Mbio za mwenge: Makamu wa rais Samia, atazindua mbio za Mwenge

Shereha za uhuru zilifanyika sio kwa magwaride na maandamano bali kwa kufanya usafi kila mmoja eneo lake analoishi au eneo lake la kazi.Sherehe hizi zilisheherekewa na watu wengi kuliko nilivyowahi kushuhudia awali

Labda ujaribu kutofautisha kati ya sherehe na maadhimisho.

Mwaka jana tuliadhimisha siku ya uhuru ila haoakuwa na sherehe ya maadhimisho ya siku hiyo.
Badala ya kufanya sherehe watu waliadhimisha kwa kifanya usafi kwenye mazingira yao.
 
Shereha za uhuru zilifanyika sio kwa magwaride na maandamano bali kwa kufanya usafi kila mmoja eneo lake analoishi au eneo lake la kazi.Sherehe hizi zilisheherekewa na watu wengi kuliko nilivyowahi kushuhudia awali
Kwa mantiki hiyo kuna shida gani kwa kubadili namna ya kusheherekea huo mwenge? Badala ya kuukimbiza na kuadhiminisha kwa matumizi makubwa, kwanini Rais asifanya mabadiliko kama ilivyokuwa kwenye sherehe ya Uhuru? Hiyo sense of nationalism itapungua vipi kama tuliweza kubadili namna tulivyozoea kusheherekea Uhuru kwa magwaride, makomando kuvunja matofali na halaiki ya watoto, na kuifanya iwe siku ya usafi?
 
Yaani Mimi bado sana nipo gizani,mpaka Leo sijuagi mwenge unamulikaje majangili,nifafanulieni jamani nipo gizani

Maneno tu hayo, hata kwenye khanga yapo, ungemulika majangili Twiga wasingepandishwa ndege, Tembo, Faru, Mijusi, Ngedere nk nk wasingeporwa kwa kasi hiyo tuliyoishuhudia miaka ya karibuni. Na mimi naunga mkono kuondokana na mbio hizi zisizo na tija.
 
Kifupi Mwenge ni nembo ya taifa kama zilivyo nembo nyingine. Hakuna haja ya kutumia mabilioni ya fedha kukimbiza nembo ya taifa.

Ni ukweli usiopingika kuwa kamwe watawala hawawezi kuleta mabadiliko bila kulazimishwa na wale wanaotawaliwa.
Watawala siku zote wanapenda kutawala kwa njia rahisi na kuwafanya walioko chini waishi kwa hofu kubwa na woga.

CCM tangu uhuru ndio wanaotawala, na tatizo lao ni woga wa kile kisichojulikana. CCM wanaimba na kujifanya kuwa wanaamini katika umoja na mshikamano wa watanzania na walienda mbali zaidi kwa kuamini kuwa sisi sote ni ndugu. Ukweli ni kwamba CCM ya leo baada ya TANU na ASP ndani ya mioyo yao wanaamini katika uadui na kutokuaminiana. Wanaamini kuwa kila mtu ni adui wa mwenzake. Ndio maana wanahofu ya mambo ya kufikirika zaidi. Hawaaminiani na hawaamini kwa mtu asiye mwenzao katika historia ya kukabidhiana madaraka. Ndio maana CCM na watawala siku zote wanafalisafa zisizo na tija kwa taifa kama hii ya kuamini amani inayoweza kuletwa na mwenge bila haki.
Mwenge hauwezi kuwa na maana kama siku kwa siku watanzania wanazidi kujengewa chuki na vijana wa chama cha mapinduzi ili tu wajipatie madaraka.

Kwanza watanzania wengi wa leo hawaamini katika ushirikina (Hasa wale wasiofungamana na CCM).
Pili.Watanzania wa leo wengi wanamini katika dini za kikristo na kiislam kwa kuwa wengi wanasoma na kuzielewa dini bila kusimuliwa na kudanganywa.

Tatu. Mfumo wa kijamaa na kikomunisti uliokuwa unapingana na uwepo wa Mungu muumbaji umeshapitwa na wakatika katika fikra zile za kuwakweza na kudumisha fikra za watawala na viongozi na hata kuwatukuza kuliko Mungu.

Haya yanatufanya tulio wengi tuukatae huu utaratibu mbaya wa kukimbiza mwenge na kufanya mikesha na ibada za zinaa na ulevi kupitia fedha za umma.

Ni dhambi kuu na aibu kutumia mabilioni ya fedha kwa kukesha na kuimba kwa ulevi na uzinzi kwa kutumia kodi za wananchi.
Tunajenga taifa lisilo na watu wenye nidhamu. Kama kiongozi wa mbio za mwenge anazunguka nchi nzima akiwa na wanawake au wanaume na huko anakokwenda anafanya uzinzi kila kata na vijiji. Hapo nidhamu inatoka wapi?
Nchi hii imekwama hapa tuliposimama kutokana na watawala kukosa nidhamu kuanzia kwenye maadili.

Mh.Magufuli achana na walafi wanaoutumia mwenge kujinufaisha.

Kama wanasababu za msingi basi kila wilaya ipewe Mwenge wake na ukimbizwe siku mbili tu bila posho. Pesa za mafuta tu .Mkuu wa Wilaya na mkurugenzi wasimamie na kupeleka taarifa ya miradi kwa mkuu wa mkoa. Lakini hawa vijana wanaozungusha mwenge kwa mabil. ya sh. Nchi nzima huku wakihamasisha ngono na ulevi kwa vitendo wasipewe tena hilo dili lisilo na tija kwa taifa letu changa.

Au kila wilaya ipokee na kukimbiza mwenge kwa kusimamiwa na mkuu wa wilaya na mkurugenzi kwa tarehe maalumu akimaliza kwenye wilaya yake anamkabidhi mkuu wa wilaya ya jirani na kuendelea na wilaya ya mwisho ndipo mwenge unapozimwa. Hapa hakuna cha posho kwani kazi ya kuhamasisha maendeleo ni kazi ya mkurugenzi na mkuu wa wilaya hivyo atatumia magari na rasilimali za ofisi yake za kusimamia miradi ya maendeleo.
Hapa tutakua tumezungusha mwenge bila kupoteza fedha za watanzania kwa manufaa ya wapotoshaji wachache ndani ya nchi hii, wanaojifanya wanauchungu sana na nchi kumbe wanalenga posho na pesa za mwenge ziwanufaishe.
 
Kwa hiyo sherehe za Uhuru zilifanyika mwaka jana kama ilivyokuwa zilifanyika miaka ya nyuma?
Unajua maana ya neno 'kuondolewa'?. Yani Rais Magufuli alisema sherehe za uhuru hazitafanyika kwa mwa 2015 na sio kwamba sherehe hizo zimeondolewa kabisa kabisa...
 
Kama bado kuna umuhimu wa kuwepo up mwenge uwe unawashwa mkoa mmoja na kumalizika siku hiyo hiyo
 
Mwenge ni zindiko ambayo siri yake aliijua mwalimu tu na wachache aliowanong'oneza. Na siku mwenge ukifutwa ndio siku watanzania watakayojitambua, ndiyo siku wananchi watakayojua mabaya na mazuri wanayofanyiwa na viongozi wao. Katika hili sidhani kama kuna kiongozi wa nchi anayeweza kuufuta mwenge.
......kweli kabisa.
 
Unajua maana ya neno 'kuondolewa'?. Yani Rais Magufuli alisema sherehe za uhuru hazitafanyika kwa mwa 2015 na sio kwamba sherehe hizo zimeondolewa kabisa kabisa...
Sawa. Ndiyo afanye hivyo kwa mbio za Mwenge. Aseme sherehe za mbio za Mwenge hazitafanyika mwaka huu na miaka inayokuja.
 
Heshima kwenu Wana JF wote

Watu wengi walikuwa wanasifia sana juhudi za jitahada za raisi katika kubana matumizi na kufuta mpaka baadhi ya sherehe ambazo zilikuwa zinatumia gharama kubwa. Nimeshangaa sana kushangaa mwenge wa uhuru unazinduliwa 18 April 2016 mwaka huu gharama yake ni zaidi ya billioni 14 ni kwamba raisi ameshindwa kufuta huo mwenge unaotumia zaidi billioni 14. Kama raisi ameshindwa kuufuta mwenge hata hizo sherehe nyingine amezifuta kwa kukurupuka kufurahisha watu . Mimi sijawahi kuona faida za mwenge labda wale wanaofahamu faida za mwenge watujuze . Sasa kulikuwa na sababu gani za kufuta sherehe nyingine wakati mwenge ameshindwa?
 
Heshima kwenu Wana JF wote Watu wengi walikuwa wanasifia sana juhudi za jitahada za raisi katika kubana matumizi na kufuta mpaka baadhi ya sherehe ambazo zilikuwa zinatumia gharama kubwa. Nimeshangaa sana kushangaa mwenge wa uhuru unazinduliwa 18 April 2016 mwaka huu gharama yake ni zaidi ya billioni 14 ni kwamba raisi ameshindwa kufuta huo mwenge unaotumia zaidi billioni 14. Kama raisi ameshindwa kuufuta mwenge hata hizo sherehe nyingine amezifuta kwa kukurupuka kufurahisha watu . Mimi sijawahi kuona faida za mwenge labda wale wanaofahamu faida za mwenge watujuze . Sasa kulikuwa na sababu gani za kufuta sherehe nyingine wakati mwenge ameshindwa?
Mwenge ndio uchawi wa Mchonga unaotumiwa kutufanya watanzania tuwe maboya boya, hatuwezi kuhoji chochote.

Akiufuta, tukaamka ataweza kutawala hii nchi??
 
Heshima kwenu Wana JF wote Watu wengi walikuwa wanasifia sana juhudi za jitahada za raisi katika kubana matumizi na kufuta mpaka baadhi ya sherehe ambazo zilikuwa zinatumia gharama kubwa. Nimeshangaa sana kushangaa mwenge wa uhuru unazinduliwa 18 April 2016 mwaka huu gharama yake ni zaidi ya billioni 14 ni kwamba raisi ameshindwa kufuta huo mwenge unaotumia zaidi billioni 14. Kama raisi ameshindwa kuufuta mwenge hata hizo sherehe nyingine amezifuta kwa kukurupuka kufurahisha watu . Mimi sijawahi kuona faida za mwenge labda wale wanaofahamu faida za mwenge watujuze . Sasa kulikuwa na sababu gani za kufuta sherehe nyingine wakati mwenge ameshindwa?
Ukiona hajafuta basi ujue ameiona hakuna madhara!we jiongeze usishiriki
Jifunze kwa maalim seif aliona hakuna madhara hakushiriki!!!
 
hii mada inahitaji tafakari ya kina sana.

hivi jiulize wewe kuchoma mafuta ya shilingi elfu 20 mpaka 30 kila siku unatoka nyumbani kwako peke yako kwenye gari eti unakwenda kazini, mafuta haya unayochoma yanawatajirisha wachimba mafuta na kutuachia sisi umasikini, gari hilohilo kila mwaka unanunua spea kutoka nje maana yake unawatajirisha waasia wanaotengeza na kututia sisi umasikini kwa maana mpaka tukusanye korosho zetu kununua gari, mafuta na vipuri sijui kilo ngapi?

hivi wewe tatizo lako ni nini? si usafiri wa kwenda kazini? sasa kama wakiimarisha usafiri wa umma ukawa wa uhakika na wewe wakakuwekea mazingira magumu ya kutumia usafiri wa binafsi na ukalazimika kutumia wa umma ambako mnapanda watu 80 kwenye gari moja huoni tutatumia korosho kidogo kuwapatia usafiri hawa?

je tunatajirijika au ?

tukirudi kwenye mwenye yawezekana mwenge ukawa na faida sana hata kuliko mkutano wa kisiasa hasa pale mkutano wa kisiasa unapotumika kuwapotosha wananchi huku mkutano wa mwenge ukielimisha, ukihamasisha kuhusu mambo ya maendeleo.

sasa tufute mikutano ya kisiasa ili wananchi wasipotoshwe au tufute mbio za mwenge ili wananchi wasielimishwe.

je mbio za mwenge na wewe kwenda kazini kwenye gari lako ukiwa peke yako kipi kinatutia umasikini zaidi na kipi kishughulikiwe kwanza?

binafsi naona kupinga mbio za mwenge ni mihemuko ya kisiasa isiyo na mantiki nyuma yake.

mwenge ni kama panga ambalo ukilitumia vizuri linakuletea faida lakini ukilitumia vibaya kinakuwa kitu hatari.

wapo watakaosema michezo haina maana kwa kuangalia watu wazima wako viwanjani wanakimbizana kila siku jioni hawalipwi wala umri wao umepita kusema wanajenga vipaji lakini zipo faida zisizoonekana moja kwa moja.

tuache mihemuko ya kisiasa tuangalie kitu gani kina tija kwa jamii na hata kama kitu hakina tija je kinaweza kuwa na tija lakini tusitangulize kupinga au kusapoti kwa sababu wenzangu wanapinga.

Heshima kwenu Wana JF wote Watu wengi walikuwa wanasifia sana juhudi za jitahada za raisi katika kubana matumizi na kufuta mpaka baadhi ya sherehe ambazo zilikuwa zinatumia gharama kubwa. Nimeshangaa sana kushangaa mwenge wa uhuru unazinduliwa 18 April 2016 mwaka huu gharama yake ni zaidi ya billioni 14 ni kwamba raisi ameshindwa kufuta huo mwenge unaotumia zaidi billioni 14. Kama raisi ameshindwa kuufuta mwenge hata hizo sherehe nyingine amezifuta kwa kukurupuka kufurahisha watu . Mimi sijawahi kuona faida za mwenge labda wale wanaofahamu faida za mwenge watujuze . Sasa kulikuwa na sababu gani za kufuta sherehe nyingine wakati mwenge ameshindwa?
 
Mwenge hauna faida yoyote kwa nchi hii. Suala la kuhamasisha maendeleo sio lazima uhusishe uwashaji mwenge.

NI UFUJAJI WA PESA BURE TU
 
Mwenge hautakuwepo mwaka huu,kilichopo kwa sasa inaangaliwa pesa zitakazookolewa zipelekwe wapi.
 
Heshima kwenu Wana JF wote

Watu wengi walikuwa wanasifia sana juhudi za jitahada za raisi katika kubana matumizi na kufuta mpaka baadhi ya sherehe ambazo zilikuwa zinatumia gharama kubwa. Nimeshangaa sana kushangaa mwenge wa uhuru unazinduliwa 18 April 2016 mwaka huu gharama yake ni zaidi ya billioni 14 ni kwamba raisi ameshindwa kufuta huo mwenge unaotumia zaidi billioni 14. Kama raisi ameshindwa kuufuta mwenge hata hizo sherehe nyingine amezifuta kwa kukurupuka kufurahisha watu . Mimi sijawahi kuona faida za mwenge labda wale wanaofahamu faida za mwenge watujuze . Sasa kulikuwa na sababu gani za kufuta sherehe nyingine wakati mwenge ameshindwa?
huu mwenge mbali na gharama zinazotumika lakini pia unaongoza kwa kuharibu maadili,kusambaza ukimwi na watu kupoteza mali zao,ukienda asubuhi sehemu ambapo mwenge umekesha utakuta pakiti za condom,viroba na nguo za kike na pengine ukakuta na watu wamelala hapo bila kujitambua kwa kuelemewa na vinywaji
 
Heshima kwenu Wana JF wote

Watu wengi walikuwa wanasifia sana juhudi za jitahada za raisi katika kubana matumizi na kufuta mpaka baadhi ya sherehe ambazo zilikuwa zinatumia gharama kubwa. Nimeshangaa sana kushangaa mwenge wa uhuru unazinduliwa 18 April 2016 mwaka huu gharama yake ni zaidi ya billioni 14 ni kwamba raisi ameshindwa kufuta huo mwenge unaotumia zaidi billioni 14. Kama raisi ameshindwa kuufuta mwenge hata hizo sherehe nyingine amezifuta kwa kukurupuka kufurahisha watu . Mimi sijawahi kuona faida za mwenge labda wale wanaofahamu faida za mwenge watujuze . Sasa kulikuwa na sababu gani za kufuta sherehe nyingine wakati mwenge ameshindwa?

Kuna siku nilimsikia Mkapa akifoka sana kuhusu wanaopinga mbio za Mwenge!!

Siku Mwenge ukiwekwa chini ndio siku CCM itakufa papo hapo!!! Na rasilimali za nchi hii zitageuka neema badala ya laana!!!
 
Kuna siku nilimsikia Mkapa akifoka sana kuhusu wanaopinga mbio za Mwenge!!

Siku Mwenge ukiwekwa chini ndio siku CCM itakufa papo hapo!!! Na rasilimali za nchi hii zitageuka neema badala ya laana!!!
mwenge ndo uchawi wa CCM ndo mana JPM ameshindwa kuufuta anajua akiufuta ndo kifo cha CCM kimefika
 
Back
Top Bottom