Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,491
- 7,028
Mbunge wa Bunda Vijijini, Boniphace Mwita Getere akizungumza Bungeni Aprili 10 amesema;
"Wengi mnakaa humu ndani Bungeni ila sijawahi kuona unakaa na mwanadamu mstaarabu kama Waziri Mkuu tuliyenaye sasa hivi, ni mstaarabu mno, ni mchapakazi na mstaarabu, kila mtu anamsikiliza."
"Sasa mimi nikasikia maneno maneno unajua bwana, eenh! Waziri Mkuu sasa amemaliza vipindi viwili akienda huku sasa, akiwa mbunge anafanyaje kama sio Waziri Mkuu? Kwani kuna hoja gani, mbona tumewaona watu wengi tu, Mzee Malechela, tumeona Marehemu Lowassa wanakuwa Mawaziri wakuu na wakaa humu bungeni? Tunamuomba Waziri Mkuu Mkuu arudi Bungeni, arudi, habari ya Vyeo Mungu atajua, yeye arudi bungeni, ni mstaarabu mno.Anafanya kazi usiku na mchana kila Jimbo la Mbunge ameshaenda."
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Tunamuombea huko anakotokea arudi bungeni tukaye naye asaidie nchi. Lakini Mheshimiwa Mwenyekiti Waziri Mkuu amepita vipindi vigumu mno, alikuwa amefanya kazi na marehemu Magufuli, amekuja kwa mama amefanya naye kazi amemuonesha kila mahali, nchi leo ipo salama."

Ili kuongeza ajira ni vizuri apumzike sababu anatunzwa maisha na anapata mafao makubwa asilimia 80 ya waziri mkuu aliyeko madarakani
Atoe hiyo nafasi ya ajira kwa watu wengine kama alivyofanya Makamu wa Raisi Philip Mpango
Pia ni vizuri Raisi mpya anapoingia madarakani awe na timu yake mpya ya kuanzia wabunge mawaziri nk
Mwacheni Mama aunde timu mpya.
Na mbunge aliyetoa hilo wazo naye asirudi bungeni ajira yake naye apishe wengine