Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,664
- 1,228
MBUNGE DANIEL BARAN SILLO AKABIDHI MASHINE ZA KUCHAPISHA MITIHANI KWENYE SHULE ZA SEKONDARI
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini (Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti) Mhe. Daniel Sillo ametimiza ahadi yake ya kukabidhi mashine za kuchapisha katika Shule za Sekondari Maganjwa na Arisaayo ili kusaidia katika kuchapa mitihani.
Akizungumza wakati akikabidhi mashine Mbili katika shule hizo, amesema kuwa hadi sasa ameshatoa mashine zaidi ya 16 kwenye Shule za Sekondari na kwamba hadi mwaka 2025 atakuwa amekamilisha kugawa na kwenye shule za Msingi.
Mhe. Sillo amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao na atakuwa mstari wa mbele kuwasaidia katika kutatua changamoto zinazo wakabili kwa kadri atakavyoweza.
Katika hatua nyingine, amewapongeza Walimu kwa kazi kubwa wanayofanya ya kufundisha na kuongeza ufaulu katika Wilaya ya Babati.
Nao Madiwani wa Kata ya Arri na Dabil wamemshukuru Mbunge huku wakisema kuwa kitendo cha kutoa msaada huo kinaonesha ni jinsi gani anaunga mkono Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassani ya kujenga miundombinu
Mhe. Daniel Sillo katika ziara aliyoanza tarehe 04 Julai, 2023 katika Kata ya Nkaiti alishiriki katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Kata na kuwapatia vijana wa Kata hiyo seti nne za Jezi na mipira.
Aidha, Mhe. Sillo aliwapatia vikundi vya kina mama vyerehani vinne huku akiungana na wajumbe wa kamati ya fedha, mipango na Uongozi katika ukaguzi wa miradi katika Kata za Nkaiti, Mwada na Magugu.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-07-06 at 09.09.55(2).jpeg76.6 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-06 at 09.09.55(1).jpeg63.5 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-06 at 09.09.55.jpeg78.6 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-06 at 09.09.54(1).jpeg53.7 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-06 at 09.09.54.jpeg39.2 KB · Views: 2