Nina siku mbili toka nianza kutumia azam decorder. Kwa kweli remote ni shida. Nilichogundua kwa sasa ni kuwa ascending na descending zinaenda ndivyo sivyo. Ukibadili chanel inaruka kwenda ya mbeeeele sana. Ngoja niendelee kukisoma zaidi hiki kitu...Nimeona Azam wametoa madishi makubwa kuliko yale ya mwanzo waliyoanza nayo.Je kuna tofauti yoyote kwenye ufanisi mwanzo ambaye ametumia haya madishi mapya?
Umeniwahi...yani kipindi cha mvua wangekuwa wanatuchaji nusu ya bei...asubuhi nzima ni hakuna channel iliyotulia...niliwai ku complain wakasema leta fundi akurekebishie...kweli karekebisha baada ya muda tatizo linajirudia sasa hivi nimeshakubali matokeo kuwa TV inaangaliwa kuanzia mida ya jioni...sambamba na hilo kuna hili la mvua....yaani mvua ikinyesha tu mawasiliano yanakata...unakuta unachek program nzuri sasa matangazo yakikata hadi yarudi kipindi kimeisha au hata kama hakijaisha basi unakosa muendelezo mzuri...
azam tunawapenda but shughulikieni haya yanatukwaza
Sisi tunaunga mkono bidhaa za wazawa (kwi kwi kwi) ndio maana tunataka arekebishe...hata Toyota alipoanza waliita Toy Pet wamarekani...leo amekuja kuwashika...Mie azam nimeitupa kule,tumieni Dstv ujinga huo hamna.angalizo kama Salio ni tatizo baki huko huko
watu wakitumia Azam sio kwamba hawana salio ama hawana DSTV. Mathalani mi nnanyo dstv chumbani na Azam sitting room.. Hawa dstv zaidi ya mpira, CGTN na CNN siangaliagi kingine. Movie zao na series ni hizo hizo hata usipoangalia miezi sita ukija angalia ni hizo hizo..Mie azam nimeitupa kule,tumieni Dstv ujinga huo hamna.angalizo kama Salio ni tatizo baki huko huko
Ukweli kwa 100% nami hivyohivyoNi kweli kabisa,ilibidi ninunue remote nyingine mwaka jana june lakini sasa n7na mwezi inazingua
Pole mkuu,Pia Azam watafute tatizo la channel kujihamisha hamisha zenyewe pasipo command ya mtumiaji.unakuta unaangalia Azam two,ghafla kimamuzi kinaamia channel nyingine kabisa.Heshima kwenu wadau
Lengo ka uzi huu si kuwaharibia biashara azam Tv lengo ni kutaka kujua tatizo gani ambalo linafanya hizi remote za kingamuzi chenu kuchanganya mpangilio wake mfano
Unabonyeza button ya kuongeza sauti unashangaa imebadili channel haya unabonyeza button ya kubadili channel unaona inaongeza saut hii kitu nilijua kwangu tu lakini nilipoongea mdau ambaye naye anatumia kingamuzi hicho akasema hata yeye hiyo hali hutokea hivyo sasa jamani tatizo nini mwaka Wa tatu huu ndio naanza kuona mapicha Picha haya nini tatizo
Ni kweli usemayo,mimi wakati mwingine nikiwasha au kuzima AC basi channel niliyokuwa naangalia inachange!Ni kweli kabisa remote zao hazipo poa, inafikia wakati mwingine unawasha taa tu bc remote yenyewe inajibadilisha chanel nyengine.ila naona wamebadilisha sasa hivi wanatoa remote ndefuo tofauti na zile za zamani
Hio mkuu utakua nwenyewe umeweka reminder. Wanayo hio kwenye king'amuzi. Ukitaka saa 2kamili ihamie channel flani inawezekana.Pole mkuu,Pia Azam watafute tatizo la channel kujihamisha hamisha zenyewe pasipo command ya mtumiaji.unakuta unaangalia Azam two,ghafla kimamuzi kinaamia channel nyingine kabisa.
Kinapatikana wapiBora nisubiri Kingamuzi cha Kwese
Mkuu, ulisolve vipi tatizo la king'amuzi?.... Changu pia button hazifanyi kazi, na remote yake nayo inazima tu na kuwasha button nyingine zote hazibadili kitu.........Mimi limoti yangu ililipuka yenyewe na kuungua
bila hata kuwa inatumika. Tatizo kubwa king'amuzi pia ni kibovu hakiwezi kusogea steshen wala kuongeza sauti au kupunguza. Mbaya zaidi ukizima king'amuzi ukiwasha tena unapelekwa azam one na siyo stesheni uliyozimia king'amuzi. Majirani wamenichoka kwa kuomba limoti.