Mbona hakuna mabadiliko ya maisha

Yaani sijui watz wamelishwa unga gani. Ili uyaone mabadiliko ya sera za uchumi bora yaone kwanza mfukoni mwako na kisha kwenye familia yako. Huku kushangilia wanaotumbuliwa bila kujua kuwa wamepewa likizo ya kwenda kutumia na kutumbua walichochota ni uzuzu! Hebu badilikeni kwa kuona mnavyozugwa na wanasiasa.

Sijasikia hata mmoja wa waliotumbuliwa akiambiwa arudishe alichoiba. Wapo wanajienjoy na akiba walizojiwekea.
 
Usijaribu kumkosoa ...watu watakushambulia...
Unatakiwa chochote kile kwanza useme 'pamoja na kazi nzuri ya Rais'

watu washalewa 'pombe' hawasikii kitu
Mkuu huwa nakuelewa mapema sana. Na jana tu nimebishana na shemeji yako mpk nikaamua kwenda container kunywa angalau soda! Nae anajua kushabikia, sijapata kuona!
 
aa548358919d3c651f97d695af7d8868.jpg
 
Mh.Magufuri yupo vizuri bwana Nchi ilioza hii watu wanapitisha meli nzima hawalipi kodi harafu mtaani tunauziwa mafuta na kodi yake..bado tuendelee kumpinga...kinachotakiwa kama wataalamu toeni ushauri mzuri na si kuwa opposite muda wote hata katika jema.
 
Nimekuwa nikifuatilia mienendo ya watanzania kumshangilia Mh kila analolifanya. Strange maisha ndiyo yanazidi kuwa ya shida. Jana nimepita hospitali, rushwa ndio imepamba moto.

Barabarani usiseme. Mnashangilia nini? Ni ile ya tukose wote, ni wivu wa sisi masikini;

Nimekuja kugundua na wala siyo kuwa masikini wanashangilia (masikini wanaoshangilia) kuwa tunaelekea kuzuri. Tatizo la sisi masikini tukiona tajiri kaporomoka, tunapata usingizi mzuri kama vile tumepata nafuu ya maisha.

Wanashangilia Kabwe kaangushwa, of what direct benefit to you from today!
Wewe ni mtu wa ajabu sana na tatizo lako ni mbinafsi na huoni mbali,anachokifanya Magu ni kwa mustakabali wa taifa kwa cku zijazo!unaweza usifaidike wewe wakaja kufaidika watoto wako!
 
kubadilisha maisha ya waafrika katika nchi masikin kama Tanzania si suala la kukurupuka, linahitaji viongozi imara na ambao hawana woga ktk kutetea masilahi ya Taifa, tushukuru mungu tumepata Rais anaeonekana mwenye nia kama hiyo. ufisadi ktkt nchi za kiafrika ndo jambo kubwa linarudisha nyuma maendeleo ya taifa mheshimiwa hajakosea kuanza na suala hili, cha muhimu ni kumuunga mkono Mr.President. Maendeleo sio jambo la kulala usiku ukiamka asubuhi unakuta maendeleo, bali nchi kama yetu hii ambayo kuna mnyoror mrefu ambao umesukwa tangu kipindi hicho na wajanjawajanja ambao wako kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe na matumbo yao lazima ufunguliwe ili pato la Taifa hata mtu wa hali ya chini aweze kunufaika nalo na aweze kuliona, hiyo ndo kazi ya magufuli aliyoanza nayo. Cha muhimu ni tuwe wavumilivu huku tukimuombea Mr.President akamilishe kazi yake baadae tutakuja kuona matunda hata kwa yule mzee aliyejichokea kule kijijini.
Wakati haya yanafanyika sisi wananchi tunaendelea kutaabika hivi hivi au vipi?
 
Back
Top Bottom