Mbunge Jumanne Kishimba: Kwanini wananchi walipe pesa ya kumuona daktari wakati wananchi walijenga kituo cha afya wenyewe?

Watanzania wengi tumekuwa na mtazamo wa kutegemea kila kitu kutoka serikalini bila kuzingatia umuhimu wa kujipanga kwa mambo muhimu kama afya. Ujinga huu ambao tumerithishwa na CCM yetu inatufanya tusipange bajeti ya afya zetu, wakati tunaweza kuchangia kwa njia mbalimbali kama vile bima ya afya ambayo inapatikana na kusaidia kwa gharama za matibabu.

Hospitali na inatumia rasilimali nyingi majengo, vifaa, dawa, mishahara ya madaktari na wauguzi na serikali pekee haiwezi kubeba mzigo huu wote, hasa kwa nchi yenye uchumi mdogo kama yetu. Serikali inajitahidi kutoa ruzuku kwa kiasi kinachowezekana, lakini idadi ya watu ni kubwa na inazidi kuongezeka.

Viongozi kama Mheshimiwa Kishimba wanapotumia lugha kama hii, wanajua ukweli lakini mara nyingi wanaangalia zaidi umaarufu wa kisiasa kuliko kuwaambia wananchi ukweli na kuwahamasisha kuchukua hatua za kujitegemea. Wananchi wanapaswa kuwa na bima za afya, kupanga bajeti zao, na kuwa tayari kuchangia kidogo katika gharama za matibabu ili kuboresha hali ya huduma zinazopatikana.

Suluhisho ni kwamba wananchi wanapaswa kuanza kuelewa umuhimu wa kujitegemea kwenye huduma muhimu kama afya, badala ya kutegemea serikali kwa asilimia mia moja. Serikali inaweza kusaidia, lakini sisi sote kama jamii tunapaswa kubadilika kifikra na kujua umuhimu wa kuchangia kwenye afya zetu wenyewe kwa kuwekeza kwenye bima na kuunga mkono gharama za tiba pale inapowezekana.
Umuhimu wa kujipanga upo na tunajioanga ila haiwezekani Kila kitu kiwe Cha kulipia,Kodi zetu zinafanya nini Sasa?
 
Je kama docta ana kituo chake binafsi cha afya na wakati huohuo ameajiliwa serikalini, hawez kutumia leseni yake hapo kituon kwake?
Mojawapo ya vigezo vya kuanzisha kituo binafsi cha afya ni kuwa na cheti cha usajili cha daktari (certificate of registration) ambacho hulipiwa na hutolewa mara moja tu. Leseni inahuishwa na kulipiwa kila mwaka.
 
Hiyo hela yenyewe (consultation fee) haiendi kwa daktari, ni mojawapo ya vyanzo vya mapato kwenye vituo vya afya (user fee) ambazo hukusanywa na mwishowe huingizwa kwenye account ya mapato ya kituo husika ambayo msimamizi wake ni serikali.

Hao hao madaktari wanaodhaniwa kwamba ndiyo wanaochukua hizo hela (consultation fee) hutakiwa kulipia Tsh. 100,000/= kila mwaka kwa ajili ya leseni wakati hakuna biashara anayofanya daktari kupitia hiyo leseni. Na hiyo Tsh. 100,000/= inaenda huko huko serikalini.
Yaani Kila mwezi Daktar anatakiwa ailipe serikali 10000 wizi mtupu
 
Naungana na Kishimba, Bora kuchangia gharama za dawa, vifaa tiba kuliko hii wanaita consultation fee, huu ni wizi sawa na Kulipishwa unapoingia stendi kukata Tiketi.

Hongera Kishimba Kwa hoja murua, unawashinda Hadi wanaojiita Wapinzani hawana hata kitu wanachoweza kusimama nacho Kwa Wananchi.

View: https://x.com/HabariLeo/status/1854495036177555573?t=R8WnnCYXCbHo5ML1KQ-_Yw&s=19

===========

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba amehoji suala la malipo ya kumuona daktari licha ya vituo vya afya kujengwa na wananchi

Kishimba alisema kwanini wananchi wamekuwa wakitozwa fedha ili kumuona daktari ilihali analipwa na serikali na wananchi walijenga kituo cha afya wenyewe


anafaa kuwa waziri mkuu yuko vizuri kuliko majaliwa
 
Back
Top Bottom