Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,695
- 1,241
Mbunge Deus Sangu: Bodi ya Utalii Tanzania Inakabiliwa na Sheria Iliyopitwa na Wakati na Uwezo Mdogo wa Kifedha
"Mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme ya Msongo wa Kilovoti 400. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha kandarasi tatu ambazo ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400, yenye urefu wa kilomita 280 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Ujenzi wa vituo viwili vya kupoza umeme msongo wa kilovoti 220/400 cha Nyakanazi na 400/132/33 cha Kigoma vitakavyohusisha ufungwaji wa mashine umba mbili zenye uwezo wa MVA 120 kwa kila moja; na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 katika vijiji 18" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Miradi ya maendeleo katika Hifadhi za Taifa za Kisiwa cha Rubondo na Burigi-Chato Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha miradi miwili ya maendeleo inayolenga kuboresha miundombinu ya malazi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Ujenzi wa Hotel ya Nyota Tano Jijini Mwanza Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa Hoteli ya Nyota Tano mkoani Mwanza (Mwanza Tourism) unaotekelezwa na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF). Utekelezaji wake ulianza mwaka 2010 kwa matarajio ya kukamilika Oktoba, 2016" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Kwa gharama ya shilingi bilioni 89.9. Hata hivyo, mradi huu haukukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya kutokupatikana kwa mwendesha hoteli (hotel operator), hali iliyosababisha mchakato huo kurudiwa mara mbili katika nyakati tofauti (mwaka 2017 na 2018)" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Bodi ya Utalii Tanzania inakabiliwa na changamoto ya sheria iliyoianzisha kuwa imepitwa na wakati na Bodi inauwezo mdogo wa kifedha unaochangiwa na kuondolewa kwa ushuru wa utalii na taasisi nyingine kuendelea kujitangaza" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Baadhi ya Taasisi za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuathiriwa na Madeni Changamoto ya Upatikanaji wa Rejesho la Uwekezaji Utendaji wa Mamlaka za Maji ambapo Mamlaka za Maji zinajumuishwa kwenye malipo ya gharama za umeme kibiashara jambo linalosababisha kuongezeka kwa gharama za uendeshaji." - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Imebainika kuwepo kwa baadhi ya taasisi na mashirika yanayotumia Mtaji wa Umma ambayo yanajiendesha bila kuzingatia vigezo vya utendaji vilivyowekwa na Msajili wa Hazina" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Baadhi ya Taasisi za Uwekezaji wa Umma kufanya Shughuli za Uwekezaji bila kuwa na Mpango wa Uwekezaji (Investment Plan) zipo baadhi ya taasisi za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma zinazojiendesha bila kuwa na Mpango wa uwekezaji, na kwakuwa, taasisi zinazojiendesha bila Mpango wa Uwekezaji zinakosa mwongozo na mikakati inayolenga tija na hivyo kutokuwa na ufanisi katika uwekezaji" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Kwakuwa, uanzishwaji wa Kampuni tanzu unaolenga kuzisaidia Kampuni mama kujiendesha kibiashara umebainika kushindwa kufanikisha azma hiyo kutokana na kukosekana kwa usimamizi wa utaratibu wake" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"Benki ya Maendeleo (TIB) iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kifedha kwenye miradi ya maendeleo, inakabiliwa na ukata wa mtaji na kwamba Ina mtaji mdogo wa kiasi cha shilingi bilioni 24 Haikidhi masharti ya Benki Kuu ya Tanzania ya kuwa na mtaji usiopungua Bilioni 200 Imeshindwa kulipa amana za jumla ya shilingi bilioni 206.854 zilizowekwa na watu binafsi na baadhi ya taasisi za Serikali Imepata hasara ya kiasi cha shilingi bilioni 195.91 kati ya mwaka 2021 na 2022 kutokana na tengo la mkopo chechefu" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC
"NARCO inakabiliwa na changamoto za kiuendeshaji ikiwemo tozo ndogo kwa watumiaji wa vitalu vyake, kutojulikana kwa idadi na ukubwa halisi wa Ranchi zinazo milikiwa na NARCO na ufinyu wa fedha; NA KWA KUWA, changamoto hizo zinachangia ufanisi na tija ndogo ya NARCO" - Mhe. Deus Sangu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC