Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,106
- 10,178
Katika siku ya kuwazawadia washidni wa stories of change 2023, sherehe zilizofanyika Hyatt Regency, usiku wa Oktoba 7, 2023. Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums alitambuamchango mkubwa wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dr. Doroth Gwajima.
Dr. Gwajima ametajwa kama mmoja wa mawziri ambao wameingia JamiiForums ili kusikia Mawazo ya wananchi, kuelezea baadhi ya vitu na kutoa taarifa kuhusu wizara yake. Jambo hili limechukuliwa kipekee kwa kuwa ni viongozi wachache ambao wako humu kwa majina yao halisi na kuwa verified.
Kwasababu sawa na hiyo, Maxence amemtambua Dr. Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa fedha na mipango kwa kushiriki na kujibu hoja za wadau ndani ya JamiiForums.
Katika sherehe hizo ambazo zilimpatia Athanas Myonga Tsh. Milioni 7 kwa kuwa mshindi wa kwanza, ndugu yetu maarufu humu JamiiForums Mshana Jr, pia alitajwa na Maxence Melo. Mshana ni kati ya wanachama walioalikwa kwenye shughuli hiyo Kwenda kula bata. Alipiga suti kali na tai ya buluu Kwenda sawa na mazingira.
Nadhani Mshana amejijengea heshima kubwa ndani ya JF na nje ya JF ndio sababu ya JamiiForums kumualika katika shughuli zake. Suala kama hili ni wito kwa wanachama wengine kuwa wazuri ili kupata fursa za kuinteract na wadau wengine kujenga connections.
Aidha kuhusu mada yangu kuu nadhani ni vyema kwa viongozi wengine kujiunga JamiiForums ili kupata Mawazo ya wadau na kushauriana ili wananchi wasione wameachwa Upweke.
Kutoka Morogoro Ndanindani (Nimerudi baada ya kula kuku wa Stories of Change 2023). Ni mimi Analogia Malenga