MKWEPA KODI
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 28,701
- 71,034
Nasikia kichefuchefu, majipu yenye usaha mwingi yamezidi, mwisho mtumbuaji atatapika
hakuna bodi ;Avunje kwanza board ya TPA,unless otherwise NGUMU SANA.
HUKU UPELELEZI UKIENDELEA!
Nimesoma gazeti moja wanasema kuwa tangu mwaka 2008 wadau wa bandari walikaa na kukubaliana kuwa kama ilivyo kwa TRA nao TPA watumie mitandao ya komputa kukusanya tozo zao. Baada ka kipindi cha kutekeleza haya kufika TPA wakakataa maana walijua hiyo ingeliwaondolea ulaji hivyo wakaendelea kutumia risiti zao.
Alivyopelekwa Dr. Mwakembe pale kupitia juhudi za wadau wakiongozwa na mawakala ndio wakamuonyesha jinsi ufisadi ulivyokuwa unafanyika hivyo akaamuru pesa za TPA ziwekwe moja kwa moja benki na ndio wakayaelekeza mabenki kufungua matawi madogo hizo sehemu. Baada ya kuona hilo limewabana ndio wakaja na hii style ya kucheza na benki.
waliofuatilia kwa karibu wanasema katika malipo yote haya yenye utata, si benki zote zilizohusika bali kuna benki moja ambayo imepelekea haya makampuni 210 kuingia kwenye matatizo.
Tukiamua kuendesha nchi kwa weledi badala ya kulea mitandao ya wakubwa hili swala ni rahisi sana.
Waweke hadharani Vipi? Wao wanalipa hela hazifiki kupasakoInavyoonekana mawakala wanaonewa kwamaana hela imepigwa na watu wa TPA NA TRA kwa kushilikiana na watu wa Bank ,lkn mawakara wao wanaogopa nini kuweka mambo hazarani?inaonekana wote wezi tu
Ngoja Faizyfox aje. Nchi ilikuwa ishakuwa ndaguroHivi waliokuwa wanaisifu serikali ya JK wanajisikiaje leo hii? Au walikuwa sehemu ya huu ufedhuli unaojitokeza sasa?
Kidogo tu JK angelipeleka taifa kuwa 'failed state'!!
Vita ya panzi furaha ya Kunguru. Wasemane tu kwa maana ushirika wao wa kutuibia umekufa. Hili tulilitarajia kuwa lazima watuumbuana tu.
Mawakala wanasingizia kuwa wao walikuwa wakilipa benki lakini wanashangaa kuambiwa hawakulipa.Benki zilizokuwa zukihusika ni CRDB na NMB.
Kwangu ni suala dogo tu kama walilipa ni kesi ndogo tu mkaguzi yeyote ataangalia akaunti mbili tu.YA MTEJA (WAKALA FORODHA) NA YA MLIPWAJI.(Bandari au TRA)
Je, akaunti ya mteja ili-debit?
Je, ya mlipwaji ili-credit?
Na kama alilipa taslimu je akaunti ya mlipwaji (TRA NA BANDARI) ziliingia.
Kama hazikuingia lakini mteja alipeleka PAY SLIP INAYOSEMEKANA KUWA NI YA BENKI yeye ndiye inabidi awasiliane na benki alikoweka kuhusu uhalali wa hiyo payslip kama haikuwa ya ku-foji aliyofoji yeye mteja au karani wa benki.
Kama ni ya kufoji hilo tatizo si la TRA wala BANDARI wao wanatakiwa walipwe chao.
Wanachotaka ni pesa sio maelezo ya SLip sijui ni feki mtatusaidiaje hayo ni ya kati ya benki na huyo mteja hatawahusu Tra wala bandari.
Na kama hawakulipa hizo tozo za Bandari na TRA waliwezaje kuondosha shehena bandarini na taratibu haziruhusu kuondoa shehena bandarini kabla ya kuthibitisha malipo stahiki?
Hivi waliokuwa wanaisifu serikali ya JK wanajisikiaje leo hii? Au walikuwa sehemu ya huu ufedhuli unaojitokeza sasa?
Kidogo tu JK angelipeleka taifa kuwa 'failed state'!!