Mauaji Ya RPC Mwanza, Barlow


"Mjumbe hauawi" nimeandika kile ninachokikumbuka baada ya kusoma hiki kijigazeti nikiwa katika mshangao hivyo hivyo kama wewe Mkuu wangu. Nikajiuliza je kwa kuwa alikuwa katika tuhuma bila mashtaka ya msingi au naye Mkuu wa gereza alipata amri toka kwa wakuu wake amwachie!! Ni maswali ambayo majibu yake inabidi uyajibu mwenyewe wee acha tu. Shukrani kwa kuliona hilo.

Kweli kabisa, majibu yatapatikana kutoka kwa Serikali! Amenichanganya sana kuchanganya madiwani wa CCM na Chadema kwenye njama za kumuua Barlow!
 
na bado....mtandao wote utafumuliwa tu.....wamezoea kuwalaza makamanda toka kaskazin.....wengine waliwafukuza kaz kizembe badae wameshinda kesi zao na hawataki kuwalipa fidia!!! system iko corrupt!!
 
Wamempima akili? Mkuu wa Gereza anaweza kuamru mtu aachiwe?

...Thanx. Ndio kitu cha kwanza nilichojiuliza kuhusu hii Udaku type 'Story'. Cha pili nilichojiuliza ni alijuaje waliomuaa Marehemu hali alikuwa Gerezani na hata alipofunguliwa alikataa kutoka kwa kuogopa kugeuzwa RIP? Tatu nimejiulza, pamoja na yooote hivi Usalama wa taifa,Polisi, madiwani wa CCM...Na Chadema, for Christ sake!!!!! wanaweza wote kukaa pamoja na kupanga mpango kwa pamoja wa kumuua marehemu Barrow????:suspicious:

...Thank You James Hadley Chase for...'Believe This and You Will Believe Anything...'
 
...Thanx. Ndio kitu cha kwanza nilichojiuliza kuhusu hii Udaku type 'Story'. Cha pili nilichojiuliza ni alijuaje waliomuaa Marehemu hali alikuwa Gerezani na hata alipofunguliwa alikataa kutoka kwa kuogopa kugeuzwa RIP? Tatu nimejiulza, pamoja na yooote hivi Usalama wa taifa,Polisi, madiwani wa CCM...Na Chadema, for Christ sake!!!!! wanaweza wote kukaa pamoja na kupanga mpango kwa pamoja wa kumuua marehemu Barrow????:suspicious:

...Thank You James Hadley Chase for...'Believe This and You Will Believe Anything...'

Point of correction kwa mujibu wa gazeti,
Moja aligombea kupitia ccm na mwingine Chadema. Wote ni majambazi ila wa chadema hakushinda. alibwagwa. Kwa hiyo kiukweli kuna jambazi ambaye ni Diwani wa ccm. jambazi aliyegombea kupitia chadema alikuwa amejiunga na chadema ili agombee ili amsaidie jambazi mwenzake. kazi kweli.
 
Mimi nilijua tu mwisho wa siku UWT wataumbuka na bado mengine yako njiani kuhusu kifo cha Mwalimu J K Nyerere.Stay tuning.
 
Wana jamvi habari za asubuhi,

Naomba mwenye updates zozote za mauji ya RPC Mwanza, Barlow au mwenye site ya gazeti la Jamuhuri maana limeandika hiyo habari leo.

will appreciate

yeyote mbaya mauti mbaya ni haki yake,hakuna haja ya kumuulizia as well hata RPC wa iringa namuombea auawe hata kesho
 
Mimi nimesoma Gazeti hili la Jamhuri lakini katika link yao bado hawaja update habari hii, iko ukurasa 2 na 13. Inasisimua sana ukiisoma. Kifupi inasimulia kuwa kuna kijana anayeitwa Mohamed Edward Malele, anasema yeye ni jambazi sugu na ameshiriki katika matukio mengi na anataja tukio moja ambalo hatalisahau kuwa siku moja alikwenda kanisani akamuita mama mmoja, yule mama alivyotoka wakamteka na kwenda kumuua na kunyofoa viungo vyake sehemu za siri, matiti kwa lengo la kishirikina.

Sasa niende kisa cha Barlow, anasema aliipata amri toka kwa polisi, usalama wa taifa na baadhi ya madiwani akamuue Kamanda Barlow anasema kwa kuwa yeye alisha wahi kufanya kazi kwake na anamfahamu alikataa kushiriki kumuua. Anasema walivyoona amekataa wakamsingizia kesi ya ujambazi wa kutumia silaha akaswekwa gerezani. Siku kadhaa baadaye akiwa gerezani alisikia kuwa Kamanda Barlow ameuawa na anasema hakushituka kusikia tukio hilo. Mkuu wa gereza baadaye akaona mashitaka dhidi yake hayakuwa dhahiri kiasi cha kuendelea kumshikilia akaamua kumwachia. Anasema alikataa kuondoka gerezani akiogopa gende la ujambazi huko uraiani litamuua likijua ameachiwa huru. Anadai alipotoka alikwenda moja kwa moja kikosi cha anga cha JWTZ pale uwanja wa ndege Mwanza.

Anadai alipowasimulia wale askari walijaribu kuwasiliana na wabunge kadha bila mafanikio lakini mbunge mmoja aliwaomba wamsafirishe hadi Dodoma. Walimsafirisha hadi Dodoma ili akaonane na ngazi ya juu. Alipofika Dodoma akiwa kwenye lango la Bunge askari walimhoji alikuwa na shida gani, akaanza kuwasimulia yote wakampigia kamanda wa polisi RPC David Misime anye akaamuru aswekwe rumande na arejeshwe Mwanza kuunganishwa na wale watuhumiwa wengine wa mauaji ya Barlow. Taarifa zikafika kwa Pinda naye Pinda akaamuru kijana huyo alindwe ili aweze kutoa picha kamili. Alipowekwa katika hali nzuri kisaikolojia aliweza kueleza ushiriki wa Usalama wa Taifa, Polisi na Madiwani wa CCM na Chadema ambao wako katika genge la majambazi sugu, kuwandio hasa walioshiriki kumuua Kamanda Barlow. Anamtaja mtu mmoja kwa jina moja kuwa ni Muna ambaye anasema huyo inawezekana alishiriki moja kwa moja katika kumuua Barlow. Hadi sasa kijana huyu amepelekwa kusikojulikana kwa ajili ya ulinzi wake ili aweze kufunguka zaidi
Hii taarifa ina utata na nadhani ni uzushi,huyu mtu naweza kukubaliana naye kuwa ni jambazi sugu na Muna ni OCCID wa Mwanza,sasa kama anavyodai ni kweli kuwa aliwahi kumuua mwanamke na kumnyofoa sehemu zake hiyo kesi aliitumikia lini?Murder haina dhamana ,yeye alitokatokaje? au kasikia anatafutwa na Muna?story ya Barlow kuuwawa inajulikana,wauwaji walionyeshwa hadi kwenye TV wakiwa na vielelezo,hadi Radio ya Barlow waliyokuwa wameifukia kwenye matope,sasa hizo story za kutaka kukodishwa kazitoa wapi,pia anadai yeye aliwahi kuwa mfanyakazi wa afande Barlow,sasa hiyo pia inaleta maswali mengi:alikuwa akimfanyia kazi gani?alifanya kazi kwa Barlow kabla au baada ya kuwa jambazi?na je waliomua approach na kutaka amuuwe Barlow walimfuata akiwa mfanyakazi wake au baada ya kuacha/kuachishwa?na kwanini wamfuate yeye?Nadhani yale wliyokuwa wakiyasema wabunge ya waandishi makajanja ndio hayo,inabidi wa digest habari zao kabla ya kuziweka kwenye public consumption
 
......... Taarifa zikafika kwa Pinda naye Pinda akaamuru kijana huyo alindwe ili aweze kutoa picha kamili. Alipowekwa katika hali nzuri kisaikolojia aliweza kueleza ushiriki wa Usalama wa Taifa, Polisi na Madiwani wa CCM na Chadema ambao wako katika genge la majambazi sugu, kuwandio hasa walioshiriki kumuua Kamanda Barlow. Anamtaja mtu mmoja kwa jina moja kuwa ni Muna ambaye anasema huyo inawezekana alishiriki moja kwa moja katika kumuua Barlow. Hadi sasa kijana huyu amepelekwa kusikojulikana kwa ajili ya ulinzi wake ili aweze kufunguka zaidi
Green:
---Hii habari imekaa kiutata...sana.

Kwa nini Kamanda Barlow(R.I.P) alijitengenezea/alitengenezewa maadaui hawa wote? Nikipata chanzo halisi cha uhasama wa Barlowa na wanausalama wenzake...ndipo nitakuwa katika nafasi ya kuthibitisha ukweli wa habari hii.
 
wajenzi makini wa hii nchi wapo njian kuijenga na kuweka msingi imara ya kumkomboa mtanzania its the matter of time
 
Back
Top Bottom