Mazoezi ya kuruka kamba ndiyo mazoezi bora kuliko yote

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
8,809
15,544
Mazoezi bora yanatakiwa kuwa na sifa nyingi. Sifa moja kuu ni yachome nguvu za kutosha. Chakula tunachokula kinaenda kuupa nguvu mwili wetu. Kama tunakula zaidi ya mahitaji ya miili yetu, chakula hicho kinaenda kuhifadhiwa kama "Kitambi."

Basi mazoezi bora yanatakiwa kuchoma kitambi cha kutosha. Katika mazoezi yaliyozoeleka hakuna mazoezi yanayopuuzwa kama kuruka kamba na hakuna yaliyo bora kama kuruka kamba(Salama, rahisi kwa pesana kufanya, yanahusisha viungo vyote nk). Mtu aliyekimbia kwa nusu saa na aliyeruka kamba kwa nusu saa, aliyeruka kama anakuwa amechoma sehemu kubwa ya kitambi kuliko aliyekimbia.

Nusu saa ya kuruka kamba anakuwa amechoka Kcal 600. Wakati yule aliyekimbia jogging anakuwa amechoma Kcal kama 500. Siku hizi kuna kamba za kisasa ambazo zinakuambia hata kiasi cha "kitambi" ulichochoma. Turukeni kamba. tuanzishe kampeni ya RUKA TANZANIA.

1690317254173.png

Mazoezi ni dhana pana sana, zipo aina nyingi za mazoezi na kila zoezi lina lengo lake.

Hilo unalolisema linaitwa skipping na lina angukia kwenye kundi la aerobic exercises, hivyo lina faida na hasara zake.

Lakini huwezi kusema hilo zoezi ni bora, kwasababu kila zoezi lina lengo lake, leo hii mwakinyo afanye zoezi hilo kwa ajili ya shughuli zake itakuwa si sahihi, lazima atafute muscle power na sio kwa kuruka kamba.

Pia kuna mazoezi tiba kwa ajili ya wagonjwa, huwezi kumrukisha kamba mgonjwa aliye serious lazima akufie, hivyo huwezi Kusema hilo zoezi ni bora kuliko yote.

Kwahiyo zoezi bora ni lile lenye lengo maalumu na lenye kukidhi mahitaji kutokana na uhitaji.
 
Umefafanua vyema sana. Hata kwenye riadha sio kwamba wote huingia barabarani na kuanza kukimbia. Wa mbio fupi wana jinsia yao ya kufanya mazoezi na wale wa mbio ndefu wana namna namna yao. Huwa wanakutana wote gym tu na baadhi ya sessions. Kwa mfano wale wa mbio ndefu na fupi wote hukutana uwanjani kwa mazoezi yanaitwa speedwork ambapo nia ni kupata spidi kali kwenye umaliziaji wa mbio.
 
Mazoezi ni dhana pana sana, zipo aina nyingi za mazoezi na kila zoezi lina lengo lake.

Hilo unalolisema linaitwa skipping na lina angukia kwenye kundi la aerobic exercises, hivyo lina faida na hasara zake.

Lakini huwezi kusema hilo zoezi ni bora, kwasababu kila zoezi lina lengo lake, leo hii mwakinyo afanye zoezi hilo kwa ajili ya shughuli zake itakuwa si sahihi, lazima atafute muscle power na sio kwa kuruka kamba.

Pia kuna mazoezi tiba kwa ajili ya wagonjwa, huwezi kumrukisha kamba mgonjwa aliye serious lazima akufie, hivyo huwezi Kusema hilo zoezi ni bora kuliko yote.

Kwahiyo zoezi bora ni lile lenye lengo maalumu na lenye kukidhi mahitaji kutokana na uhitaji.
Mwakinyo ile ni kazi. Na mgonjwa anatakiwa apate mazoezi-tiba na si mazoezi kama mazoezi. Kwa mtu anayetaka kuchoma kitambi kwa kutumia mazoezi yaliyozoeleka, kuruka kamba ni mazoezi bora aidi.
 
Mazoezi yote yanachoma calories, ila kama alitaka kuzungumzia hivyo angeandika "" kuruka kamba ni zoezi bora kuliko mazoezi yote ya cardio exercises "" na angeeleza katika muktadha huo.

Hivyo alivyo andika ni tofauti na wewe unacho eleza.
Mtoa mada anatuelezea sisi wenye vitambi aina rahisi ya tizi tena yenye gharama nafuu

Km kuna aina nyingine yenye gharama nafuu tujuze

Tunaposema gharama tunamaanisha muda na vifaa vya kutekeleza tizi husika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom