Mazingaombwe ya REDET: Utafiti mpya wabaini Watanzania hawana imani na mawaziri

inawezekana kikwete akaaminiwa zaidi kuliko chama kwa kuwa wananchi wenyewe wakati walipojibu masuala walichagua hivyo.

hii inaweza kuonyesha kuwa watanzania wengi bado mawazo yetu ni finyu, na kwamba rais hatumchukulii kama ndio mwenye jukumu la utendaji wa chama chake na serikali.
 
Nilisema hapa huko nyuma, FMES na Mtoto wa Mkulima wakaanza ooohh binti Asha wa mipasho, hujasoma- ona sasa wasomi wenzenu wamesema CCM haikubaliki kwa asilimia 80 kama mnavyoendelea kujidanganya. Tena wamewaonea aibu tu, ukweli ni kuwa kwa sasa mnakubalika kwa asilimia 20 tu! Sisi kwenye salun za kike tunajua kwamba kati ya wanawake 10 wanaopenda CCM na serikali yake hawazidi 2. Wengine wanaona Kikwete ni mnafiki tu kama walivyowakina Lowosa na wengine.

Narudia tena kuwakumbusha, mjirekebishe sio kuanza kusema tu kwamba sisi tuna mipasho oooh jina lako linadhihirisha ufinyu wa akili eenn, nyie endeleeni kututukana tu wananchi. Ipo siku mtapata 0% kabisaaaaaa.

Jamani hebu nionyesheni pale mahali Mtoto wa Mkulima aliponitusi niliposema hawakubaliki kwa 80%

Kura za maoni zijazo waangalie kiongozi gani anaongoza kwa kuwa kichwa kitupu, debe shinda. Nani atashinda?

Asha
 
Mwanzo wa ngoma ni nilele. Kutolewa kwa matokeo ya REDET yanayoosha kuporomoka kwa Lowasa na kutokukubalika kwa baraza la Mawaziri ni gia tu ya Kikwete kubadili baraza la mawaziri ndani ya siku chache zijazo. Kwa kisingizio cha miaka miwili ya utawala wake. Kwetu sisi wambea tumeshalishtukia hilo. Hata mfanyeje, hamsafishiki. Mmeoza, tokeni wote....

Badala ya kubadili baraza, Kikwete wafunge Karamagi, Lowasa na Rostam, hapo nitakuona shujaa. Rushwa haishughulikiwi kwa kubadili baraza tu huku unamuacha Mkapa apumzike.

Asha
 
takwimu za redet ni kichefuchefu....huwezi kusema jk ni bora kuliko chama ..wakati yeye ndio rais na mwenyekiti wa chama.....

mawaziri hawawezi kuwa wabovu ..alafu useme rais safii...kwa kuwa anawelea lea ..lazima kuna walakini na ripoti ya redet ingeenda mbali kuhalalisha hilo...

nani asiyejua mukandara...aliyetoa ripoti ya kura za maoni iliyohalalisha ...wizi wa kura utakaotokea 2005...

mukandara hana jipya...

Kwa hii tafsiri waandishi ni kama wanasema timu ni mbaya ila kocha ni mzuri! Wanasahau kuwa kocha ndio anachagua na anapanga wachezaji na yeye ndio anafundhisha style ya kucheza.

Sasa kocha anaweza kuwa kuwa mzuri katika kufundisha lakini kama asipokuwa na msimamo kuhakikisha mafunzo yake yanafuatwa kila mchezaji ataonyesha show yake! Na mashabiki tunasema Huyu kocha hatufai!
 
Nilisema hapa huko nyuma, FMES na Mtoto wa Mkulima wakaanza ooohh binti Asha wa mipasho, hujasoma- ona sasa wasomi wenzenu wamesema CCM haikubaliki kwa asilimia 80 kama mnavyoendelea kujidanganya. Tena wamewaonea aibu tu, ukweli ni kuwa kwa sasa mnakubalika kwa asilimia 20 tu! Sisi kwenye salun za kike tunajua kwamba kati ya wanawake 10 wanaopenda CCM na serikali yake hawazidi 2. Wengine wanaona Kikwete ni mnafiki tu kama walivyowakina Lowosa na wengine.

Ni jambo la kushangaza kama CCM inapendwa tu kwa 20%?, Kwa hiyo tunatakiwa kuamini kwamba upinzani unapendwa kwa 80%, sasa kwa nini CCM ndio iko madarakani???...

This is a big challenge to vyama vya upinzani, hivi kuna-opportunity kama hii ya kuongoza nchi inawezakutokea tena kama haya yanayosemwa ni kweli?

Kumbuka bahati haiji mara mbili!!!
 
Maana ya hizi takwimu ni kuwa rais ameshindwa kazi ya kuongoza nchi.

Mpaka kieleweke
Conclusion yako iko sawa ila mie nadhani niongeze kuwa huyu JK, hajui kitu na si tu kwamba imemshinda bali haiwezi.
Kuna tofauti ya kushindwa kitu kwa sababu ya kukosa nyenzo nk,lakini wewe mwenyewe ukawa unaijua kazi.CCM walimuweka pale si kwa ajili ya kuja kuwatumikia watanzania!! Walifanya hivyo kwa kuwa ni mtu pekee ambaye waliona angeweza kuwaletea ushindi bila kujali uwezo wake.
Hii nchi inahitaji mtu asiyetetereka katika kuchukua maamuzi mazito na uwezo wa kuyasimamia katika kuyatekeleza na si bla bla. Magufuli ni 100 times better than JK in any sense.
 
Hata kama REDET wanaboronga, lakini angalau kwa sasa wameonyesha ukomavu kidogo na sura halisi ya mtazamo wa Watanzania. Suala la waandishi wa habari kupindisha mambo kwamba Kikwete anakubalika lakini wasaidizi wake hawakubaliki mie nalipinga pia, kama wachangiji wengine walivyopinga. Spedi lazima iwe Spedi, haiwezi kuitwa kijiko kikubwa! Najua baadhi ya wamiliki wa vyombo hivi na wahariri ni wanachama wa sisi M, lakini lazima wafuate maadili ya kazi.
Naona REDET wamejirekebisha kidogo mwaka huu, unajua mwaka juzi walipondwa kwa kupiga kampeni badala ya kutoa matokeo.
Ni wakati mwafaka kwa mkuu kukaa na kutafakari kuwa kajikwa wapi. Bila shaka aje hapa JF achukue "DESA" ajue pa kuanzia, ili kuweka mambo sawa na kurejesha imani ya Wadanganyika!
 
Nashukuru kipendi hiki REDET wakuwa rafiki wa wanaJF wengi, tofauti na wakati mwingine wote!!!
 
Nashukuru kipendi hiki REDET wakuwa rafiki wa wanaJF wengi, tofauti na wakati mwingine wote!!!
Kilitime na mimi ni matumaini yangu kwamba sasa umejionea mwenyewe wananchi(kwa mujibu wa sample space yao)walivyotoa dukuduku lao, hata kama wangechukua JF kuwa ndo sample space ya kufanyia hiyo experiment yao nadhani wasingepata matokeo tofauti sana na hayo, japo nadhani Muungwana angepata Maksi chache zaidi
 
Ni jambo la kushangaza kama CCM inapendwa tu kwa 20%?, Kwa hiyo tunatakiwa kuamini kwamba upinzani unapendwa kwa 80%, sasa kwa nini CCM ndio iko madarakani???...

Mh. Kilitime
Fanya kautafiti kako kadogo,jaribu kwenda hapo mjini ongea na watu wengine mbalimbali ambao huwajui.Waulize kuhusu CCM wanaionaje? Watakwambia ni bomu la kutupa. Kisha waulize kwanini hawaiondoi madarakani watakwambia CCM haiwezekaniki
Suala hapa ni kuwa Watanzania wamekwishaichaoka CCM,lakini waklati huohuo wamekwisha jikatia tamaa katika kuiondoa,kutokana na mbinu zake chafu.Mtu unamuuliza anakwambia mie siendi tena kupiga kura kwani kura yangu haitobadili kitu.Kwa ufupi "HAITOBADILI MATOKEO AMBAYO TAYARI YAPO"
 
Kwa hii tafsiri waandishi ni kama wanasema timu ni mbaya ila kocha ni mzuri! Wanasahau kuwa kocha ndio anachagua na anapanga wachezaji na yeye ndio anafundhisha style ya kucheza.

Sasa kocha anaweza kuwa kuwa mzuri katika kufundisha lakini kama asipokuwa na msimamo kuhakikisha mafunzo yake yanafuatwa kila mchezaji ataonyesha show yake! Na mashabiki tunasema Huyu kocha hatufai!

Hili sio jambo jipya hapa duniani? Wananchi wanaweza kumpenda Rais lakini wasipende baraza lake!!!

Kwa maana nyingine watu wakisema baraza la mawaziri sio zuri... ndio sababu kubwa zinasababisha baraza la mawaziri ku-be-disolved...

Kwa hiyo sio kitu cha kushangaza kutokea...
 
Mh. Kilitime
Fanya kautafiti kako kadogo,jaribu kwenda hapo mjini ongea na watu wengine mbalimbali ambao huwajui.Waulize kuhusu CCM wanaionaje? Watakwambia ni bomu la kutupa. Kisha waulize kwanini hawaiondoi madarakani watakwambia CCM haiwezekaniki
Suala hapa ni kuwa Watanzania wamekwishaichaoka CCM,lakini waklati huohuo wamekwisha jikatia tamaa katika kuiondoa,kutokana na mbinu zake chafu.Mtu unamuuliza anakwambia mie siendi tena kupiga kura kwani kura yangu haitobadili kitu.Kwa ufupi "HAITOBADILI MATOKEO AMBAYO TAYARI YAPO"

Lakini sample yako ya hapo mjini ni asilimia ndogo sana ya watanzania, hii mambo niliona 95% enzi za mzee wa Kiraracha,,,, kelele nyingi watu hawapigi kura...

JF kengele nyingi, sasa tume ya Richmond wanataka jamaa waenda kutoa ushahidi watu hakuna...
 
Nilisema hapa huko nyuma, FMES na Mtoto wa Mkulima wakaanza ooohh binti Asha wa mipasho, hujasoma- ona sasa wasomi wenzenu wamesema CCM haikubaliki kwa asilimia 80 kama mnavyoendelea kujidanganya. Tena wamewaonea aibu tu, ukweli ni kuwa kwa sasa mnakubalika kwa asilimia 20 tu! Sisi kwenye salun za kike tunajua kwamba kati ya wanawake 10 wanaopenda CCM na serikali yake hawazidi 2. Wengine wanaona Kikwete ni mnafiki tu kama walivyowakina Lowosa na wengine.

Narudia tena kuwakumbusha, mjirekebishe sio kuanza kusema tu kwamba sisi tuna mipasho oooh jina lako linadhihirisha ufinyu wa akili eenn, nyie endeleeni kututukana tu wananchi. Ipo siku mtapata 0% kabisaaaaaa.

Jamani hebu nionyesheni pale mahali Mtoto wa Mkulima aliponitusi niliposema hawakubaliki kwa 80%

Kura za maoni zijazo waangalie kiongozi gani anaongoza kwa kuwa kichwa kitupu, debe shinda. Nani atashinda?

Asha

However, a good 40.7 per cent of respondents said they ’’approved’’ the performance of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM), while just 19 per cent ticked in favour of the opposition political parties.
 
Hiyo ni kadiri ya Mukandala kada wenu akijaribu kuwavika nguo msiwe uchi kabisa eeeeeeee. Bahati nzuri la kuvunda halina ubani. Mficha ugonjwa, kilio huumbuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Pafuka moshi, ndipo moto utakapowaka. CCM inakubalika kwa 20% tu, kama unabisha kamata watu kumi mtaani waulize utapata jawabu badala ya hawa REDET
 
Tanzania: Local Authorities Most Corrupt, Says Report

The Nation (Nairobi)

5 December 2007
Posted to the web 4 December 2007

Mwanamkasi Jumbe
Dar es Salaam

Local government authorities were the most corrupt institution in 2006, painting an unflattering picture of one of the key organs handling people's welfare, a report released by the Tanzania's Prevention and Combating of Corruption has shown.

Minister of State in the President's Office (Good Governance) Mr Philip Marmo released the quarterly report at a news conference at State House on Tuesday.

"Information and reports from the regional and district offices of the bureau show that local government authorities were the worst performers in corruption indicators in 2006, having the number of highest reported cases of bribery and unethical conduct except in Dar es Salaam," reads part of the report.

According to the report, the second most corrupt entity in the institutions category was the police force, closely followed by the judiciary.

In Dar es Salaam, the top five corrupt institutions were licensing authorities, the police, the judiciary, education, health and lands, Mr Marmo said, adding that the overall performance on corruption was based on the number of allegations reported and bribery allegations received.

According to the report, during the last quarter of 2006 alone, a total of 2642 complaints concerning cases of corruption and unethical behaviour were recorded.

The sources of information were Parliament, the media, letters, non-governmental organisations and other sources, the report indicated.

In Dar es Salaam, the PCCB received more complaints from the public in relation to the licensing authority sector followed by the police and the judiciary, while only two cases were reported against natural resources and tourism in the region, he said.

The two cases were on bribery allegations and unethical behaviour he further stated. The PCCB received only three cases from the public against the Tanzania Revenue Authority.

Sasa Ripoti ya REDET inasema hivi:

Alisema wahojiwa waliosema wanaridhika sana na utendaji kazi wa Baraza la Mawaziri, ni asilimia 20, huku Bunge likiwa na asilimia 21.8 na idadi ndogo pia kwa Jeshi la Polisi (asilimia 24), Mahakama (asilimia 21) na serikali za mitaa (asilimia 32.5).

Huko nyuma TRA ilikuwa inaongoza kwa lawama za Rushwa n.k sasa TAKUKURU chombo cha kuchunguza rushwa ndicho ambacho hakiaminiki kabisa. Tumuamini nani kwenye suala hili?
 
Nimesoma Report ya REDET na maoni ya JF members. Conlusively ni kuwa je REDET walikuwa wanataka ku proove kuwa wananchi hawana imani na serikali ya Vasco da Gama(Kikwete) nina maana Hypothesis yao ilkuwa ni ipi? Maana tunaona tu conculision/matokeo. Pili sample waliotumia ni akina nani? ndiyo mikoa yote lakini je watu wa itikadi zipi? ni raia wote au wana th th m? au ni mjumuiko. SIWEZI KUKOMENT RESULTS bila kujua methodology waliotumia.

Any way ninachoweza kusema ni kuwa haikuhitajika kufanya research ili kugundua kitu ambacho hakipo. Ukweli ni kuwa Kikwete amepoteza umaarufu, hafai, hawezi, hajui kuongoza. Kwani kama mawaziri hawafai ina maana rais ndiye mhimili wao. Je yeye haoni? na kama anaona hawafai je mbona bado wako hapohapo? sana sana anawatishia watu aliowateua kuwa atawasemea kwa wanchi!! Sijawahi kusikia kauli ya mtu asiyejiamini kama rais. Amiri jeshi mkuu. Je alipata shule kidogo ya kujua job specification yake kama rais wa jamhuri ya muungano?

CCM haifai tena lakini uchaguzi ukifika wanashinda kisa, Rushwa, kununua kura kwa wapiga kura wanaonyonywa na kubakia maskini hivyo kuuza uhuru wao. Angalia mkutano mkuu wa ccm wajumbe wanakodishiwa treni maalum, wanalipiwa B and B. NA PESA TASLIM KAMA POSHO. Bado vibahasha vinatembea. je unategemea kura kuwa za haki? NO. Uchaguzi mkuu CCM bado wanakomand majority kwa rough game. Je matokeo hayo yatamnyima Kikwete usingizi? La hasha. je Vijijini wanajua hayo matokeo ya REDET? no bado wanaimba 'Ohh TANU YAJENGA NCHI!!!' Nyerere aaaaa nyerere ajenga nchi. Ohh Kawawa ajenga nchi, Jumbe aaaaaa, TANU YAJENGA NCHI... UKitaka kuamini fanya utafiti vijijini ambako viongozi wa kitaifa hawatembelei mpaka wakati wa kura. sample yako iwe watu wa umri wa mika 50..... Swali ni Nani rais wa Tanzania? dont give them clue majibu uone.... ndipo utajua ni lini CCM itaondoka madarakani.
 
Mh.Maarifa,
Umenifanya nibwatuke kicheko cha nguvu ndani ya Library.Nilishindwa kuvumilia baada ya kujizuia sana nisicheke.
Ka SMS kako kafupi lakini kanguvu kwelikweli na kufurahisha juu.Kana ukweli 200%
 
Inside infor. matokeo ya REDIT mpaka sasa JK na serikali yake Kutoka 80.28% hadi 47.60% mchakato huu bado una endelea sehemu mbali mbali nchini , sehemu kubwa wana tumia simu kuwaambia wahusika kukusanya maooni mikoani watu wengi wanaoulizwa ni makada wa chama husika,na mambo mengine yata malizikia mezani. wananchi wengi wamekata tamaa na ,wanaona hii ni siasa tu,

serikali ya kikwete hina hali ngumu sana wanakiri wanao kusanya maoni ya watu. kwaza ni tuhuma zinazo kabili viongozi wa awamu ya nne na ya tatu.

nitaendelea kuwahabarisha inavyo kwenda mchakato mzima wa kukusanya maoni.

asanteni
 
Back
Top Bottom