio huamua. Hivyo wabunge wako wa CCM waliamua hilo jambo. Mbona hukulalamika walipopitisha? Au mlitaka wabunge wa CCM ndio wapigiwe salute? Kila siku tunawaambia wabunge wenu wanapitisha mambo bungeni kwa ushabiki wa kichama. Ona sasa na hii sheria ya mitandao inavyoumiza watu na ninyi mpo kimya.
 
Stupid chadema people! Watu wanauwana Wakulima na Wafugaji yeye analilia saluti!!!

OTH_6079.jpg
Hapa LOWASA nae kazingua, anapigaje saluti akiwa kavaa kiraia?

Salute kwa huku bongo inasheria zake
 
SIJUI NI MBUNGE WA CHAMA GANI HOVYO NAMNA HII? ATAKUWA ANAAKISI MAWAZO YA CHAMA CHAKE BILASHAKA, NA HICHO CHAMA NDIO KINA VIONGOZI WENYE MITAZAMO KAMA YAKE. AJABU WAZIRI YUPO KWENYE KUSULUHISHA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YEYE ANADAI SALUTI. SALUTI NDIO ITAONDOA KERO ZA WANANCHI WA JIMBO LAKE. NI TANZANIA TU WANASIASA KAMA HAWA HUCHAGULIWA.
 
Back
Top Bottom