JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,696
- 6,491
Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumza na viongozi wa vyama vya siasa leo Januari 3, 2022, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema:
Taifa letu limekuwa na mfumo wa ukandamizaji wa demokrasia kwa muda mrefu, kuanzia ngazi ya taifa hadi vitongozi, lakini tutaangalia kwa macho angavu jambo hio katika ngazi za nchini.
"Rais ameruhusu mikutano ya siasa iendelee, hilo ni jambo muhimu na jema kwa kuwa ni jambo la kikatiba.
"Sisi kama chama kikuu cha upinzani nchini tumelipokea jambo hilo positive, ni hatua muhimu.
"Amezungumza pia kuhusu kukwamua mchakato wa Katiba.
"Suala la Kikatiba siyo la kusubiri, ni suala la sasa na kizuri zaidi ni kuwa Rais amekuja na tamko la kuwa mchakato utaendelea na kutoufanya kuwa wa chama kimoja.
"Jambo zuri pia amezungumzia kuhusu ushirikishwaji katika mabadiliko ya Sheria, zipo nyingi sana zinatakiwa kufanyiwa maboresho.
“Huko nyuma Serikali ilikuwa inafanya mabadiliko ya Sheria, inaleta Bungeni katika Certificate of urgency, zinapitishwa bila kuridhia maoni au mawazo ya wapinzani au makundi mengine ya kijamii.
Kuna Sheria ambazo zinagusa umma kwa ukaribu kama Sheria kama za Vyombo vya Habari, za Uchaguzi, Takwimu na nyingine mbalimbali zinaoongoza taasisi zisizo za Kiserikali.
“Ushirikishwani ni mzuri, kwani kama mnavyojua Bunge letu leo ni la Chama kimoja, hivyo unavyopeleka Sheria ya Serikali ya chama hichohicho ni Sheria ya CCM na siyo ya Kitaifa.
"Kwa ujumla tumepokea tamko lake positive na kwa tahadhari kubwa, muhimu pia tutashirikiana na kutoa presha ili kupatikana kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba ya Taifa ambalo italiunganisha Taifa.
“Sisi kama chama tutaenda kujadiliana katika vikao vyetu vya chama kwa kile ambacho kimejili Ikulu siku ya leo.”