Mbunge Elibariki Kingu Ameishauri Serikali Kuiongezea Mkataba wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya SONGAS

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,503
1,171

MBUNGE ELIBARIKI KINGU AMEISHAURI SERIKALI KUONGEZA MKATABA WA SONGAS

"Na kule wanakopita watu wa CHADEMA wanapiga propaganda kwamba Rais Samia Suluhu Hassan anaweka mabango, nataka nikuambie ukiona mtu anapiga kelele jua umembana vizuri, Mama amewashika kwelikweli kupitia Wizara yako January (Wizara ya Nishati)" - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

"Nataka niwaombe wabunge wote tuendelee kumuunga mkono Mhe. January Makamba na Mama Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Nishati, tuendelee kuwashika mkono. Kazi wanayoifanya ni kubwa. Sisi kwenye Ilani tuliwatuma mtuwashie Umeme, Umeme unawaka unataka nisikusifie? - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

Wabunge mbalimbali wakati wakijadili Bajeti ya Wizara ya Nishati leo Jumatano Mei 31, 2023 bungeni jijini Dodoma wameitaka Serikali kuongeza mkataba wa kampuni ya kuzalisha umeme ya SONGAS. Mmoja wa wabunge ni Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

"SONGAS inapaswa kuongezewa mkataba kwa sababu inafanya kazi nzuri ya kuzalisha Umeme wa uhakika na kulipunguzia mzigo Shirika la Umeme nchini (TANESCO). SONGAS ni mfano bora wa matokeo ya ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)" - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi.

WhatsApp Image 2023-05-31 at 17.13.29.jpeg
 
Serikali ina hisa ktk taasisi na makampuni mbalimbali na imekuwa ikipata gawio..mfano toka CRDB,NMB..

Kwa miaka 20 iliopita ni kiasi gani Serikali imepokea gawio toka SONGAS?

Kwa umiriki wa 75% au hizo 40% zilizobaki baada ya watuhumiwa wa majambazi kujimegea zingine Msajiri wa hazina ana nguvu gani ya kufuatilia maslahi ya Nchi?

Kwa sasa SONGAS inaidai Tanesco kiasi gani? Na Serikali inaidai kiasi gani Songas?

Kuna Utatu mtakatifu kati ya SONGAS,Pan African Energy na Globaleq..Nani ni nani na kwa maslahi ya nani?

Ikiwa ni kweli JMT ilikopa WB 75% ya Mtaji wa kianzisha Songas na imelipa mkopo..Kwa nini imiriki 40%? Ni nani wamiriki wa 35%?DAHHH..

Hawa waliojichotea 35% za nchi Mapato yao kwa ujumla mwanzo mpaka mwisho wa mkataba ni kiasi gani?

World Bank wanabariki hili? Kwa faida ya nani?US analijua hili?SFO Wanalijua hili?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom