The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 389
- 1,166
Habari kaka? Sisi ni wazazi wa watoto wanaosoma shule ya msingi JK Nyerere, iliyopo Manispaa ya Moshi. Mwaka jana uongozi wa shule uliitisha kikao cha wazazi na kueleza nia ya serikali ya kuigeuza shule hiyo kuwa ya mchepuo wa kiingereza (English Medium school).
Katika kikao hicho wazazi tulihoji hatma ya watoto wetu wanaosoma hapo. Tukajibiwa hakuna athari zozote zitakazotokea kwani wanafunzi wa darasa la pili hadi la 7 wataendelea na masomo yao katika mchepuo wa Kiswahili, isipokua wale watakaodahiliwa darasa la awali na la kwanza ndio wataanza na mchepuo wa kiingereza.
Lakini jana tumepigiwa simu kwamba kila mzazi mwenye mtoto shuleni aende akajaze fomu ya kumhamisha. Tukauliza kwanini wahamishwe wakati tuliambiwa wataendelea na masomo hapohapo. Na kwanini iwe ghafla hivi? Tukajibiwa DEO amesema watoto wote waondolewe.
Tukampigia simu hakupokea. Leo tumefika shuleni tukapewa hivi vikaratasi tujaze ili kuhamisha watoto wetu. Unajaza jina la mwanafunzi, darasa alilopo na shule unayotaka ahamie. Shule nyingi ziko mbali na mtoto atalazimika kupanda gari mbili kufika. Huu usumbufu ni kwa gharama ya nani?
Sisi wazazi tunaona hatujatendewa haki. Kwanini hatukushirikishwa mapema? Kama mpango ulikua ni kuondoa wanafunzi wote si wangetuambia tangu mwaka jana ili wazazi tujipange? Wanakuja kutuambia leo, zimesalia siku mbili shule zifunguliwe, wanataka tufanyeje?
Na bahati mbaya hakuna wa kutusikiliza. Hata ofisi ya Mbunge tumeenda lakini hatujasikilizwa. Tumeomba kikao na Afisa elimu lakini amekataa na kusema maelekezo aliyotoa hayana mjadala. Kama mwanzoni aliitisha kikao na wazazi, kwanini sasa hivi anaogopa kuitisha kikao kutueleza mabadiliko yaliyojitokeza? Kuna siri gani nyuma y pazia?
Hivi mtoto wa darasa la 7 unamtoa leo kumpeleka shule nyingine ataweza fanya vyema? Kwanini hili suala wamefanya kwa mabavu? Halafu kama watadahili darasa la awali na la kwanza tu kama walivyoeleza, hayo madarasa mengine yatatumika kwa ajili ya nini? Je yatabaki wazi kwa miaka 6 ijayo? Si yatageuka magofu? Kwahiyo wameona bora yageuke magofu kuliko watoto wetu waendelee kusoma hapo?
Tunaomba utusaidie kupaza sauti.