Mbunge Aysharose Mattembe Aibana Serikali Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,909
1,340

MBUNGE AYSHAROSE MATTEMBE AIBANA SERIKALI UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA

Serikali imeeleza kuwa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida inatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2027, ikiwa ni baada ya utekelezwaji kwa awamu tatu za mradi huo muhimu kwa huduma za afya mkoani humo.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Aysharose Ndogholi Mattembe, aliyetaka kujua ni lini Serikali itakamilisha ujenzi huo

"Katika awamu ya kwanza, Serikali ilitoa Shilingi Bilioni 6, na awamu ya pili zilitolewa Shilingi Bilioni 3.3," amesema Dkt. Mollel.

Aidha Dkt. Mollel ameongeza kuwa, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga Shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya awamu ya tatu ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Dkt. Mollel amebainisha kwamba Serikali inaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu na makazi yao.

Hadi sasa Serikali imeshatoa jumla ya Shilingi Bilioni 9.3 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
 

Attachments

  • sddefaultlopiuyt.jpg
    sddefaultlopiuyt.jpg
    50.1 KB · Views: 1

Similar Discussions

Back
Top Bottom