Maxence Melo: Vijana Wana nafasi kubwa ya kuzuia rushwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,640
6,315
IMG-20230710-WA0445.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo amesema vijana wana nafasi kubwa ya kupambana na vitendo vya rushwa kwa kupitia mitandao ya kijamii ambayo inakutanisha kundi kubwa la vijana.

Melo amesema hayo wakati akichangia mada kwenye Kongamano la Mapambano dhidi ya Rushwa linalofanyika jijini Arusha, Julai 10, 2023.

Ameongeza kuwa kwa sasa Dunia imekuwa kama kijiji ambapo taarifa inaweza kusambaa kwa muda mfupi, hivyo ni vema mitandao itumike kama nyenzo mojawapo ya kupambana na rushwa.

Source: TBC Online
 
Vijana wenyewe ndio hao walamba asali kama akina Kitenge, Zembwela, Mwijaku hawa ndo waitwa vijana,chini ya hapo wanaitwa watoto wasubiri wakue
 
Kama kuwataja wala rushwa na wanaoomba, basi hapa ndio mahali pake

Yaani ukiombwa rushwa unaamuanika hapa name and shame huenda wakaogopa kuomba maana imekuwa kama haki yao kuomba rushwa

Kweli mtu anajenga nyumba kwa hela za hongo na rushwa
Yaani hao mngegawana matofali tu
 
Write your reply...rushwa tulizoea mahakamani police hao ndyo walikuwa wananuka rushwa leo mahosp hata mashuleni rushwa tupu wananuka.ofisi zote zimeharibika.
 
Back
Top Bottom