Kisu Cha Ngariba
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 22,135
- 48,826
Kwenye hili la Katiba tupo pamoja. Lakini swali la msingi. Kama Makonda naye ana kinga ya kutoshitakiwa kwa kumdhalilisha mtu hadharani. Kinga ya Rais ya kutoshitakiwa inakwenda mpaka kwa wateule wake? Na kwa hoja yako ni kwamba mahakama itaona hata kama mtu anavunja sheria na haki ya mtu mwingine kwa kuwa mtu huyo anatekeleza majukumu ya "Serikali" basi mtu huyo ashitakiki mahakamani?
Kutekeleza majukumu kwa Makonda je ni tafsiri kwamba Rais Magufuli ndiye alimtuma atangaze majina yale hadharani kwa njia ile aliyoitumia? Swali langu hapa jee huko kutekeleza majukumu kwa niaba ya rais hata utekelezaji huo ukiwa wa hovyo kiasi gani watekelezaji hawatashitakiwa wao moja kwa moja kwa kuwa tu wanamwakilisha Rais? Kwa mfano mkuu wa mkoa akimpiga risasi mtu anayemhisi kwamba anajihusisha na madawa ya kulevya, Mkuu wa Mkoa hatashitakiwa bali serikali ndiyo itashitakiwa?
Nilitegemea maswali yako yatajibiwa na mleta uzi,mpaka sasa ajajibu swali lolote. Inaonyesha ametumwa kuleta uzi bila ya kuwa na details yoyote kuhusu alichokileta.