Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 1,039
- 2,031
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa matokeo ya usaili wa maandishi uliofanyika Machi 29 na 30 mwaka 2025 kwa watahiniwa walioomba nafasi za kazi TRA yatatangazwa Aprili 25 kupitia tovuti ya TRA (www.tra.go.tz) baada ya kuwasilishwa na mshauri elekezi NBAA Aprili 23, mwaka huu.
Akizungumzia mchakato huo wa ajira za TRA tarehe 02 Mei 2025 Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu na Utawala Bw. Moshi Jonathan Kabengwe amesema baada ya majina kutangazwa, tarehe 02 hadi 04 mwezi Mei utafanyika usaili wa vitendo kwa madereva na waandishi waendesha ofisi.
Amesema baada ya usaili wa vitendo utafuata usaili wa mahojiano kwa kada nyingine ambao utafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 07 hadi 09 Mei, 2025 ambapo watakaofanikiwa kushinda usaili huo wataarifiwa tarehe 18 Mei 2025 na kuanza mafunzo elekezi tarehe 22 Mei 2025 mpaka tarehe 02 Juni 2025 watakapoajiriwa na kuanza kazi rasmi.
Bw. Kabengwe ameeleza kuwa katika mchakato wa usaili maombi yaliyokidhi vigezo yalikuwa 112,952 yakaongezeka maombi 71 baada ya kukata rufaa na kufikisha idadi ya maombi 113,023 yaliyohusisha waombaji 86,314 na waliofanya usaili wa maandishi ni waombaji 78,544 sawa na asilimia 91 ya waombaji wote, na waombaji 7,770 sawa na asilimia 9 hawakufika kwenye usaili kwa sababu mbalimbali.